Kwanini mwanamke wa Kiislam kuwa Rais ni kukiuka nguzo za Uislamu?

rudia kusoma vizuri kuendelea kuwa na utawala wa kifalme sio kwenda kinyume na uislam kwa sababu haukatazi hilo
Kwahiyo katika uislamu mwanamke anaruhusiwa kuwa kiongozi and at the same time haruhusiwi kuwa kiongozi?

Maana pamoja na kwamba hizo zote ni nchi za kiislamu lakini hawa wanaruhusu mwanamke kuwa kiongozi na hawa hawaruhu mwanamke kuwa kiongozi, lazima kuna mmoja anakosea na mwingine anapatia.
 
Mimi ushahidi wangu huu,

Jamaa ame backup hoja zake kwa Aya na Hadithi mbalimbali.

Zamu yako na wewe leta ushahidi wako
" لن يُفْلِحَ قَوْمٌ وَلَّوْا أَمْرَهُمْ امْرَأَةً
A people will not succeed who are commanded by a woman."

Hii hadithi tu ingetosha kuwa dalili ya kubatilisha uongozi wa mwanamke, lakini shekhe wako ameitafsiri anavyotaka yeye.

Mtume swallallahu allaihi wasallam aliyasema hayo maneno baada ya kufahamu kuwa Wafursi wanaongozwa na mwanamke.

Sasa shekhe wako ameitafsiri hadithi kuwa inazungumzia mwanamke kukomand jeshi, wapi na wapi?

Plus hata Aya aliyoitaja nayo hivyohivyo na maneno yake ndio mengi kuliko hizo Aya au hadithi au maneno ya wanawachuoni.

Halafu dalili zake nyingi amemuelezea mwanamke akiwa kama mke, na anavyoweza kuwa na mchamgo wa kimawazo kwa mumewe(kama aliyovyo mtaja Ummu Salama -radhwiyallahu a'nha-)

Sasa wapi uislamu umekataza hilo, lakini kulitumia hilo kama hoja kuwa eti mwanamke anweza kuwa kiongozi wa wanaume katika jamii, wapi na wapi?
 
Swali la uelewa,

Kwa nini mama wa kiislamu kuwa rais ni kukiuka mafunzo ya Mtume Muhamadi?

Huu ni uelewa tu, kwa hiyo tujengeane uwezo bila jazba wala kashfa

c.c FaizaFoxy
Waziri mkuu wa Bangladesh na yule aliyemtangulia je hao si waislam tena toka nchi ya msimamo mkali?
Pakistani iliongozwa na waziri mkuu mwanamke Zia na ni nchi yenye msimamo mkali je ulisikia fwatwa???
Haya ni mawazo ya watu walioshiba ugali na dagaa wakakorezea na maji yasiyochemshwa. Au yawezekana ni wale wa Mbichi lakini nazitaka ila sizitaki.
 
Hio hadithi uliotaja ni grade gani? Je ni sahihi ama ipo categorised kama Dhaif?

Je ikiwa Hadith inapingana na Quran tunafuata Hadith ama Quran?

Hawa ni baadhi ya Maulamaa (Scholars) wanaokubali Mwanamke anaweza kuwa Head of state.
1.Mohammed Al Ghazali na Yusuf Al Qaradawi

Humo ndani pia kuna maelezo ya Chain ya hio Hadith.

2. Grand mufti wa Egpty pia anakubaliana na Hio Hoja

Pia kama unasoma kingereza pitia hapa
Yaani wewe ndiye uliyeleta link mwanzo nimeenda kusoma, nimekuletea hadithi ambayo huyo shekhe ameitumia, halafu sasa hivi unaniuliza usahihi wake!!?

Ila hadithi hadithi inapatikana katika Sahihi Al-Bukhari (4425) na pia katika Sunan Annasai, sijui unazungumziaje usahihi wake?

Na unaposema inapingana na Quran sijui unamaanisha nini?

Pia kuhusu mashekhe ulionitajia hapo hiyo inaonyesha wewe ni mtu wa aina gani.

Na mimi ushauri wangu ni kama aliotoa ndugu yangu hapo juu tuendelee kusoma ili tuujue Uislamu wetu vizuri.

Wallahu aa'lam
 
Ni kweli wakitofautiana maulamaa sisi hatuna cha kusema.

Tuishie hapa, dhima yake ni kubwa.
 
Dini kandamizi, waarabu hao waasisi wa utumwa, hivyo sioni ajabu mwanamke kuwa mtumwa wa mume wake
Leta reference 1 tu kuwa Waarabu ndio waasisi wa utumwa. Hawa hapa wote Waarabu?👇👇👇

IMG-20220508-WA0030.jpg
 
Mimi ushahidi wangu huu,

Jamaa ame backup hoja zake kwa Aya na Hadithi mbalimbali.

Zamu yako na wewe leta ushahidi wako
Sio Kila kinachoandikwa kwenye mitandao kina afya kwenye dini,kwamba kinapaswa kiaminike ukija kusoma hapo utakuja kuona kuwa hakuna sehemu mwanamke anaruhusiwa kuwa kiongozi mbele ya wanaume,bali hoja inabaki pale pale na baadhi ya ushahidi ninauweka hapo chini

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ

Men are guardians over women by what Allah has favored some over others and by what they spend of their wealth.

Surat al-Nisa 4:34

Tafsiri ya mwanachuoni juu ya hiyo Aya
أَيْ يَقُومُونَ بِالنَّفَقَةِ عَلَيْهِنَّ وَالذَّبِّ عَنْهُنَّ وَأَيْضًا فَإِنَّ فِيهِمُ الْحُكَّامَ وَالْأُمَرَاءَ وَمَنْ يَغْزُو وَلَيْسَ ذَلِكَ فِي النِّسَاءِ

It means men sustain women by spending upon them and defending them. Likewise, among men are rulers, commanders, and those who wage military campaigns; it is not like that among women.

Source: Tafsīr al-Qurṭubī 4:34

Kauli ya mtume Muhammad
لَنْ يُفْلِحَ قَوْمٌ وَلَّوْا أَمْرَهُمْ امْرَأَةً

A people will not succeed who are commanded by a woman.

Source: Ṣaḥīḥ al-Bukhārī 4163, Grade: Sahih

Zaidi ya hapo mtu ambaye amemfanya kuwa hoja ni mtu ambaye ametumia maneno yake kupingana na huo ushahidi.

Waislamu hatufanyi hoja maneno ya watu wahuni wachafuzi wa dini
 
Mkuu tuishie tu Hapa, Nimekutajia mpaka Majina ya Maulamaa wenye views kwamba mwanamke anafaa kuwa Kiongozi.

Hata aya ulioitaja imezungumzia Ruler, Commander, na Millitary campaigns, Maulamaa wengi wanakubaliana na hili na issue ya Judge (japo wapo wachache wanaohalalisha hili pia).

Ila tunapozungumzia nchi za leo, kukitokea Vita Raisi haparticipate, kwenye kesi mahakamani Raisi haparticipate, kazi ya Raisi ni kama hizi mahusiano na Nchi nyengine, kusimamia wizara zake, na mambo mengine.

Ndio maana views ya kuruhusu unaiona, kuna Comment hapo juu Nimemjibu msonjo wamegawanyisha katika mambo matatu

  1. al-wilayah al-‘amah (general authority,)
  2. al-wilayah al-'udhma al-kubra (maximal or greater authority,) and
  3. al-wilayah as-sughra al-khassah (lesser or specialized authority.)
Soma kwenye views zote 3
 
MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA SUZA NAYE ATOA UFAFANUZI

7 September 2020

Profesa Issa Haji Ziddy - Ufafanuzi, wanawake na Uongozi katika Uislam

Prof. Issa Haji Ziddy ambae ni Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) amesema hakuna mantiki ya kidini ambayo inaweza kumzuia Mwanamke kutokua kiongozi kwa kuwa wanawake wana haki sawa na wanapaswa kuwa viongozi kama walivyo wanaume.

Dr. Issa Ziddy is professor of religious education at the State University of Zanzibar (SUZA).

He obtained his PhD in curriculum development & methodology of teaching from the International University of Africa in Khartoum, Sudan.

His research and publications in Arabic, Swahili, and English concern the history of Islamic education in Zanzibar, Muslim-Christian relations, Gulf-Zanzibar connections, and Islamic teachings on current issues.

He was a visiting scholar in Islamic studies at the University of Leipzig, Institute of Oriental Studies in Germany, Bayreuth University in Germany, and in Northwest College in Wyoming through the Fulbright Visiting Scholar Program.

He has partnered with the government and organizations in Zanzibar seeking to bring Islamic leaders into their work in educating communities on pressing current issues, including gender-based violence, family planning, and positive discipline for children in homes and schools and environmental issues.

Source : TAMWA ZANZIBAR
Anatafuta uteuzi… Prof ukweli anaujua
 
Mkuu tuishie tu Hapa, Nimekutajia mpaka Majina ya Maulamaa wenye views kwamba mwanamke anafaa kuwa Kiongozi.

Hata aya ulioitaja imezungumzia Ruler, Commander, na Millitary campaigns, Maulamaa wengi wanakubaliana na hili na issue ya Judge (japo wapo wachache wanaohalalisha hili pia).

Ila tunapozungumzia nchi za leo, kukitokea Vita Raisi haparticipate, kwenye kesi mahakamani Raisi haparticipate, kazi ya Raisi ni kama hizi mahusiano na Nchi nyengine, kusimamia wizara zake, na mambo mengine.

Ndio maana views ya kuruhusu unaiona, kuna Comment hapo juu Nimemjibu msonjo wamegawanyisha katika mambo matatu

  1. al-wilayah al-‘amah (general authority,)
  2. al-wilayah al-'udhma al-kubra (maximal or greater authority,) and
  3. al-wilayah as-sughra al-khassah (lesser or specialized authority.)
Soma kwenye views zote 3
Hivi huyu jamaa wa vipi huyu? Hivi wewe hujui kuwa Rais ni amiri jeshi mkuu? Halafu hili suala halina khilafu achana na wachumia tumbo. Hakuna mtu anatoa Aya halafu anaitafsiri Kwa mtazamo wake!! Labda iwe hiyo dini ni mali baba yake.
 
Nakuwekea hiyo tafsiri ya kiswahili labda utaelewa.
Umeshaambiwa kuwa Allah anasema wanaume ni wasimamizi wa wanawake. Hapa ilitosha kuelewa Kwa wanaofikiri.

View attachment 2223022
Hatutakiwi kutafsiri Aya kwa utashi wetu mkuu, ndio maana toka mwanzo natumia Maulamaa mbalimbali Kutetea hoja yangu. Si wewe wala si mimi hakuna anaeijua hiyo Aya vizuri kuliko Maulamaa wetu.

Surat An nisaa aya 34 na Hadith ya Abu Bakrah ni Basis ya wanaopinga Leadership ya mwanamke.

Na Suratul An-Naml aya ya 23 mpaka 44, ni Basis kubwa ya wanaoruhusu Leadership ya mwanamke.

Moja ya Maulamaa wanaopinga mwanamke kuwa kiongozi ni Ibn Baazi, ambaye ni katika Maulamaa wa kisalafi (Answari, Wahabi etc inategemea unawajua kwa jina gani) yeye anapinga kwa level zote, Al willay, Khilafa etc.

Moja ya maulamaa wanaokubali ni Mufti wa Zamani wa Egpty kama niliposema Juu ambaye pia Alikuwa ni Sheikh wa Al Azhar university.

“…that a woman occupying a position of leadership over a state (ri’asat ad-dawlah) does not conflict with the Islamic shari’ah. He said that the Qur’an praises a woman’s occupation of such a position when the Lord mentions the Queen of Sheba [Bilqis.] If this conflicted with the shari’ah, the Qur’an would have clarified this when telling the story. Regarding the narration in which the Prophet ﷺ says, “A people who make a woman their ruler will never be successful,” Tantawi says that the hadith was specific to those particular circumstances in the state of Persia; the Prophet ﷺ did not mention this in order for it to be generalized. A woman may therefore be the president of a country, a judge, a minister, an ambassador, or a member of a legislative assembly. However, she absolutely may not occupy the position of Shaykh al-Azhar. This position is exclusively for men since it is imperative for the one who holds it to lead the Muslims in prayer, and the Shari’ah does not permit a woman to do this.”

Ulamaa huyu yeye Anakubali Mwanamke Anaweza kuwa Kiongozi kwa level ya Al willaya ila hawezi kuwa Imam.

Pia Maulamaa wengine kama Yusuf al-Qaradawi na Ali Jum’ah Muhammad ‘Abd al-Wahhab wana view kama Hio hapo juu. Na hoja yao kubwa ni kwamba Nchi zetu za sasa ni al-wilayah al-‘udhma hivyo mwanamke anaweza kuwa kiongozi, hawezi tu kuwa Kiongozi wa al-imamah al-‘udhma kwani yaani imam wa Ummah mzima kama unavyosema Makhalifa wa Zamani ambao walikuwa ni Ma imam na viongozi wa Vita.

Suala la Amri Jeshi mkuu ni utata ndio, ila kwangu ni Ceremonial position zaidi, no way Raisi wa Nchi apigane vita kwa miaka yetu hii.
 
Nakuambia hivi ili kukuzindua, najua wewe itakuwa unajifundisha au umejifundisha dini kupitia kwenye mitandao.
Hiyo dini ni kauli za Allah na Sunna za mtume wake Kwa ufahamu wa maswahaba wa mtume.

Kila kilichokuwa Cha kheri katika dini yetu tumeshatanguliwa na Mtume na maswahaba wake katika kukifanya.

Maswahaba walikuwa na pupa ya kuiendea kheri na hakuna kheri katika dini isipokuwa wametutangulia kuifanya.

Hiyo hoja yako Kama ingekuwa na mashiko isingekuwa isipokuwa jambo hili tungeliona kuanzia huko katika zama za maswahaba.

Katika maswahaba waliwepo wanawake wasomi lakini hawakupata nafasi ya kuwa makhalifa. Badala yake nafasi hizo zilichukuliwa na maswahaba wanaume Abu bakari,Umar,Uthmaan,na Aliy radhi za Allah ziwe juu Yao.

Nakukumbusha tena,hao unaowaona maulamaa wako wametafsiri hizo Aya Kwa ufahamu wao na wamekhalifu ijmaa. Mwisho Kwa sisi ahl Sunna hatumzingatii huyo Yusuf Qardhaw katika wanawachuoni.
 
Hakuna Ulamaa hata Mmoja Aliesema Mwanamke anafaa Kuwa Khalifa, tatizo lako husomi nilichoandika badala yake unarudi kwenye Hoja yako ile ile ya Kugeneralise.

Na nitakurudia na Position Mbalimbali za wanawake Through Islamic History, kuanzia Mtume, Maswahaba, Maimamu wanne etc.
 
Kama sisi waislam tunawaonea tu wanawake basi si sisi mana hata Mungu mwenyewe angeona inafaa angechagua miongoni mwa manabii wake wote hata mmoja tu awe mwanamke

Na jambo hili si kwa waislam tu, tunaona hata wenzetu wakristo hapajapatapo kutokea nabii wa kike na hata wanafunzi 12 wa bwana yesu woooooooooote walikua wanaume

Kwa jicho la Uungu hayo si makosa wala madhaifu kwa kua mwenyezi Mungu anajua zaidi sababu ya hayo na kwake si uonevu...... Lakini kwa jicho la wazee wa ladies first ni unyanyasaji mkubwa waislam tunaoneoana tunaufanya

Qur'an inatamka wazi mwanamke ataongozwa na mwanaume na hii ni katika nyanja zote na kwa wale wanaokiuka wajue wazi si mida watakwenda kukutana na yule aliyewatengeneza
 
Unauthibitisho wa haya unayoyasema?

Na mambo katika uislamu haya make sense?
Yes, mfano wa kutotamani mke wa mwenzio lakini Mohammed alikuwa anabaka wake za watu na hakuna anayeuliza hili, kimyaaaaa.
 
Una Uhakika Na Unayoongea Au Alimbaka Mke Wako Labda.Mtume Alikuwa Anaoa Na Kakataza Uzinifu Sio Kama Huku Kwa Wenzetu Wanapokataza Viongozi Wa Dini Wasioe wala Wasifanye Mapenzi kama Hamuhamasishi Ubakaji au Uzinifu Ni Nini.Hakuna Mwanaume Anayeweza Hivo labda Kama Hanithi Au kama Huwa Mnawaakisi kama Ng'ombe Hapo Sawa
 
Hizi dini ni majanga matupu..zilipaswa vitabu vyake. Vifungiwe museums au vifundishwe kama historia sio kuaminishana.

#MaendeleoHayanaChama
Kwa bahati mbaya hao unaotaka vitabu vyao vifungiwe ndio wametoa wanawake wengi kama maraisi katika nchi za kiaslamu, Pakistan, Banglasesh, Kosovo, Turkey, N.Cyprus,Krygzastan, Indonesia hapo siajweka Tanzania sababu sio nchi ya kiiaslamu. Sasa nenda nchi zenye dini nyingine hapo Italy tu karibu na Vatican basi hata Papa atoke mdada mmoja aitwe Mama. Nchi za kiislamu zina wanawake wengie katika nafasi za juu nchi yenye waislamu 100% Pakistan siasa kali lakini imeongozwa sana na Mama. USA na kelele zote ndio mara ya kwanza kuwa na makumu wa Rais mwanamke.
 
Back
Top Bottom