Binadamu ni kama viumbe wengine tu, ana wivu kama wanyama wengine lakini hana shida kuchangia mwanamke au mwanaume kama walivyo wanyama wengine. Ndiyo maana mwanaume na mwanamke wanaweza kutembea na mke au mume wa jirani, rafiki, boss au mtu mwingine tu wanaemfahamu au wasiomfahamu, ila hawako tayari mke au mume wake yeye aliwe na mtu mwingine. Huu ni wivu tu walionao viumbe wote wakiwemo jogoo, fisi na beberu. Mwanaume wa kweli hamuachi mkewe au mumewe kwa kutembea na mke au mume mwingine, bali atalipiza kwa kutembea na mke au mume mwingine ili kutuliza roho na kumaliza 'kosa'. Msemo wa kitanda hakizai haramu ulianzia hapo, yaani kesi ya mapenzi inamalizwa kwa mapenzi, na kesi ya kucheat inamalizwa kwa kucheat, kesi ya kuzaa nje inamalizwa kwa kuzaa nje, na kesi ya masikini hakimu wake ni Mungu pekee.