Uchaguzi 2020 Kwanini Paul Makonda ametoswa na Patrobas Katambi amepata uteuzi?

Uchaguzi 2020 Kwanini Paul Makonda ametoswa na Patrobas Katambi amepata uteuzi?

Katambi ni kiongozi mahiri ndio maana hata Mbowe alikuwa anamkumbatia.
Hana lolote huyo na wategemee Jimbo kwenda kwa mpizani maana zitapigwa kura za maruhani
Matokeo ya Kura za Moni CCM Shinyanga mjini
matokeo kura za maoni yalikuwa:
1. Stephen Masele - kura 152
2. Jonathan Ifunda - kura 65
3. Gasper Kileo - kura 51
4. Patrobas Katambi 12
 
Siasa bhana hazitabiriki kabisa.

Bado sijavijua vigezo vya kumtosa kijana aliyeipigania CCM kwa jasho na damu Paul Makonda na kumpitisha Patrobas Katambi ambaye mchango wake mkubwa uko CHADEMA.

Namsubiri mnec mzee Mgaya aje anipe ufafanuzi.

Maendeleo hayana vyama!
Ndugulile kashinda kihalali. Hakutoa Rushwa. Makonda alitoa Rushwa.
Shy town number moja mpaka tano wote walitoa Rushwa. Katambi hakutoa Rushwa.
 
Nadhani kilichotokea ni kuwa baada ya makonda kuota mapembe na kumchukulia poa kila kiongozi awe wa chama au serikali isipokuwa rais tu karibu kila mtu alimchoka na wengi kumchukia. Aliendelea kuwa alipo kutokana na kushikiliwa na rais tu ila sasa kajichanganya kaamua kumchukulia poa rais pia kwa kuondoka kwenye nafasi aliyomuweka. So hata rais anaweza kuwa na mapenzi ya ndani kwa mtu lakini pia hua anajali sana maoni ya walio wengi kuepusha sintofaham za baadae. Kina Katambi wanaweza kuwa waliondoka kwenye nafasi walizopewa ila hawakuwaudhi wengi kwahiyo hata ukimpa nafasi tena haiwaumizi wengi.

Lakini pia niliwahi kufikiria scenario flani kwamba kwa makonda alipokuwa amefikia alikuwa kamuudhi kila mtu hadi rais ila kwa jinsi rais alivo hana tabia ya kufanya maamuzi kwa kushinikizwa na mtu ilibidi Makonda atengenezewe mtego ale ndoano wamnyoe. Umeshanichosha, kukutumbua direct itaonekana nafanyia kazi maagizo ya mange kimambi na kigogo so nakutafutia wajanja wakujaze upepo kuwa ulipo ni padogo so kagombee ubunge na kwa kuwa unaamini nina kukubali sana unajihakikishia kushinda. Unachukua form natoa maelekezo upigwe spana katika level zote movie linaisha steringi umefia kwenye maua na lawama kubwa zinaenda kwa wajumbe sio mimi nilieaminiwa ni baba yako.

By the way bado muda upo na mengi yanaweza kutokea so tuwe na akiba ya maneno
 
Hana lolote huyo na wategemee Jimbo kwenda kwa mpizani maana zitapigwa kura za maruhani
Matokeo ya Kura za Moni CCM Shinyanga mjini
matokeo kura za maoni yalikuwa:
1. Stephen Masele - kura 152
2. Jonathan Ifunda - kura 65
3. Gasper Kileo - kura 51
4. Patrobas Katambi 12
Pascal alikuwa wa sita baada ya Gasper kuna wengine wawili then ndo Katambi.
 
Hana lolote huyo na wategemee Jimbo kwenda kwa mpizani maana zitapigwa kura za maruhani
Matokeo ya Kura za Moni CCM Shinyanga mjini
matokeo kura za maoni yalikuwa:
1. Stephen Masele - kura 152
2. Jonathan Ifunda - kura 65
3. Gasper Kileo - kura 51
4. Patrobas Katambi 12
Tutatumia jeshi letu pendwa kumpa Katambi ushindi msukuma mwenzetu
 
Mtu namna hii utamuachaje kwa akili ya kawaida? Endelea
Hivi uzuri wa mtu ni kuweza kuongea sanaaaa. Nauliza kwa kua kajamaa kwa kweli kanaongea sana tu. Na kwa hiyo haka kajamaa ndio kana akili kuliko kila mtu wa upinzani. Kwamba msomi Lissue, msomi Zitto na wengine wote wa upinzani si lolote na si chochote lakini kenyewe ndio kaji smart ass sio?!
 
Daah!nadeclare interest kuwa makonda simpendi,ila jana nlimuona olympc shell igoma anaweka mafuta kweny kagar kake kale hakika anatia huruma,anahitaj msaada wa kisaikolojia maana c kwa lile tamaa alikuwa kashika
 
Watumishi wa umma mateso ya miaka 5 ya hakuna increments, kupanda vyeo (walimu),ongezeko la mshahara,kutolipwa malimbikizo yenu n.k iwe ni fundisho na akili zenu kuikataa ccm kwa nguvu zote.Familia zenu ziikatae ccm.

Msiwapigie kura ya urais,wabunge wala madiwani.Ndiyo wadhalilishaji wenu
 
Makonda ametumiwa tu na kwa kuwa hazichaji kivile akachanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom