Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Ni zaidi ya mwezi sasa hili suala la bandari limeendelea kuwa gumzo, kinyume na matarajio yangu!
Mwanzoni nilidhani lilikuwa ni upepo tu upitao kama yalivyo masuala mengine.
La hasha. Haijawa hivyo.
Kila kunapokucha, gumzo la bandari zetu ndo linatawala vinywa vya wananchi.
Hali hii imenifanya nijiulize maswali kadha wa kadha;
Kwa vile ni gumzo ambalo limeendelea kutawala mazungumzo ya watu kwa muda mrefu [kwa zama hizi za utandawazi, umma kuongelea jambo moja kwa zaidi ya mwezi, ni muda mrefu!], basi ni wazi kuwa wananchi wengi wanaliona kuwa ni suala la muhimu sana.
Sasa kwa nini mpaka sasa Rais Samia hajaitisha mkutano wa habari na waandishi wa habari ili kulizungumzia na kulitolea ufafanuzi na kujibu maswali ya wananchi?
Badala yake, ni kama vile kajificha nyuma ya makada wa chama chake pamoja na baadhi ya wateule wake serikalini ambao wao ndo wamejaribu kulizungumzia, lakini kila wafanyapo hivyo, wanaishia kuzua maswali mengi zaidi.
Ni kwamba hana taarifa za kutosha za kumwezesha kulizungumzia hilo suala mbele ya waandishi wa habari?
Au hajiamini kuongea na waandishi wa habari?
Come on Samia….talk to the press [and the nation].
If everything is above board….is on the up and up, it shouldn’t be that difficult for you to talk to the press and take their questions.
Ona huyu alivyokuwa anakabiliana na waandishi wa habari wa kimataifa…