Kwanini siku hizi wanandoa wengi hawapendi kuvaa pete za ndoa?

Kwanini siku hizi wanandoa wengi hawapendi kuvaa pete za ndoa?

Kuna jambo linanitatiza sana maana nimefanya research kiasi nikuwa huko mikoani na hata nilipofika huku Dar hili nimeliona sana.

Kwa mujibu wa utafiti wangu nilioufanya kwa kiasi toka miaka ya 2000 wanandoa wengi japo sio wote hawaonekani kuwa na pete za ndoa kwenye mikono yao, nilijaribu kuuliza baadhi ya wanandoa upande wa jinsia ya Me wengi walitoa sababu mbambali japo nyingi hazina mashiko na Kwa jinsia ya Ke ni hivyo hivyo.

Nimejaribu kutafakari ila naona kama kuna sababu zingine zenye uzito zaidi ambazo zinawafanya wawe si watu wa kuvaa pete za ndoa japo wanaishi wote kama wanandoa na wengi wakiwa sawa tu.

Hii kitalaamu imekaaje wajuvi mje mnifundishe Je, kuvaa pete ya ndoa ni Ushamba? Au si kitu cha maana kwenye utamaduni wetu sisi waafrika?


Sio wana ndoa
 
Mkuu, kwa hiyo sisi tunaopinga kuvaa pete tuna letu jambo? Tunajificha tusionekane kama tumeoa. Hivi kwa umri wangu nikikutana na mdada nina haja ya kumwambia nimeoa/nina mke?

Binafsi sioni tija ya pete, kiimani kwangu haina nafasi yoyote, nikiamua kucheat pete haiwezi kunizuia.
Kwa kifupi tu mueleze tunawala na Pete zao za ndoa vidoleni.
 
Mi naona wanawake wanavaa ila wanaume nadra sana labda watu wazima sana.
Wanaume wanataka uhuru wa kuchepuka anytime, mambo ya kuulizwa

"Jamani, yaani wewe unanitongoza na naona Pete ya ndoa kidoleni hapo vipi?" Hatutaki
 
Sio lazima, kikubwa wanandoa kuaminiana.Hayo mengine Ni mbwembwe tu.
 
Back
Top Bottom