Tokea tarehe 22/04/2020 Rais wetu, John Magufuli, alipofanya kikao maalum na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, kuhusiana na ugonjwa wa COVID 19, tumeshuhudia kimya kizito kwa upande wa mamlaka za utoaji taarifa wa Tanzania Bara ya maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo
Tukumbuke pia katika kikao hicho tulimsikia Rais wetu, akipiga "mkwara" mzito, kuwa haridhishwi na namna taarifa zinazotolewa na wizara ya Afya, kuhusu maambukizi mapya na vifo vinavyotokana na ugonjwa huo wa corona
Tulishuhudia pia akifanya "mini reshuffle" kwa kumwondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa wizara ya Afya na kumteua mwingine
Tumeshuhudia waziri wa Afya, Ummy Mawalimuambaye amekuwa akitupa "updates" za ugonjwa huo, akipata ghafla "kigugumizi" baada ya kikao hicho cha Mheshimiwa Rais kwa kutoweza tena kutupa taarifa zinazohusiana na ugonjwa huo
Ndipo hapo tunapomuuliza waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, nini kimekutokea hadi usitishe kutupa "updates" za maendeleo ya ugonjwa huo nchini?
Tunashuhudua kwenye nchi jirani za Zanzibar, Kenya na nchi nyingine za mbali za Uingereza na Marekani wakitoa "updates" za ugonjwa huo kila siku.
Tunafahamu pia kuwa Taifa la Tanzania limetoka kwenye maombi mazito ya kumlilia Mungu wetu atuepeshie na janga hili la corona.
Tunadhani ni muhimu sana kwa wananchi kuendelea kupewa "updates" za ugonjwa huo za kila siku, kama yafanyavyo mataifa mengine.
Ikiwa hakuna maambukizi mapya wala vifo, basi ni vyema waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akawa anatipatia "daily briefing" na sisi wananchi turejeshe utukufu kwa Mungu wetu, kwa kutuondolea janga hili la corona
Kwa kuendelea kukaa kimya kwa serikali, kunatoa mwanya kwa wananchi wasilitakia mema Taifa letu, kwa kutangaza wao taarifa wanazozijua wao za maambukizi mapya na vifo vinavyotokea nchini kutokana na ugonjwa huo wa corona
Naziomba mamlaka zinazohusika za wizara ya Afya zitujibie utata huu wa suala nyeti sana la ugonjwa wa corona hapa nchini, ili sisi wananchi zituondolee hofu kubwa inayotukabili hivi sasa kuwa wananchi wa Taifa hili, hususani wa Jiji la Dar, wanapukutika kwa wingi sana
Ni lazima pia tuwajulishe watawala wetu kuwa kupewa taarifa za maendeleo ya ugonjwa huu wa corona siyo hisani kwa watawala wetu, bali ni kitu cha LAZIMA kwa wananchi wake