Kwanini Tanzania hakuna daily briefing juu ya Corona virus pandemic?

Mzee baba keshasema "wewe Ummy hakuna kutangaza idadi ya wagonjwa tena uliotangaza yatosha acha waendelee kujifukiza huko"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: sab
Wapo mbioni kuibadili jina isiwe tena homa ya mapafu waiite, "Changamoto ya upumuaji"

Nina taarifa ya wagonjwa wawili wa changamoto ya upumuaji walioondokea Darisalama jana usiku kuelekea Chattle, na mwingine "intentionally" kaondokea leo asubuhi uelekeo ni huo huo chattle kuambukiza kwa "makusudi" wale waliokimbilia huko kujificha
 
Madam Ummy yupo kwenye mfungo, msije mkamharibia funga yake kwakutaka awape data za uongo. Ni bora kukaa kimya kuliko kuongopa saizi akitoa mjue anatoa taarifa halisi na sio za wagonjwa 108 kupona ndani ya Siku moja baada ya hotuba.
 
BBC ndo nani kwanza?waache kufuatilia mambo yetu!sie hatuna mgonjwa mpya,na waliopo wanaendelea vizuri mpaka wanafanya besidei kama sio dethi day hospital!

Hao wananchi wakitaka kujua maendeleo ya corona hapa kwetu,waende wakaulize wizara ya afya ya Uganda!hapa ni mwendo wa kujivukizia tu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzuri ni kwamba Corona ni sawa na mimba huwezi ficha, watu wameshaanza kufia mitaani na barabarani huko. Serekali itaumbuka tu!
 
Kuongoza watz ni sawa na kuongoza maiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu amejibu maombi tunapona kwa kujivukiza.Mungu tunaomba iponye Tanzania.
 
Madam Ummy yupo kwenye mfungo, msije mkamharibia funga yake kwakutaka awape data za uongo. Ni bora kukaa kimya kuliko kuongopa saizi akitoa mjue anatoa taarifa halisi na sio za wagonjwa 108 kupona ndani ya Siku moja baada ya hotuba.
serikali haina dini.
 


Tunaambiwa tusizurure bila sababu ya msingi ili kukwepa maambukizi , lakini idadi ya wagonjwa wapya hatuambiwi ! kiongozi anakufa tunaambiwa atazikwa na watu 10 tu bila hata maelezo ya ziada , huku baadhi ya marehemu wengine wakizikwa na zaidi ya watu 10 !

Nchi zote zinazotuzunguka zinatoa taarifa mara kwa mara kuhusu maambukizi ya corona kiasi kinachowahamasisha wananchi wake kujilinda zaidi , sasa pita mitaa ya DSM
ujionee mwenyewe misongamano isiyo
na tahadhari yoyote ile.

Ambulance zimeongezeka mitaani utadhani kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe , huku imechukua maiti kule imechukua mgonjwa , hali hii inaleta Taharuki kwa wananchi kiasi cha kuleta hofu kubwa sana .

Hapa Tanzania serikali ina mpango gani , kwanini imeacha mambo hewani tu ili kila mtu aseme lake?
 
Umeshaambiwa " wengi".............uwe unaelewa bwashee!
 
Subiri ikikupata utajua takwimu zote wapya na wazamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…