Mambo mengi watu wanafanya kiujanja ujanja!
Kipindi cha Sea tax za azam zilipoanza kutoa huduma kwa zaidi ya miezi 4 kienyeji; tulihoji humu hao azam wako pale kwa mkataba gani wa kiserikali? (Hata kama walikuja kutoa msaada ni jambo zuri lakini kwa mkataba gani?) (Watu wa procurement watanielewa zaidi)
Hawakuwa na majibu yoyote zaidi ya kusema ni msaada.
Lakini kwa mujibu wa sheria za usafilishaji! Walikuwa wanamakosa makubwa!
Siku tatu baada ya kuhoji hilo wakaenda kutangaza tenda ya sea tax huko TANEPS!
Na wakaweka vigezo vyote vya azam hadi rangi ya TAX, yaani kiufupi ni kwamba hata angekuja mwingine asingepewa! Yote kheri!
Matengenezo ya MV magogoni
Hiki kivuko kiliundwa kipya kwa 7.5bil
Hata kama kuna ongezeko la shilingi haliwezi kuzidi 70% ya bei ya awali! HAIWEZEKANI
Ufafanuzi wanadai kwamba kwa sasa vifaa vimepanda kwamba ingekuwa kukisuka upya Leo kingegharimu 25bil yaani ni uongo wa standard gauge!
Labda watu tueleweshane vizuri!
Marekebisho ya MV magogoni iliyoundwa mpya kwa 7.5bil yanagusa sehemu zifuatazo
1. Kuondo vipande vya Bati (ungalvanise sheet) ambayo bei ya square meter moja ni around 1mil; kipande cha mbele na nyuma ambacho ni kibovu hakizidi square mita 100 >Fanya iwe Mara tatu yake potelea mbali ni 300 mil
2. Engine mbili mbovu! ( lina engine 4) hapo kuzikarabati kila moja ni 100mil sasa tufanye kuziondoa zote kabisa tufunge mpya 400mil jumla 1.2bil
Na hapo ikumbukwe injini za MV Magogoni zilikufa kwa tabia ya kubana mafuta, yaani badala ya kuendesha kwa kuwasha injini zote, walikuwa wanazima mbili hivyo lilisukumwa na injini mbili tu kiasi ya kuzifanya zife mapema!
3. Kupuliza rangi 100mil inatosha
4. Marekebisho ya umeme Fanya unanunua vifaa vipya 300mil
5. Yale mabenchi ya mbao juu chini wape 100mil
6. Yale maboya na makorokoro hayazidi 50mil
Jumla ya mambo hapo 2bil sasa ongezea mafuta, escort na miundombinu wezeshi kama crane haiwezi maliza 300mil
Only 2.3bil ambapo kwa mkandarasi wampe 3.5bili tena anabakiwa na faida kibao ambayo angeweza tengeneza MV kigamboni kama asante!
Na hayo ni mahesabu ya juu sana!
Yameleta only 2.3bil
Sasa hiyo wanayosema 8.9 bil Kurekebisha wana rekebisha nini jaman!
Songoro marine na wenzake waliopo tanzania waliwezaje kuunda inakuwajre Leo washindwe kukarbati?
Wekeni tenda wazi gharama za ukarabati haizidi 3.5 billion
Kama VIVUKO Siyo sehemu ya upigaji si bora mjenge daraja la chini ya maji kwa 350bilion kuondoa kero ya kudumu ?
Namna ya kulijenga daraja niliwahi kuainisha hapa
Historia ya mji wa kigamboni ilikuwa shamba, kama ilivyokuwa mbezi beach na maeneo mengine yaliyokuwa pembezoni mwa mzizima (Dar) Mawazo ya kuleta kivuko pale kigamboni yalilenga tiba ya dharula kwa wakati huo teknolojia ilikuwa haijasambaa duniani! Hivyo matumizi ya kivuko siyo usafili wa...
Hamuoni hata huruma roho za watu zinavyoeelea hapo kila Siku miaka nenda miaka rudi jaman