Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Songoro anatengeza vivuko hadi vya Uganda au huna taarifa?Labda Songoro hawana utaalamu wa kukarabati MV Magogoni ndio maana amepewa Mkandarasi wa Nje ya Nchi
Sio lazima Songoro angepewa Kampuni yoyote ya kitanzania yenye uwezoKwani songiro yeye nani .
Mbna makampuni saiv kibao tu kila deal yeye na sisi tutatusua vipi.
Kwa dau Hilo inasikitisha kweli ila mmamshabikia sana huyu songiro utazani yeye ndo anazitengezaga fresh.
Hapo ni sahihi kujiuliza na ni muhimu sana lakini kumbuka kosa halirekebishwi kwa kosa na ukumbuke hii nchi ya Watanzania na wala sio ya Jiwe.... hizo ni fedha tunazolipa kodi mimi na weweTupate jibu hili kwanza,ni kwanini kipindi cha awamu ya tano tenda zote za kutengeneza/kukarabati vivuko na meli zilikuwa hasitangazwi na zote alikuwa akizifanya SONGORO MARINE tu?!!tukipata jibu hili kwanza ,itakuwa rahisi kujua huwa ni nini kinatokea.
Hii mirangi ya Kijani nayo daahBILIONI 7.5 KUKARABATI KIVUKO MV. MAGOGONI
![]()
Posted On: February 16, 2023
Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) leo imesaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV. MAGOGONI wenye thamani ya shilingi Bilioni 7.5. Mkataba huo umesainiwa leo katika eneo la kivuko cha Magogoni Kigamboni jijini Dar es Salaam kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Lazaro N. Kilahala na mkandarasi African Marine and General Engineering Company Ltd.inayotoka Mombasa nchini Kenya na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo, Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb), Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge, Wakuu wa Wilaya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa amesema ukarabati wa Kivuko cha MV. MAGOGONI ni juhudi na mikakati ya Serikali katika kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafirishaji nchini na kuongeza kuwa ukarabati huo utakapokamilika utaharakisha na kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa wananchi waishio katika Wilaya ya Kigamboni, Ilala na maeneo mengine
’’Madhumuni ya ukarabati wa kivuko hiki ni kuhakikisha huduma inayotolewa na kivuko hiki ni salama kwa watumiaji na hivyo kuwaondolea wananchi kero ya usafiri inayotokana na kuchakaa kwa kivuko hiki.Kivuko hiki kilijengwa mwaka 2008 na kina uwezo wa kubeba Tani 500 yaani abiria 2000 na magari madogo 60 na ni kiunganishi muhimu kati ya maeneo ya Wilaya ya Kigamboni na Wilaya ya Ilala.’’ Amesema Profesa Mbarawa na kuongeza kuwa wakati umefika sasa wa kivuko hicho kufanyiwa ukarabati mkubwa.
’’Wakati kivuko hiki kinafanyiwa ukarabati kutakuwa na changamoto ya usafiri, kwahiyo niwaombe sana wakazi wa Dar es Dalaam hasa maeneo haya watumie kwa wingi Daraja la Nyerere ili kupunguza msongamano katika kivuko hiki, amesema Profesa Mbarawa na kuongeza kuwa wakati wa kutoa tenda Serikali inaangalia mambo mawili makubwa, ’’Jambo la kwanza tunaangalia bei, nani ni mwenye gharama za chini, kama alivosema Mtendaji Mkuu TEMESA, mkandarasi ambaye alikuwa na bei ya chini ilikuwa ni bilioni 7.5, aliyemfuatia wa pili alikuwa na bilioni 10, tofauti ya bilioni 2.5, kama hii ni pesa yako wewe utampatia nani mkataba wa kazi hiyo? Nawaachieni mjibu,’’ alimaliza Profesa Mbarawa.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu akizungumza katika hafla hiyo amewaomba wananchi wa maeneo hayo kuvumilia changamoto ya kukosekana kwa kivuko hicho wakati kitakapokuwa kwenye matengenezo kwa kuwa matengenezo hayo yanalenga kuleta huduma bora na kivuko hicho kuwa salama kwa ajili ya kutumiwa na wananchi hao.
Naye Mbunge wa Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza katika hafla hiyo ametoa rai kwa Serikali kutoa fursa kwa sekta binafsi kuruhusiwa kuanza kutoa huduma ya kivuko katika eneo hilo.
Aidha, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Lazaro N. Kilahala akisoma taarifa fupi ya mradi huo amesema mkandarasi African Marine and General Engineering Company Ltd. Ataanza rasmi ukarabati wa kivuko hicho mara baadaa ya kulipwa malipo ya awali na anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo ndani ya miezi sita.
’’Kivuko cha MV. MAGOGONI ni Tegemeo kubwa kwa wananchi wa Kigamboni kutokana na uwezo wake wa kubebea abiria na magari mengi kwa wakati mmoja hivyo ukarabati huu utawezesha kivuko hiki kutoa huduma ya uhakika na tija kwa wana Kigamboni.’’ Amesema Mtendaji Mkuu na kuongeza kuwa kazi ya ukarabati wa kivuko hicho itahusisha kazi za chuma, kuondoa mabati yaliyochakaa ya muundo wa chini na wa juu, ujenzi wa milango mipya ya kushushia na kupakia abiria, ukarabati wa chumba cha kuongozea kivuko, ufungaji wa injini mpya nne aina ya Caterpillar pamoja na gia boksi zake, matengenezo makubwa ya pampu jeti, marekebisho makubwa ya mfumo mzima wa umeme na elektroniki wa kivuko, kufungwa kangavuke (majenereta) mapya mawili, matengenezo ya mfumo wa tahadhari ya moto, kufunga kamera za CCTV, kuweka vifaa vya kisasa vya kuongozea kivuko, vifaa vya tahadhari na vya uokozi, pamoja na kupaka rangi kivuko chote.
Mtendaji Mkuu alimaliza kwa kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa kukubali kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo na miradi mingine na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na jitihada kubwa ili kufikia malengo na matarajio ya Serikali na wananchi kwa ujumla.
Watu elfu 2 inabebea wap shekhe?We jamaa uko timamu kweli? Kivuko kile hakiwezi kuchukua watu 2000 at per??
We weka hapa thamani ya kivuko kipya chenye capacity kama ya Magogoni.
Watanzania mnapenda kulaumu na kuonekana nyie ndio wenye uelewa kuliko wataalam wenyewe.
Wametoa sababu hii hapa na naona ni logicalWadau nawasabahi.
Nikiwa mlipa kodi pamoja na tozo mbalimbali najisikia uchungu sana kusikia kuwa Serikali inataka kukarabati kivuko cha Mv Magogoni kwa bil.7. wakati bei ya kuunda kivuko kipya ni kati ya bil.8.5 -9
Najiuliza kwanini ufanyike ukarabati?
Kwanini kisinunuliwe kivuko kipya?
Hata kama kununua ni gharama lakini tofauti yake ni ndogo sana. Hebu watendaji wa serikali tuwe na uchungu na kodi za masikini wananchi wananchi wana maisha magumu sana hata kama mnatuamulia mtakavyo lakini tunaumia tunapohisi mnatuibia.
Juzi juzi mmetoka kutuibia kwenye ukarabati wa mv hapa kazi mlikikarabati kwa bil.4.5 wakati kivuko kipya ni bil 7.5 kumbukeni watanzania sio wajinga kihivyo
Ni sawa,lakini haya mambo kama mna katiba nzuri ambayo inalifanya bunge kuweza kuisimamia serikali ipasavyo yasingekuwepo.Shida inaanzia pale jitu zima tena lisomi linasema KATIBA HAIWEZI KUKULETEA CHAKULA MEZANI!!!Kuna mambo yanafanyika Afrika hadi mtu unajiuliza hivi hiki kiumbe (Mwafrika mweusi)kilitoka wapi?!!Hapo ni sahihi kujiuliza na ni muhimu sana lakini kumbuka kosa halirekebishwi kwa kosa na ukumbuke hii nchi ya Watanzania na wala sio ya Jiwe.... hizo ni fedha tunazolipa kodi mimi na wewe
Unalia mapema mno, lakini ni haki yako.Kwanini watanzania wengi wameshtuka kuhusu ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni cha kwa gharama za Bilioni 7.5 kwenda kukarabatiwa nchini Kenya.
Lakini ukipitia Tovuti ya TEMESA kwenye eneo la Zabuni hakuna mahali ilipotangazwa zabuni ya kukarabati wa Kivuko cha MV Magogoni.
Lakini nimepitia pia kwenye Account ya Instagram ya Mbunge wa Kigamboni, Dk Ndugulile naye hakuna post aliyoweka kuhusiana na ukarabati wa kivuko hicho.
Yote haya yanakuza mjadala kwanini asipewe Songoro Marine kukarabati kivuko hicho hapo nchini hadi kipelekwe Kenya?
Wajuzi tuendelee kujifunza
"...hakuna tatizo", kwa "mtu kupewa tenda bila kufuata mchakato", kwa vile tu "Rais alisharuhusu".Rais alisharuhusu mtu kupewa tenda bila kufuata mchakato hakuna tatizo hapo.
Tatizo lipo kwako usiye na kumbukumbu.
CCM sio chama cha wakulima na wafanyakazi, ni chama cha mafisadi, wezi na majambazi wa Uchumi wetuKwanini watanzania wengi wameshtuka kuhusu ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni cha kwa gharama za Bilioni 7.5 kwenda kukarabatiwa nchini Kenya.
Lakini ukipitia Tovuti ya TEMESA kwenye eneo la Zabuni hakuna mahali ilipotangazwa zabuni ya kukarabati wa Kivuko cha MV Magogoni.
Lakini nimepitia pia kwenye Account ya Instagram ya Mbunge wa Kigamboni, Dk Ndugulile naye hakuna post aliyoweka kuhusiana na ukarabati wa kivuko hicho.
Yote haya yanakuza mjadala kwanini asipewe Songoro Marine kukarabati kivuko hicho hapo nchini hadi kipelekwe Kenya?
Wajuzi tuendelee kujifunza