Kwanini tukarabati kivuko kwa Tsh. bil 7.5 wakati kipya ni bil 8.5?

Kwanini tukarabati kivuko kwa Tsh. bil 7.5 wakati kipya ni bil 8.5?

Nikumbushe tu kwamba 2020 tulipokwa haki yetu ya kuchagua viongozi tunaowapenda. Sio upinzani tu hata ndani ya CCM majina ya watu wenye akili yalikatwa. Mfano mzuri Ni Korogwe vijijini. Mahindi wa kwanza na wa pili walikatwa majini. Kachukuliwa mbumbumbu hata huko bungeni haendi.
Na,wizi ule ni mfano tu
 
Kuna kiongozi mmoja mwasisi wa taifa hili aliwahi nukuliwa akisema kama hamtaki kujihusisha kwenye siasa za nchi hii, kama hamtaki kujihusisha na maendeleo ya nchi hii basi huko mbele mambo yakiharibika msijekulaumu kwa sababu hakuna mtu atakayewafanyia hayo bali ni nyie wenyewe. Sasa mwenzako ameleta masikitiko yake kwa jambo la msingi kabisa wewe kwa ujinga au kutofahamu unaona jambo hilo halina maana, ila cha ajabu ikitokea kukawa hakuna kivuko hapo Kigamboni ndiyo utakuwa wa kwanza kulialia.
Sahihi
 
Achana na mambo hayo fanya yako,hakuna jipya TZ
Either Two;
1. Hujui wajibu wako kama mlipa kodi or
2. Ni mmoja wa mchwa wa kodi za wananchi
The guy was right, anauliza si kwa sababu hana mambo yake ya kufanya, ila kwa kuna kila dalili ya sehemu ya kodi kuliwa na mwacha nyie!
 
Na mimi niliposikia 7.5B nikajua tumepigwa tena. Sitaki wazo la viongozi wakuu katika sakata hili kuwa hawana uchungu na mali za Wabara liingie kichwani mwangu. Hivi Songoro Marine hana uwezo ku kukarabati hiyo feri kweli. Kama kweli ilijengwa kwa 8 B leo tena unatoa kiasi kama hicho kukarabati TEMESA na wote mliotia sahihi mna la kujibu kwa Mungu. Upinzani msikae kimya na kwa hili, maana ni kama hampo hapa Tanzania. Zito, Lisu, nk mko wapi?
Hao wote wana matonge mdomoni sio wa kuwategemea.

Hii nchi inatafunwa mpaka tutaanza kwenda makanisani na misikitini kumuomba Mungu atunusuru.
 
😂😂😂😂😂shukrani mkuu
Pamoja!
Nilianza kufurahishwa na wewe kwenye bandiko flan nazan lilikuwa ni lako mwenyewe.
Vituko toka Facebook.
Waliokaribu na wewe naamin hawana stress🙏
 
Mawazo ya wajinga tu, mbona simu za Sumsung ukiua tachi au kioo kuweka kipya ni zaidi ya nusu ya bei ya manunuzi
Sasa nani mjinga anayetengeneza kitu kilichochoka kwa 75% ya bei ya kununulia kipya? Ila sisi rangi ya tako tuna safari ndefu sana kufika hata robo ya wale weupe...
 
Hiki hapa ni kivuko kipya kilijengwa na Songoro Marine kikapelekwa Mafia- Nyamisati!, Kilijengwa kwa Billion 5.8 kipya sio ukarabati! Sasa sijui wanapeleka tender Kenya kufanya nini wakati miaka mingi Songoro Mirine amekuwa mjenzi na mkarabati wa hivi vivuko vyetu kwakushirikia lna na TEMESAView attachment 2519632
Hiki si kinabeba abiria 200 tu na tani 10 wakati MV Magogoni inabeba abiria 2000 na tani 500, ni zaidi ya mara 10 ya hiki.
 
Either Two;
1. Hujui wajibu wako kama mlipa kodi or
2. Ni mmoja wa mchwa wa kodi za wananchi
The guy was right, anauliza si kwa sababu hana mambo yake ya kufanya, ila kwa kuna kila dalili ya sehemu ya kodi kuliwa na mwacha nyie!
Historia ya Watanzania inatuhukumu wote mimi na wewe,Kwa kifupi hii ni nchi ya mchongo mchongo,haki yako kama mlipa Kodi iko wapi,hiyo ni ishu moja je umejiuliza maeneo mengine kuanzia ubora wa
1.Barabara,2. Ubora wa Bidhaa 3.Makato ya malipo mbalimbali 4.Mikopo ya nje na Matumizi yake.
So,hivyo ndo ilivyo.
Mimi nimesema.yangu,soo,jitahidi kufuatilia
Kuna kiongozi mmoja mwasisi wa taifa hili aliwahi nukuliwa akisema kama hamtaki kujihusisha kwenye siasa za nchi hii, kama hamtaki kujihusisha na maendeleo ya nchi hii basi huko mbele mambo yakiharibika msijekulaumu kwa sababu hakuna mtu atakayewafanyia hayo bali ni nyie wenyewe. Sasa mwenzako ameleta masikitiko yake kwa jambo la msingi kabisa wewe kwa ujinga au kutofahamu unaona jambo hilo halina maana, ila cha ajabu ikitokea kukawa hakuna kivuko hapo Kigamboni ndiyo utakuwa wa kwanza kulialia.
Umesahau kuwa Bunge Lina genge lisilo na haki ya kuwa hapo mjengoni sababu ya ugaidu katika kura.
 
Hiki si kinabeba abiria 200 tu na tani 10 wakati MV Magogoni inabeba abiria 2000 na tani 500, ni zaidi ya mara 10 ya hiki.
Wakati mwingine tutumie akili zetu sawasawa! hivi kivuko chakubeba watu 2000 kwa pamoja kiko wapi pale? watu 2000 unawajua au unasikia? wao walkadilia kwa siku sio kwa trip moja ibebe watu elfu 2 bwashekhe
 
Kwanini watanzania wengi wameshtuka kuhusu ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni cha kwa gharama za Bilioni 7.5 kwenda kukarabatiwa nchini Kenya.

Lakini ukipitia Tovuti ya TEMESA kwenye eneo la Zabuni hakuna mahali ilipotangazwa zabuni ya kukarabati wa Kivuko cha MV Magogoni.

Lakini nimepitia pia kwenye Account ya Instagram ya Mbunge wa Kigamboni, Dk Ndugulile naye hakuna post aliyoweka kuhusiana na ukarabati wa kivuko hicho.

Yote haya yanakuza mjadala kwanini asipewe Songoro Marine kukarabati kivuko hicho hapo nchini hadi kipelekwe Kenya?

Wajuzi tuendelee kujifunza
 
Wakati mwingine tutumie akili zetu sawasawa! hivi kivuko chakubeba watu 2000 kwa pamoja kiko wapi pale? watu 2000 unawajua au unasikia? wao walkadilia kwa siku sio kwa trip moja ibebe watu elfu 2 bwashekhe
We jamaa uko timamu kweli? Kivuko kile hakiwezi kuchukua watu 2000 at per??
We weka hapa thamani ya kivuko kipya chenye capacity kama ya Magogoni.

Watanzania mnapenda kulaumu na kuonekana nyie ndio wenye uelewa kuliko wataalam wenyewe.
 

BILIONI 7.5 KUKARABATI KIVUKO MV. MAGOGONI​

News Image

Posted On: February 16, 2023

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) leo imesaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV. MAGOGONI wenye thamani ya shilingi Bilioni 7.5. Mkataba huo umesainiwa leo katika eneo la kivuko cha Magogoni Kigamboni jijini Dar es Salaam kati ya Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Lazaro N. Kilahala na mkandarasi African Marine and General Engineering Company Ltd.inayotoka Mombasa nchini Kenya na kushuhudiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo, Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb), Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge, Wakuu wa Wilaya pamoja na viongozi mbalimbali wa Taasisi nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa amesema ukarabati wa Kivuko cha MV. MAGOGONI ni juhudi na mikakati ya Serikali katika kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafirishaji nchini na kuongeza kuwa ukarabati huo utakapokamilika utaharakisha na kurahisisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa wananchi waishio katika Wilaya ya Kigamboni, Ilala na maeneo mengine

’’Madhumuni ya ukarabati wa kivuko hiki ni kuhakikisha huduma inayotolewa na kivuko hiki ni salama kwa watumiaji na hivyo kuwaondolea wananchi kero ya usafiri inayotokana na kuchakaa kwa kivuko hiki.Kivuko hiki kilijengwa mwaka 2008 na kina uwezo wa kubeba Tani 500 yaani abiria 2000 na magari madogo 60 na ni kiunganishi muhimu kati ya maeneo ya Wilaya ya Kigamboni na Wilaya ya Ilala.’’ Amesema Profesa Mbarawa na kuongeza kuwa wakati umefika sasa wa kivuko hicho kufanyiwa ukarabati mkubwa.

’’Wakati kivuko hiki kinafanyiwa ukarabati kutakuwa na changamoto ya usafiri, kwahiyo niwaombe sana wakazi wa Dar es Dalaam hasa maeneo haya watumie kwa wingi Daraja la Nyerere ili kupunguza msongamano katika kivuko hiki, amesema Profesa Mbarawa na kuongeza kuwa wakati wa kutoa tenda Serikali inaangalia mambo mawili makubwa, ’’Jambo la kwanza tunaangalia bei, nani ni mwenye gharama za chini, kama alivosema Mtendaji Mkuu TEMESA, mkandarasi ambaye alikuwa na bei ya chini ilikuwa ni bilioni 7.5, aliyemfuatia wa pili alikuwa na bilioni 10, tofauti ya bilioni 2.5, kama hii ni pesa yako wewe utampatia nani mkataba wa kazi hiyo? Nawaachieni mjibu,’’ alimaliza Profesa Mbarawa.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu akizungumza katika hafla hiyo amewaomba wananchi wa maeneo hayo kuvumilia changamoto ya kukosekana kwa kivuko hicho wakati kitakapokuwa kwenye matengenezo kwa kuwa matengenezo hayo yanalenga kuleta huduma bora na kivuko hicho kuwa salama kwa ajili ya kutumiwa na wananchi hao.

Naye Mbunge wa Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza katika hafla hiyo ametoa rai kwa Serikali kutoa fursa kwa sekta binafsi kuruhusiwa kuanza kutoa huduma ya kivuko katika eneo hilo.

Aidha, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Lazaro N. Kilahala akisoma taarifa fupi ya mradi huo amesema mkandarasi African Marine and General Engineering Company Ltd. Ataanza rasmi ukarabati wa kivuko hicho mara baadaa ya kulipwa malipo ya awali na anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo ndani ya miezi sita.

’’Kivuko cha MV. MAGOGONI ni Tegemeo kubwa kwa wananchi wa Kigamboni kutokana na uwezo wake wa kubebea abiria na magari mengi kwa wakati mmoja hivyo ukarabati huu utawezesha kivuko hiki kutoa huduma ya uhakika na tija kwa wana Kigamboni.’’ Amesema Mtendaji Mkuu na kuongeza kuwa kazi ya ukarabati wa kivuko hicho itahusisha kazi za chuma, kuondoa mabati yaliyochakaa ya muundo wa chini na wa juu, ujenzi wa milango mipya ya kushushia na kupakia abiria, ukarabati wa chumba cha kuongozea kivuko, ufungaji wa injini mpya nne aina ya Caterpillar pamoja na gia boksi zake, matengenezo makubwa ya pampu jeti, marekebisho makubwa ya mfumo mzima wa umeme na elektroniki wa kivuko, kufungwa kangavuke (majenereta) mapya mawili, matengenezo ya mfumo wa tahadhari ya moto, kufunga kamera za CCTV, kuweka vifaa vya kisasa vya kuongozea kivuko, vifaa vya tahadhari na vya uokozi, pamoja na kupaka rangi kivuko chote.

Mtendaji Mkuu alimaliza kwa kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa kukubali kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo na miradi mingine na kuahidi kufanya kazi kwa weledi na jitihada kubwa ili kufikia malengo na matarajio ya Serikali na wananchi kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom