Wadau nawasabahi.
Nikiwa mlipa kodi pamoja na tozo mbalimbali najisikia uchungu sana kusikia kuwa Serikali inataka kukarabati kivuko cha Mv Magogoni kwa bil.7. wakati bei ya kuunda kivuko kipya ni kati ya bil.8.5 -9
Najiuliza kwanini ufanyike ukarabati?
Kwanini kisinunuliwe kivuko kipya?
Hata kama kununua ni gharama lakini tofauti yake ni ndogo sana. Hebu watendaji wa serikali tuwe na uchungu na kodi za masikini wananchi wananchi wana maisha magumu sana hata kama mnatuamulia mtakavyo lakini tunaumia tunapohisi mnatuibia.
Juzi juzi mmetoka kutuibia kwenye ukarabati wa mv hapa kazi mlikikarabati kwa bil.4.5 wakati kivuko kipya ni bil 7.5 kumbukeni watanzania sio wajinga kihivyo