Kwanini usijengwe ukuta katikati ya barabara za mikoani kupunguza ajali?

Kwanini usijengwe ukuta katikati ya barabara za mikoani kupunguza ajali?

mchawi barabara ni ndogo gari zipo nyingi,watanue barabara njia hata 4 kwa 4 uone kama kutakuwa na mambo ya overtaking
 
Safi sana kwa kufikiri vyema mtoa mada. Usifadhaishwe na wapumbavu wanaoamini wanatunza familia kwa mawazo yao bora ilhali hawana uwezo wa kufikiri.

Naamini ulilenga kuwasilisha kitu kama Concrete Barriers, yes inawezakana concrete ni urefu 2 to 4 feat na inaweza kuzuiza magari kuintervene. Mamlaka zifanyie kazi wazo lako.

View attachment 2196430

Kama picha inavyoenesha ukianza kwenda hadi tamati au eneo rasmi la kuingia njia nyingine hii imesaidia sana mataifa mbalimbali kupunguza ajali.
Wazo zuri, nashangaa wapuuzi wanamnanga. Ila barrier ya namna hii inataka four lane sio two lane.
 
Vizuri sana mkuu

Nashangaa kwa nini? Hawa jamaa wa jamii forum huu uzi hawajauweka kwenye kielelezo cha watu wanaofikilia zaidi au kile kipengele cha intelligent nashindwa kuamini mpaka sasa.

Ajali zimekuwa nyingi na sababu kubwa ni miundo mbinu ya barabara zetu “ watu umewafikirisha uliposema ujengwe ukuta lakini ukiusoma uzi wako ki-mafikirio utaelewa tu kuwa umejaribu kuwafikirisha,

Kikubwa nilichokiona ni warekebishe barabara zetu japo ziwe na unafuu wa kupunguza ajali nyingi zembe, barabara zetu ni changamoto na ukifikiria uwezo wa kujenga barabara zenye viwango lipo ndani ya uwezo wetu” ni tunaweza kabsa kutengeneza barabara za nchi nzima na tunapunguza ajali.. hili lifike kwa serikali yetu pendwa tunafahamu hilo jambo linawezekana kabsa.
 
Wazo zuri, nashangaa wapuuzi wanamnanga. Ila barrier ya namna hii inataka four lane sio two lane.
kabisa mkuu Jamaa kaleta wazo badala ya kumchallenge kwa hoja wanasema tu haiwezekani ndiyo nin sas
Jamaa ana wazo zuri lakin haitawezekana kwasababu ukuta utazuia kuovertake vinginevyo labda atayewahi kuingia kwenye njia ndy huyo anatangulia vinginevyo hapo ni ngum kuweka ukuta barabaran
 
Nadhani huna idea hizo njia mbili zinavyojengwa. Kawaida hizi za highway huwa zinaacha nafasi kubwa katikati. Ukishajenga hivyo huhitaji tena kuweka hizo kuta kwani ni upotevu wa fedha. Kuta zinawekwa sehemu zenye ulazima tu.
Nimeona njia 9 left na njia 9 right na njia 4 na 2 nyingi sana. Soma reply yako hii vizuri uelewe andiko lako. “Sehemu zenye ulazima”

Hamna mtu kasema barabara itoke Kagera hadi Mtwara na concrete barriers.
 
Wazo zuri, nashangaa wapuuzi wanamnanga. Ila barrier ya namna hii inataka four lane sio two lane.
Inasikitisha hawa wanatoa maneno ya ajabu ni watu wanaohusika kulijenga taifa. Watu hawajiulizi ni mada zipi za utani na zipi zinahitaji umakini na mawazo halisi.

Yes barriers hizi 4 lines na juu, lakini maeneo machache zinaweza kuwekwa hata kweye kulazimisha watumiaji kukwepa maeneo hatarishi.
 
Watu wengi wanamdhihaki jamaa harafu hawajui kitu na hawana exposure yeyote zipo Nchi nyingi zilizoendelea ukuta mdogo wa Zege iliyoshiba inapangwa katika kati ya bara ili ajali za upande mwingine zisihusishe upande huu mbona kawaida sana hiyo tena unakuta concrete linewekwa kilomita za kutosha tuu ni vile ameongea kitu ambacho watu hawajui kama kipo Duniani...
 
Please ...siyo kwa sababu katoa wazo la kipumbavu mumwite mpumbavu. Ni haki yake kikatiba. Mumweleweshe tu taratibu atajifunza ataelewa. Sawa mtasema ni sababu ni darasa la saba lakini lia hata hao darasa la saba wanapaswa kueleweshwa. Mimi nimemuelezea tu kistaarabu sijataka kumuonesha kuwa ni mpumbavu. Atajisikia vibaya naye ni binadamu jamani
 
Mtoa mada yupo sahihi,Haya mambo yapo wala sio mageni pesa umaskini ndio unafanya tumshangae....

download (1).jpg

images.jpg

images (1).jpg
 
Nimeona njia 9 left na njia 9 right na njia 4 na 2 nyingi sana. Soma reply yako hii vizuri uelewe andiko lako. “Sehemu zenye ulazima”

Hamna mtu kasema barabara itoke Kagera hadi Mtwara na concrete barriers.
Naona unaanza kuomba ''po'' kiaina. Rudi post yako no 20 uone fyongo uliyoandika. Utaungaje mkono wazo wa kijinga eti barabara zetu tatizo la ajali litatatuliwa kwa kujenga ukuta katikati? Mkibanwa mna-google na kuja na picha za barabara zenye barrier ambazo zimewekwa sehemu muhimu kwa sababu maalaum.
 
Watu wengi wanamdhihaki jamaa harafu hawajui kitu na hawana exposure yeyote zipo Nchi nyingi zilizoendelea ukuta mdogo wa Zege iliyoshiba inapangwa katika kati ya bara ili ajali za upande mwingine zisihusishe upande huu mbona kawaida sana hiyo tena unakuta concrete linewekwa kilomita za kutosha tuu ni vile ameongea kitu ambacho watu hawajui kama kipo Duniani...
Wanaobisha hawasemi kuwa kuna sehemu ambazo hazistahili kuwekwa ukuta. Umesoma mtoa mada? Yeye anataka kwa mfano barabara ya Arusha mpaka Dar ibaki hivyo hivyo, na wembamba wake halafu uwekwe ukuta katikati.
 
Inawezekana mkuu sema jamaa ameshindwa kuelezea ni ukuta wa aina gani huo!.

Huyu jamaa alitaka kusema kingo ngumu za zege ambazo kuna nchi kadhaa hata hapo Kenya zimejengwa kwenye ile High Way ya kuelekea kasikazini, hata mtu wa kutembea kwa miguu huwezi kuruka kwa haraka.

Hii kitu ni nzuri sana tatizo ni mfumo na serikali kuamua kuwekeza kwenye eneo hilo.

View attachment 2196546View attachment 2196547
Google bila akili inafanya wengine waonekane vituko. Ona wewe hujajua mwanzisha mada kasema nini na watu wanambshia nini, umeingia google na kuja na kituko chako.
 
Watu wengi wanamdhihaki jamaa harafu hawajui kitu na hawana exposure yeyote zipo Nchi nyingi zilizoendelea ukuta mdogo wa Zege iliyoshiba inapangwa katika kati ya bara ili ajali za upande mwingine zisihusishe upande huu mbona kawaida sana hiyo tena unakuta concrete linewekwa kilomita za kutosha tuu ni vile ameongea kitu ambacho watu hawajui kama kipo Duniani...
Jamaa kaongea kitu ambacho wengi wamekitafsiri kwa namna ya Low IQ watu wanadhani jamaa alimaanisha ukuta mrefu lakini sio... pia back to the point barabara zetu hasa za mkoani ni nyembamba sana magari yanapopishana yanaacha nafasi ndogo mnoo kiasi kwamba ile nafasi haitoshi hata kuweka separation blocks anachosema muandishi kinawezekana barabara zikiwa pana
 
Back
Top Bottom