Kwanini vyama vya upinzani havishindi, na hata vikishinda havishindi?

Huu ndio unaita uchaguzi wewe zezeta , huyu mtu akiwa msimamizi wa uchaguzi 2020 halafu 2025 akaenda kugombea kwa maccm unafikiri hiyo 2020 alikua anakipigania chama gani?

2020 Mahera alikua msimamizi wa kiitwacho uchaguzi huku ana kadi yake ya kijani kibindoni na anakipigania chama chake cha kijani 2025 wakamzawadia ubunge feki.

Wajinga waliisha hamuwezi kutudanganya tena hatupo 1960 &1970.


View: https://x.com/JamiiForums/status/1310446371623895041
 
Wewe zezeta hapa huyu Nepi anasema kabisa matokeo ya kura na mshindi anayetangazwa hayahusiani na watu waliopiga kura na kuziweka kwenye sanduku kama machaguo yao.

Ulitegemea hapo mpinzani atashindaje wakati kuanzia nafasi ya juu hadi chini wanaosimamia kiitwacho uchaguzi ni maccm?

Una maoni gani hapa wewe chawa wa bei rahisi?


View: https://x.com/JamiiForums/status/1813259138639798332
 
Katiba ya Tanzania ni ya mfumo wa chama kimoja
1992
80% ya watanzania walikataa ku adopt mfumo wa vyama vingi.
Zilikuwa shobo za viongozi kuruhusu vyama vingi ndio maana karibia vyama vyote vilianzishwa na mapandikzi ya serikali
 

Porojo hizo. Lissu, Mnyika, Sugu, Msigwa, Lema, nk wote walikuwa wabunge kwa tume hiihii. Hata Kenya na Marekani walizilalamikia tune zao kughushi matokeo. Uchaguzi siku zote duniani kote ni jambo la survival of the fittest. Fanya kampeni za nguvu, pata wafusi, washawishi wakapige kura wengi utatangazwa tu.

Hata chadema ikiwa madarakani haiwezi kukubali ishindwe kiboya kama uwezo wa kushinda upo.
 


Porojo gani wewe zezeta?

Nimekuwekea video hapo ya Nape akisema watu wakipiga kura hawaamui mshindi bali anayetangaza sasa unabisha nini?

Ulivyo mpumbavu unajiandikia tu eti "survival for the fittest " nenda kajielimishe kwanza hiyo statement ina maana gani , uchaguzi unawezaje kuwa survival for the fittest wakati uchaguzi haufanyiki katika mizania sawa

Survival for the fittest inahusu mazingira yenye mizania sawa ndio hapo sasa chenye nguvu kitabaki na kisichoweza kitatoweka , nenda darasani upya ujielimishe hujachelewa.

Huu upumbavu wa kuingiza mabunda ya kura ndio mnaita uchaguzi?

Hebu nieleze hapa mtu anayeingiza mabunda ya kura waliyotiki usiku wake upande wa Samuya utaanzaje kumshinda mtu kwa mtindo huu?

Nakubaliana na Warioba kwamba uchafuzi ule tume ya CCM ndio ilimchagua Samuya sio wananchi.

Ukizungumzia CHADEMA kuwa madarakani na kusema hawatakubali watoke unataka nikuamini vipi kwa kitu ambacho hakijatokea, inatakiwa waingie wakigoma kutoka ndio tuone wamegoma sio hizo propaganda uchwara .

Mbona husemi Moi alikua na kila kitu cha kuweza kuinusuru KANU ila alikubali kushindwa uchaguzi na NARC , 2002 hata kabla ya matokeo ya mwisho ya majumuisho kutolewa mgombea wa KANU , Uhuru Kenyatta aliambiwa akatangaze kukubali kushindwa na kukubaliana na chaguo la wananchi?

Your browser is not able to display this video.
 
Kwa sababu ya watu wenye mtazamo kama kavulata
 
Cc kavulata
 
1992
80% ya watanzania walikataa ku adopt mfumo wa vyama vingi.
Zilikuwa shobo za viongozi kuruhusu vyama vingi ndio maana karibia vyama vyote vilianzishwa na mapandikzi ya serikali
Tutahakikisha chadema inarudishwa kwa wenyewe.
 
Cc kavulata
Kwahiyo akina Lissu walikuwa wakishinda viti vya ubunge? Usiwe na akili za kushikiwa katika umri wako. Chadema ni dhaifu sana kuweza kushinda uchaguzi. Ni wanaCCM tu akina Lowasa, Kingunge. SUMAYE na wengine wakihamia chadema ndio wanapata wabunge na kura nyingi. Wale unaowaona kwenye mikutano ya chadema wengi wao ni wavuta bhangi ambao hawapigi kura, na ni haohao wanaokwenda kwenye mikutano ya vyama vingine.
 
Kila nchi Ina miiko ya kiroho na tambiko lake!

Hapa kwetu tambiko letu ni mwenge wa uhuru na Champa chake CCM,ili upinzani upewe lazima kufanyike tambiko jingine la kusimika upinzani wenyewe ili usilete dosari kwenye amani ya nchi na upngozi!

Mambo haya ni kama hekaya lakini ukiongea na wazee wa chama hasa wale dar es salaam japo sio wa dar bali huitwa TU kidesturi kama tafsida Yao !!

Ccm lazima ilindwe Hadi pale tambiko jingine lifanyike ndipo upinzani upewe!!
Tambiko linahusisha damu sasa hatujui ni damu kiasi Gani zapaswa kumwagika ili kutakasa upinzani kupewa!!

Labda zile za October 29 na zijazo ambazo labda zitatokea zitatakasa upinzani kupewa!!

Nawaza TU,

Mambo ya utawala na uongozi si rahisi sana ndio maana alpnaeshika huamriwa ashike Dunia nyingine tofauti na hii!!mkumbuke shehe yahaya husein!!
 
Chadema ishinde uchaguzi kwasababu zipi?
 
Kafara kubwa zilifanywa na akina sheikh Ramia wa Bagamoyo na Sheikh Tambaza. Huyu Heche anadhani kuleta Uhuru ni kama kuvuta bhangi tu. TANU/ASP/CCM wanaona ni kitu cha hovyohovyo tu hivi, na rahisi kukatiza kwenda Ikulu kwa kukinukisha. Wakaishia kuchambia mgomba.
 
Chadema ishinde uchaguzi kwasababu zipi?


Kwani KANU walishindwaje uchaguzi 2002,?

KANU ndio ilikua kama CCM imeshika dola kila mkenya alilazimishwa kusema baba na mama yake ni KANU na kuimbishwa KANU JUU NYAYO JUU JUU KABISA.

Moi hakuwa anaitwa rais Moi au mheshimiwa Moi bali aliitwa Mtukufu Rais Moi.

Moi alikua na machawa hata sidhani kama Samuya amemkaribia, ndio maana wakenya wanatuona tunaishi 2026 maisha waliyoishi miaka ya 1980 hadi 1990.


KANU licha ya kuwa na dola , polisi, usalama wa taifa na jeshi chini ya miliki yao chaguo na mrithi wa Moi , Uhuru Kenyatta alishindwa uchaguzi mapema tu na Kibaki ambaye hata wakati huo alikua uhamishoni kwa matibabu baada ya ajali , kwa ufupi wakenya walichagua mtu ambaye hawakujali atarudi akiwa hai au mlemavu ndio maana Kibaki aliapishwa kwenye kiti maalum cha walemavu wa viungo.

Muda wa mabadiliko ukifika mazezeta kama wewe hamna tofauti na yule mama aliyekua akifanya kazi ikulu anaitwa Saly Koagei alilia sana siku Moi anaondoka ikulu maana hakuamini amekabidhi madaraka kwa chaguo la wananchi alitegemea angetumia jeshi na polisi kimabavu kuendelea kutawala.

Hii hapa ni video ya mgombea wa KANU , Uhuru Kenyatta akikubali kushindwa uchaguzi hata kabla tume haijatoa matokeo ya mwisho kumtangaza Kibaki kuwa mshindi na chaguo la wakenya na kuhitimisha miaka 39 ya utawala wa KANU.


View: https://youtube.com/shorts/yc6xgq92hjY?si=44CvMZB1aHgtZ6CM
Wajinga kama nyie ni jukumu langu kuwakumbusha kwamba kuna siku CCM itatoka madarakani msijisahau na kujiona mnayo hatimiliki kuongoza nchi.
 
Unaongelea kushinda au kupora uchaguzi, ama unadhani watu wanagoma kushiriki huo upuuzi bila sababu za msingi? Machafuko pekee ndio yatawafanya mpate akili.

Kama issue ni kushinda tu, VAR ililetwa kwenye soccer kwa ajili gani? Ama washindi walikuwa hawapatikani hapo kabla?
 
Kweli kabisa kwa mfano Lissu amejikita sana kwenye ishu za katiba, huwezi ukamsikia anaongelea ishu za maendeleo au uchumi au kwasababu siyo taaluma yake.
 
Tutahakikisha chadema inarudishwa kwa wenyewe.

Utahakikisha wewe na nani zezeta?

Inachekesha sana eti mazezeta ya Lumumba mnataka kuwapangia CHADEMA uongozi na viongozi wao uwe vipi.

Mlisema mwanzo ni chama cha wachagga na walutheri , wajumbe wameleta mabadiliko mmeanza kelele sababu ya mtu mliyekua mkipiga nae dili kawekwa kando.

Wajumbe waliamua na uchaguzi ulifanyika wazi na video zipo kila hatua hadi kuhesabu kura ilikua wazi na Mbowe alishindwa.

Mambo ya wenyewe yako huko CCM ndio maana Kikwete alisema CCM ina wenyewe ila kwa CHADEMA mtu awaye yoyote akikubalika na wajumbe atapewa uongozi.
 
Hata hujui kitu aloo. Sera za KANU na waliokiangusha zilikuwa zinafanana kabisa, infact siasa zao zilikuwa zinafanana kabisa.

Sera za KATU zilikuwa ubepari, ardhi kunyakuliwa na wachache, ukabila na kuacha kutaifisha mali za wakoloni. Hata vyama vilivyoiangusha KANu hakuna kitu wamebadili kuhusu ardhi, ukabila na ubepari.
Hapa kwetu wapinzani wanadunda kwakuwa wanatangaza kutaka kubadilisha kila kitu wakifika Ikulu.

Wewe huna unachokijua kwenye siasa za ndani na regional politics, unafuata mkumbo tu.

Unadhani ni kwanini Raila hata akiungana na nani alikuwa haendi Ikulu?
 
Simama hapohapo usitikisike. Mtei na Makani walikuwa ni watu wa system kindakindaki, chama chao kugeuzwa chama cha kigaidi na wahuni ni kashfa isiyovumilika. HECHE amekigeuza ng'ombe wake wa maziwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…