Kwanini vyama vya upinzani havishindi, na hata vikishinda havishindi?

Tafadhali ndugu naomba tupe somo hapo kwenye Nyerere kupinduliwa sisi wapenzi watazamaji

Nyerere baada ya nchi kuwa rais 1962 alishiriki chaguzi mbili tu za kidemokrasia 1962 na 1965.

Baada ya hapo alifuta vyama vya siasa na kuibakiza TANU kama chama pekee halali na chenye kuruhusiwa kufanya siasa.

Miaka ya 1960 & 1970 baada ya safari zake kwenda nchi za kijamaa kujifunza na kuomba misaada alijikuta anaingia kwenye sera za ujamaa hapo ndio aliaanza kutofautiana na viongozi wengine wa chama na hata raia.

Mfano wa sera ya kuanzishwa vijiji vya ujamaa ni watu kulazimishwa kutoka maeneo yao wanayoishi kwenda kukusanywa eneo moja kwa amri ya rais.

Nyerere alijitengenezea sheria ya preventive detention act kupitia sheria hii rais aliweza kuamuru mtu yoyote kuwekwa kizuizini mpaka pale atakapoamua aachiwe kupitia sheria hii tulipotezan watu wengi tu waliofichwa nyumba za siri kwa miaka mingi bila kujulikana wako wapi na hata kutofikishwa mahakamani kwa sababu hakukua na kosa wala sababu bali utashi wa Nyerere tu.

Jaribio la kwanza lilitokana na mambo wanajeshi wazawa kutopata maslahi sawa kijeshi , lilizimwa na jeshi la Uingereza na ndio ikaundwa JWTZ upya 1964.

Jaribio la pili kubwa ni wale wanajeshi na raia 1983 ambapo ilitokana na ukata na mdororo wa kiuchumi kwenye nchi baada ya vita ya Uganda 1979 , bidhaa ziliadimika na hata zikipatikana ilikua kwa mgao na kuporomoka kwa thamani ya shilingi na uchumi vilichangia huku Nyerere alipokua akishauriwa kuachana na sera za ujamaa zilizofeli yeye aliendelea kushikilia misimamo yake na aliyejaribu kumpinga aliwekwa kizuizini na hakukuwepo na uwanja wa mabadiliko maana hakukua na demokrasia wala uchaguzi ambao ungeleta mawazo mbadala maana chama kilichokuwepo na kuruhusiwa kufanya siasa ni CCM na yoyote ili upate nafasi hata chuo kikuu lazima upate kadi ya CCM.

Nimejaribu kueleza kwa ufupi athari na majaribio ya mapinduzi siku zote ni kutokana na kuminya demokrasia na uhuru wa mawazo mapya na kinzani hali ambayo hufanya watu kutaka kutumia njia nyingine kuingiza serikali mpya madarakani .
 
Hivi Nchimbi yuko wapi?
 

Kumbe hujui hata unachoandika, Maraga amestaafu ujaji mkuu 2021 na uchaguzi wa kushindana Ruto na Odinga umefanyika August 2022 akiwa na mwaka mzima tangu aondoke ofisi.

Halafu kwa katiba ya Kenya chombo pekee kinachosimamia uchaguzi ni IEBC, na uchaguzi ambao matokeo yake ya urais yalifutwa mahakamani ni wa Uhuru na Odinga 2017 na uchaguzi ulirudiwa siku 60 baadae japo Odinga aligomea kushiriki marudio.

Mahakama ya upeo ya Kenya haisimamii uchaguzi bali wagombea wasioridhika na matokeo ndio hupeleka malalamiko mahakamani kama alivyofanya Odinga.

Na kupitia petition ile Kenya ndio iliweka rekodi kuwa nchi ya kwanza Africa kufuta matokeo ambayo rais aliyepo madarakani alitangazwa kutetea kiti chake kwenye hili umevaa miwani ya mbao na kujivika uoga ukidai hakuna tume na mihimili huru duniani sishangai maana ndio akili za maccm.

Unaruka ruka tu kwamba sera ya Raila ni mjaama mara baba yake kwani unafahamu mzee Jaramogi alikufa kitambo tangu 1994 na inahusianaje na Raila kuwa rais kama baba yake alikua mjamaa kwani na yeye lazima we mjaa?

Usichokijua ni kwamba Raila alishinda uchaguzi wa 2007 ilitumika nguvu nyingi kupindisha ule ushindi kwa maslahi ya watu wachache wa kambi ya Kibaki waliofuatilia ule uchaguzi wanaujua ukweli hata majuzi mzee Macharya wa Royal Media Group alisema na ndio kupitia uchaguzi ule na vurugu zake walipata katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Huwezi kusema tume huru ya uchaguzi Kenya ni sawa na hii tume ya maccm iliyowekwa kwenye mkoba wa Samuya.

Tume ya uchaguzi ya Kenya nafasi zake zote hutokana na merit hauteuliwi , tangazo hutoka watu huomba nafasi, hufanyiwa usaili wa wqzi na huthibitishwa na bunge ndio jina linaenda kwa rais tu kukamilisha mchakato wa kuapishwa na viongozi wa tume hawatolewi na rais na sio waajiriwa wake.

Huu ni usaili wa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Kenya unaofanyika wazi kila mtu anajionea.


View: https://youtu.be/q8QNuA8l9e0?si=JhetSA7X6c1OtAm4
Sasa wewe weka hapa video mchakato kama huu kwa Tanzania tuone , maana kwa Tanzania ni kwamba Samuya akiamka na jina la kada yoyote wa CCM anampachika hapo na anapewa maelekezo na asipofanya anatimuliwa.
 
Tume ina kazi ya kuwasaidia wapiga kura kuwaepusha na mapandikizi ya kisaisa, vibaraka wa nchi za Magharibi, waganga njaa na waongo.

Ni mara ngapi wabunge wa upinzani walienda CCM kuunga juhudi na kuuacha ubunge wa upinzani? Ni mara ngapi viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani wamerudi kujiunga na CCM? Ni mara ngapi wagombea wa vyama vya upinzani wamepewa nafasi za uteuzi serikalini?. Ni mara ngapi mwanachama wa CCM anaefukuzwa CCM anapewa nafasi ya kugombea kwenye vyama vya upinzani?
Hii ni kuonyesha kuwa wananchi hawana elimu ya kuwachambua wapinzani, hawana elimu juu ya vyama vingi bado. Ni rahisi kumpeleka Kibaraka Ikulu kwa kutokujua.

Tume za kwenye mataifa machanga kama haya zinatakiwa kuwa water tight kuzuia vibaraka na wakora kupenya. Yaani tume za Afrika zisiwe too porous kwakuwa uelewa wa wapiga kura wetu bado mdogo sana; vibaraka wanatumia kero za wananchi kuombea kura bila kuwauliza watakwenda kuzitatua vipi wakifa Ikulu.
 
Hivi Nchimbi yuko wapi?
We subiri tu, Nchimbi ni ndoana nyingine CCM wamewategea wapinzani, lazima wataimeza tu 2030.

Nchimbi katulia nyumbani kwake anakula mafao yake akiyasubiria mazuzu wayakanyage. Mpina anarudi nyumbani baada ya kumaliza kazi yake.
 
Hapo nakukubalia 100% kuwa nilipuyanga. Mwenyekiti aliyepindisha ushindi wa raila alikuwa Wafula Wanyonyi Chebukati
 


Tume haina kazi ya kuwasaidia wapiga kura hiyo ni kazi ya tume ya maccm.

Hujui waunga mkoni juhudi walikua wanafuata mapesa waliyopelekewa na akina Polepole enzi zile ndio ulikua mradi wake.

Kibaraka ni nani , utamjuaje?

Taifa lina miaka 60+ liko huru linajiitaje changa, ujinga ulionao kwenye hicho kichwa chako ni mkubwa sana.

Kero za wananchi ni zipi hujui hata baada ya miaka 60 CCM inatembelea magari ya milioni 600 halafu vyoo wanajengewa na Canada na USA so CCM ni kibaraka ?

Akina Abdul wanapiga mabilioni halafu vyoo mnajengewa kwa kodi za mnaowaita mabeberu sio unafiki huo?

 
Umepuyanga.
 
Mpaka leo tuna watu bado wanachamba kwa kusota miambani hapa nchini, na wengine kujisaidia vichakani, na wengine wanakata viungo vya binadamu, na wengine wanashikwa bega na nyeti zao kupotea na wengine wanaogopa popobawa. Hiyo ni jamii iliyokomaa? Sisi bado sana aloo, hebu nenda kwa Mwamposa ukaone namna tulivyo bado kabisa kuachiwa tupige kura wenyewe na matokeo kutangazwa kama yalivyo. Bado inahitajika the survival of the fittest kuamua mambo mengi hadi hapo tutakapopiga kura kwa informed choice.

Tuko level ambayo hata Peter Msigwa anaweza kuhamia CCM kuisadia ishinde uchaguzi kisha kurudi tena kulekule upinzani akachote siri nyingine na kuzipeleka CCM wakati mwafaka ukikaribia. Bado kabisa upinzani baaadoo.
 


Rudia kusoma ujinga ulioandika halafu uone hata kama wewe mwenyewe utaulewa .
 
Wewe ndio umepuyanga kwenya hii mada yako mbovu na bado unazidi kupuyanga kwa kuandika ujinga .
Hata sijui unachopinga kwenye hii mada ili nifafanue zaidi kwaajili yako. Yaani unapinga kwamba mjini haviendi hata vikioga au nini?

Kumbuka hivi vyama vilishiriki uchaguzi 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, 2020, na 2025 kote huko havikwenda Ikulu ila wanaitwa tu kwenda kula, kunywa na kupiga picha. Hawajiulizi kwanini hata kama wana viongozi mabumunda?

Vyama hivi havina watu wa maana wanaoweza kujenga hoja, watu wa maana kama Prof. Mkumbo, Nasari, Kafulila,m hawawezi kukaa meza moja na watu aina ya Sugu, Lissu, Lema.
Bado vinasubiri watu wenye akili kutoka CCM waende wakaongezee nguvu japo ya kupata wabunge wengi na ruzuku kubwa.

Vina sera kinzani na historia yetu ya miaka 65 ya uhuru, haikubaliki hata kidogo. Hakuna anaeviamini

Njia pekee wameona ni kuasi ili kupata wanachokitaka, ni hiyo ndiyo hatari zaidi kwao, kwakuwa hata China, Urusi, NKOREA, Cuba, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini, Msumbiji, Afrika Kusini, Zimbabwe watu kama Lissu na Heche wapo lakini nchi zao zinakwenda nao tu polepole na haraka pia.

Yaani wako watu kama Malema, Chivangilai, Mangusutu, Kiza Besije, Bob Wine, Raila, nk lakini sera zao zinakinzana na misingi ya Taifa. Hakuna chama kinatakiwa kuitikisa misingi iliyowekwa na waasisi. Hata Museveni hakuitikisa misingi ya Obote kama alivyofanya Idd Amini



Hivi vyama
 

Huwezi kujua ninachopigania maana mimi nafikiri kwa kutumia ubongo wewe unatumia tumbo maana ndio order of the day huko CCM.

Mnatiki kura usiku halafu asubuhi mnazileta kwenye masanduku mnasema mtu kapigiwa kura milioni 31 kati ya 32 na kapata 98 % katikati ya mabomu, risasi na ukosefu wa internet eti ndani ya saa 72 mmepata majibu.

Sera ya CCM kwa sasa ni ufisadi , wizi, kuteka , kuua, kufira wakosoaji .

Hii mada tutaenda hata mwaka mzima huna evidence ya kunithibitishia Samuya alipata kura milioni 31 wala kuniaminisha ule ulikua uchaguzi.

Your browser is not able to display this video.
 
Ubongo umeoza huo, tangu 1995 hupati jibu la maana kufikiri kumefika mwisho kilichobaki mwachie Mungu.

Ukiona wapinzani wameshindwa kutofautisha kati ya mali ya wananchi na mali ya CCM na Rais ujue hali ni mbaya sana. Unajiuliza kwenda Ikulu kuna uhusiano gani na kuchoma mwendokasi tunaotumia sisi makabwela?
 
Akili kama hii huipati upinzani asilani. Anaongea bila kuwafokea anaowaambia. Hamna tusi hamna keli hamna kulowa jasho. Kwanini wananchi wasimuelewe?

View: https://youtu.be/yOE41fjGLsM?si=xiVJdLAou88WEmL_
 

Sheria inasema matokeo ya uchaguzi yanatakiwa kukaa kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi kwa miezi 6 baada ya kutanganzqa je hayo matokeo feki ya 98 % za Samuya yaliwekwa lini wewe zezeta chunguza utajua kuwa hayakuwahi kuwekwa sababu hakukua na uchaguzi.

Nguruwe hata umvike suti na tai umpulizie na marashi haibadili uhalisia ni nguruwe na atafanya tabia za nguruwe .

Uchaguzi ambao mabomu , risasi, mauaji yalishamiri kwa kiasi kikubwa unaanzaje kuwa na wapiga kura wengi kuliko chaguzi zote zilizowahi kupita na hazikupata janga kubwa kama la October 29?

Hii inawezekana vipi ambapo mtandao umezimwa , na video zipo nyingi tu tangu saa 2 asubuhi watu wanavuruga na kuvunja vituo vya kupigia kura visivyo na watu maana walipuuza zoezi hilo uchwara eti siku tatu mbele mje mtudanganye ule ndio ulikua uachaguzi ambao watu wengi walipiga kura?

 
97.6% ya waliopiga kura, hata akili hamna. Hata kama waliopiga kura walikuwa 100,000 tu, lakini 97.6% (97,000) yao walichagua CCM. Chadema mliweka mpira kwapani kaeni kimya.
 
Sababu chama tawala hakiwezi ruhusu, vyama vya upinzani vishinde...


Cc: Mahondaw
Vyama vya upinzani ni dhaifu, havina agenda. Pale Zanzibar sera kuu ya wapinzani ni Zanzibar kuwa na mamlaka kamili, hawana agenda nyingine. Huku bara pia hawana sera, wanaorodhesha kero za watu kama mtajj waoʻ

Vyama vinavyopishana Ikulu ni vyama vinavyofanana sana kwenye misingi ya taifa, la sivyo votaenda parallel hadi hapo itakapotangazwa tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…