Kwanini waajiriwa wengi hawana utamaduni wa kufanya savings nchini?

Yani umeongea point kubwa sana....save at your own risk...yanii hata kama unapata 1M save hata 70k ambayo haitaguswa kamwe...haya mambo ya savings yaendane na uhalisia wa kipato, mahitaji na majukumu..na usisahau kuishi.
 
Sababu kubwa ni ya kitabia na mazoea. Ili ufanikiwe saving anza tabia hiyo tangu ukiwa na umri wa miaka 20.

Sababu nyingine ni vipato duni ambavyo haviendani na uhalisia wa maisha. Wengi ujikuta wanaishi with deficity budget . Solution wafanyakazi wajifunze kutanua vyanzo vya kipato. Tabia hii ianze punde tu unapoanza kujitambua kua pesa inahitajika.

Sababu nyingine ni unyonyaji wa kimfumo. Watumishi Kila mwenzi wanahitajika kisheria kusave 10% ya mishahara Yao. Pia serikali inawachangia another 10% that mount to 20%. Hizi pesa zinachukuliwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kama NSSF and PSSSF. Lakini mifumo ya operation and return kwa wafanyakazi sio rafiki coz pesa hizo watumishi hawana access nazo hadi watakapostaafu. Ni vyema mapitio ya kisera yafanyike ili pesa hizi wafanyakazi wazitumie kufanya shughuri za maendeleo kama kuwa bond ya mikopo ya nyumba n.k
 
Umeongea point kubwa sana, kusave ni tabia na utamaduni unaojengwa angali mdogo, pia pesa za mifuko ni Kama serikali imezifanya zakwao hata hivyo wamezitumia karibia zote
 
M naona kwanza lazima ujue unasave kwa ajili ya lengo gani mfano kama kwa ajili ya emergency, kwa ajili ya kununua kitu flani au kwa ajili ya vacation, baada ya hapo ndio utajua kiwango gani cha kusave kwa muda gani ili uweze kufanikisha hilo lengo,nimependa wazo la jamaa hapo Save kiwango ambacho unaweza kukimudu, maisha mengine lazima ya endelee.
 
Hakika mkuu, tukiambiana ukweli kama huu uliosema watu wengi watatoboa, mwaka 1 mpaka 5 ndani ya ajira hutoa tathimini ya maisha ya mtu ya miaka inayofuata. Unakuta huyu anaepokea 500,000 hana familia na ametoka katika familia ya kawaida sana hivyo kama akijiongeza anaweza akachukua room moja tu 50,000 to 70,000 ambayo ipo maeneo ambayo yanafikika kiurahisi kutoka kwenye mihangaiko yake. Inabaki 430,000 ambapo savings 200,000 kwa mwezi na 230,000 inabaki ya matumizi mengine. (baada ya mwaka si atakuwa amefika pazuri)

Kwa maisha ya sasa ukishindwa kujipanga mwanzoni kabisa yaani mwaka 1 mpaka 5 kabla hujawa na familia, usitegemee kufanya savings wakati una familia, na kama ni mwanaume utaishia kuwalaumu wanawake wanapenda ela.
 
Ni wazo zuri sana ili, shida utokea muda wowote ule
 
kaka wazo zuri lakini imagine mtu analipwa net pay laki mbili kwa mfano baada ya deductions hapoa natakiwa kula nauli alipie makazi sasa hapo ata save nini lets get real jamani
 
Wacheni kujitweza na uongo mwingi wa kuwa kila kitu munalipia nyinyi wababa.

Mfanyakazi huwa analipwa na mama kwa vile nyinyi munagoma kulipa mishahara yao. Mavazi ya watoto yanalipiwa na mama nyinyi munajifanya kama hamuna habari kwamba watoto huwa wana mahitaji ya kuvaa.

Na hao waarabu unaowatolea mfano ni kweli mwanamke huwa hafanyi kazi lakini pia huwekewa mfanyakazi na kuhudumiwa kikamilifu.

Kijana, hakuna mshahara unaotosheleza hata siku moja maana kila ukipata nyongeza basi unajipandisha cheo na wewe.

La muhimu ni kujiwekea discipline ya kusave, hakuna ujanja mwengine wowote.
 
mtu anayelipwa laki 9 ni sawa na elfu 30 kutwa

mama na baba 200000
pango 150000
chakula 300000
pretrol 100000
saluni, bar, michepuko, fegi, bangi n.k 100000
nguo, viatu, na mpesa kwa ndugu 100000

kila mwezi unabaki na deni la 50000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…