Kwanini waajiriwa wengi hawana utamaduni wa kufanya savings nchini?

NIMETEMBEA DSM KARIBU MAENEO YOTE NYUMBA NYINGI NA MAENEO MENGI WANAKOISHI MATAJIRI MAENEO YANAYOMILIKIWA NA WAAJIRIWA AU WALIWAHI KUAJIRIWA KUANZIA OYSTERBAY,MASAKI,MIKOCHENI,MBEZI BEACH,KUNDUCHI ,KIJICHI,MBWENI, SASA KAMA HAWAWEKI AKIBA WALIWEZAJE KUISHI HUKO?
 
mtu anayelipwa laki 9 ni sawa na elfu 30 kutwa

mama na baba 200000
pango 150000
chakula 300000
pretrol 100000
saluni, bar, michepuko, fegi, bangi n.k 100000
nguo, viatu, na mpesa kwa ndugu 100000

kila mwezi unabaki na deni la 50000
Hapo kwenye bangi umenichekesha sana, Mimi kwa Mwezi nafuta around bangi ya 15,000/= at maximum
 
Pole sana mtoto ukikua utayaona!!! Hata mm nikiwa mdogo nikimshangaa sana baba yangu kwann hakuwa na gari!!! Nilivyokua na Mimi sina gari naona ugumu baba alioupitia!!!hivyo Hata wewe ukikua utaona kufanya saving ilivyo ngumu
 
Pole sana mtoto ukikua utayaona!!! Hata mm nikiwa mdogo nikimshangaa sana baba yangu kwann hakuwa na gari!!! Nilivyokua na Mimi sina gari naona ugumu baba alioupitia!!!hivyo Hata wewe ukikua utaona kufanya saving ilivyo ngumu
Ukubwa gani, na Nina zaidi ya nusu muongo
 
Wazo huenda likawa zuri lakini ujue kuwa mfumo wetu wa maisha ni tofauti na wa Wazungu.

Sisi tunaongozwa na matukio,yani,panapokuwa na tukio ndiyo tunawajibika. Kwahiyo,haijalishi kuna matukio mangapi. Huwezi kubajeti. Hapa muda si mrefu nimepigiwa simu baba mkubwa ni hoi taabani. Ana watoto wake,lakini, wamechoka. Mimi mtoto wa mdogo wake ndiyo naokoa jahazi hapo. Huku nina watoto wa dada ambao baba zao hawajawahi kujitokeza ninawasomesha.

Aidha, nikija afya yangu mwenyewe. Bima ya afya haitoi huduma kwa 💯. Nikiugua hapa gonjwa kuubwa, mshahara huohuo uniuguze.

Hapo mke wangu ni mama wa nyumbani, zigo la home mke na watoto ni mimi.

Mzungu anafanikiwa kwakuwa wao mfumo wao wa maisha ni nyoofu, linear. Mzungu anaweza kujua katika miaka mitano ijayo ,ataishi na watu wangapi. Anajua kabisa mtoto wake X ,ikifika mwaka Y anaondoka home. Sisi fanya tathmini tu, kwa mfano, hili kundi limemaliza vyuo mtaani wanaishi wapi.

Haya ni machache tu, hiyo akiba tunaweka haikai. Ndiyo maana baadhi wanakuwa wabadhirifu. Pesa ya mbongo haiwekeki kwenye bajeti. Wengi wakipata fursa wanajilimbikizia mali ili kukabiliana na majanga yasiyotabirika.Sisi unaweza kuwa mbunge au waziri na bado ukafa masikini. Maana jamii nzima inakutazama wewe.

Ungeshauri tujiongeze labda, kuwa na vyanzo vingine vya mapato.Hii inasaidia sana.
 
Research topic nzuri hii ... Ila usiweke leading questions
 
Kwa hiyo unatuona kama hatuna akili au?
Hivi unadhani mishahara inatosha mpaka kufikia hatua ya kuweka akiba? Mtu wa daraja C.. anapokea 400000,hapo ni hana mkopo, hivi huyu mtu anaweza kuweka akiba?
 
Kwa hiyo unatuona kama hatuna akili au?
Hivi unadhani mishahara inatosha mpaka kufikia hatua ya kuweka akiba? Mtu wa daraja C.. anapokea 400000,hapo ni hana mkopo, hivi huyu mtu anaweza kuweka akiba?
Co ugomvi ndugu, ni wazo. Hiyo ni changamoto nimeiona hata kwangu
 
Akiba ya kimasikini haikai benk mkuu.Weka genge la nyanya au mkaa au matunda au kiduka n.k hapo utakuwa umefanya saving..
 
Mbunge aliwakumbusha kuwa wafanya kazi wanakopa mpaka SONGESHA!Sasa hiyo 10000 hatakuwanayo?.
 
Sio kwamba watu wana bweteka. U can only save if there is surplus.
Mshahara wenyewe kumaliza mwezi shida mpka ukope, hiyo saving utaipataje?
 
Bado magendo,bidhaa feki na biashara zingine haramu,lkn yule mtu anaetafute kihalali kamwe hawezi toboa

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Wazo Bora kabisa,umenena vyema kabisa mfano halisia ktk halmashaurinnayofanyia KAZI ,mama mmoja amebakisha miaka5 asitaafu kutoka ktk utumishi wake ,alifukuzwa KAZI,lkn hakua amesave kitu chochote wala hakuna kitegauchumi kokote Kule,kwasasa anaishi maisha yafedheha nakulima kmaa mlalahoi mwingine tu.umetutoa gizani nakutukumbusha Jambo la maana Sana.
 
Kusave ni kujinyima, Sasa watumishi wengi hawako tayari kujinyima ili wawe na akiba kwasababu wana uhakika wa mshahara mwisho wa mwezi, tofauti na wafanyabiashara ambao asilimia kubwa ni wabahili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…