Kwanini Wakristo hawavui viatu wakiingia Kanisani? Mbona Musa aliambiwa avue viatu?

Kwanini Wakristo hawavui viatu wakiingia Kanisani? Mbona Musa aliambiwa avue viatu?

Anasema yeye kuwa wa kwanza kusilimu miongoni mwao.
- Tangu kuzaliwa kwake mpaka anaingia kwenye hilo pango na umri wa miaka 40 alikuwa ana-practice dini ipi?

Kwahiyo kipi kilitangulia? Utume wake au kitabu chake?
- Nguzo za uislamu zilikuwepo kabla ya Quran?

Ukristoni, Agano la kale ni kabla ya Yesu na Agano jipya ni baada ya Yesu.
  • Kabla ya Yesu hakuna wafuasi wa Kristo, baada ya Yesu kuna wafuasi wa Kristo.
  • Hapa, inawataja wooote kuanzia Yohana mbatizaji kurudi mpaka kwa Adamu, na baada ya Yesu, ni yeye, wafuasi wake na Roho Mtakatifu.
Hakuna mahali Injili, Torati au Zaburi zina mtaja Mtume Mohammed, hakuna popote, mwenye ushahidi aweke hapa.

Lakini Yesu anatajwa katika Quran yao, kwahiyo Ukristo au Yesu hahuhitaji utambulisho katika Uislam , lakini Uislam wana tumia nguvu nyingi kulazimisha Muhammed atambulike ili hali hakuna hata nukta alipotajwa katika Vitabu hivyo juu.
 
Tafsiri
“Alipomwambia Mola wake Silimu! Akasema nimesilimu kwa Mola wa walimwengu wote.”
Nieleweshe, kusilimu na kujisalimisha zina maana sawa? Na lipi ni neno sahihi la kiarabu lililotumika kwenye hiyo aya?

Kama ni kusilimu, dini ya Ibrahimu ilikuwa ni ipi kabla hajasilimu?

Na kama alisilimu kuwa Islam, ni vipi Muhammad aseme yeye ni wa kwanza kusilimu.

Mwisho, maandiko haya asili yake ni nani?
  • Ni nani aliyeuzungumza uislamu kabla ya Muhammad?
  • Kabla ya karne ya 7 mpaka ya 10, nani aliujua uislamu?
  • Tumeona wakureshi wakisema Allah kuwa na watoto watatu wa kike kwa mujibu wa wasomi wa historia, ndiye huyu Allah aliyemsilimisha Ibrahimu?
 
Ukiandika "mungu" unamaanisha "shetani." Katika 2 Kor 4:4 shetani anatajwa kuwa ni mungu wa dunia hii.
Kamwe shetani hastahili kuheshimiwa. Ndio sababu nimewashauri watu wakiandika jina lake waanze na herufi ndogo
So negative kwahiyo mungu anaelewa nukuu ya erufi kubwa tu, ? mungu hayupo hivyo unakosea sana.
 
Yesu alikuwa Muyahudi kama kabila, lakini alifundisha habari njema kwa watu wote, walio mfuata yeye ndio wakristo, maana yake alifundisha ujumbe aliokuja nao yeye (Injili) na kuendeleza mafundisho ya kabla yake.
safi sana upo sahihi sasa jiulize hizi dini sijui ulokole, usabato na uislam zina maana gani zaidi ya kugawa watu katika imani ni wazi ni mpango wa siri wa shetani kuwapoteza watu yesu hakuanzisha dini.
 
Hao washirikina wa Makka walivyotumia jinahilo ndiyo lisiwe halali je washirikina wa Tanzania wanavyotumia jina "Mungu" ndiyo litakuwa siyo halali.
Hawakutumia jina tu, mpaka Kaaba, ile inayosemekana kujengwa na Mtume Ibrahimu(sikumbuki vizuri) ilikuwa ni yao sio?

Na muendelezo wa hayo ukawa ndo Muhammad, kuonekana amerogwa kisha kuhakikishiwa na mkewe kuwa yeye ni mtume wa Mungu, ndivyo?
  • Kwamba kurogwa kwake hakukuathiri wahyi aliyoshushiwa, kwakuwa alikuwa akilindwa na Allah.
  • Aliwahi kumlinda swahaba wake kwa kuchora mstari chini mchangani, viumbe watatu wakashindwa kuuvuka kumfikia swahaba, hii si sehemu ya ushirikina?
 
Wapi ametajwa
Kama Isa ni yesu, basi Isa ametajwa mara 25 kwenye Quran, Muhammad mara 4.

Na mama wa Isa katajwa kwa jina kwenye Quran, na kapewa Surah, hakuna mwanamke mwingine yeyote aliyetajwa kwa jina kwenye Quran ila yeye!

Na ni Isa pekee alichukuliwa kwa Allah, sio mtume mwingine yeyote.

Na ni Isa pekee aliyezaliwa bila baba na akaweza kuumba na kufanya miujiza kwa mujibu wa Quran, sio mwingine yeyote.
 
Kama Isa ni yesu, basi Isa ametajwa mara 25 kwenye Quran, Muhammad mara 4.

Na mama wa Isa katajwa kwa jina kwenye Quran, na kapewa Surah, hakuna mwanamke mwingine yeyote aliyetajwa kwa jina kwenye Quran ila yeye!

Na ni Isa pekee alichukuliwa kwa Allah, sio mtume mwingine yeyote.

Na ni Isa pekee aliyezaliwa bila baba na akaweza kuumba na kufanya miujiza kwa mujibu wa Quran, sio mwingine yeyote.
Isa siyo yesu
 
Kwanini wakristo hawavui viatu wakiingia kanisani? Mbona Musa aliambiwa avue viatu?

☝️☝️Hapo nijibu nini? Ulichotaka nijibu ungeandika kwenye title ,title ndiyo inabeba kila kitu ,ukibadilisha context basi hiyo title iendane na context uliyobadili.
Elimu ni bahari. Nakushauri ukasome communication principles ili ujifunze kutofautisha headline na content. Lakini kama unahisi umri wako umeenda, usipoteze muda, soma tu Biblia, maana Yesu yu karibu kurudi.
 
Aya niambie sasa wapi yesu katajwa kwenye Qur’an kama ulivyodai
Surah 3:45, 4:157, 4:171, 5:110, Surah 9, Surah 4, 5

Hapo, hulamaa wenzio walikuwa wanachanganya kuwa hizo ayat zinamtaja Yesu, wakanifundisha hivyo.

Nadhani walichanganya baada ya kuona, Maryam na Marry zinafanana, wote walizaa bila kumjua mwanaume na watoto wao wakiwa wakiume na wakihusishwa na Mungu huku na kule
 
Surah 3:45, 4:157, 4:171, 5:110, Surah 9, Surah 4, 5

Hapo, hulamaa wenzio walikuwa wanachanganya kuwa hizo ayat zinamtaja Yesu, wakanifundisha hivyo.

Nadhani walichanganya baada ya kuona, Maryam na Marry zinafanana, wote walizaa bila kumjua mwanaume na watoto wao wakiwa wakiume na wakihusishwa na Mungu huku na kule
Sawa hizo zinamtaja Isa bin Maryam sasa niambie zile ulizokuwa unasema zinamtaja yesu
 
Basi wewe ulidandia nilipomreply mwingine ndio maana mimi nikajua wewe
Mkuu, ni sawa, haina shida!

Kwako tukubaliane kuwa;
  • Yesu si Isa
  • Allah si Mungu wa Biblia
  • Uislamu ni dini halal ya Allah na Muhammad ni Mtume wake
  • Ukristo ni imani

Hakuna sababu ya uislamu kutafuta uhalali dhidi ya ukristo, na hakuna sababu ya waislamu kuhangaika na uhalali wa ukristo.
 
Mkuu, nilisoma na sehemu pekee uliyoamua kuhusianisha jina la Allah na Mungu ndipo nilipoona umeamua kuwa biased...

Allah lilitumika na wapagani wa kiarabu wa kabila la wakureshi Mecca kumtaja mungu wao, hili hukulisema.

Kwamba pale Mecca, walikuwa wakiabudu watoto wa Allah, Al-lat, Al-Uzza na Manat, wote wakiwa watoto wa kike, kwamba hawa ndio watawaweka wao karibu na Allah baba yao.

Na Kaaba ndo ilikuwa sehemu yao ya ibada, ikiwa na miungu midoli kama Habal. Kaaba pia ikawa ni nyumba ya Mungu wao Allah

Kwahiyo, Muhammad akaamua kulitakasa jina la Allah kuwa ndio Mungu wa Tawhid yao.
Nijaribu kukufafanulia na hapa kama utaelewa muendelezo ya maelezo uliopewa hapo juu

Neno Allah, ni synonymous ya neno Mungu kwa kiswahili, God kwa kingereza, Zumbe kwa kisambaa, Mnungu kwa kizigua na popote linapotumika hilo neno itakuwa either mtumiaji amemaanisha Mungu/Allah/God/Zumbe/Mnungu wa kweli au masanamu au milima ya kwao

Hivyo hivyo waarabu walikuwa na miungu/Allah/Gods/Wazumbe yao masanamu waliowapa jina la Uzza na manat. Alipowajia Mtume kutokana na wao kuwaambia habari za Allah/God/Mungu wa kweli na sio hao masanamu yao yenye hayo majina ndio wakampinga na kuona ni muongo kama wafanyavyo kaumu/ummah nyingi zilizopita kuwakataa mitume

Hapa chini Mungu anawaambia makafiri wa kiarabu kuwa, je wanawafanya uzza na manat kuwa ndio miungu kuliko Mungu mkuu? Sasa wewe ukiona tu ametajwa Allah basi waona ndio Mungu wa waislam hata kama hilo neno limetumika kurefer miungu ya masanam ya kikafiri wakati huo
 

Attachments

  • Screenshot_20250805-193855.png
    Screenshot_20250805-193855.png
    50.1 KB · Views: 15
  • Screenshot_20250805-193915.png
    Screenshot_20250805-193915.png
    81.6 KB · Views: 16
Mkuu, ni sawa, haina shida!

Kwako tukubaliane kuwa;
  • Yesu si Isa
  • Allah si Mungu wa Biblia
  • Uislamu ni dini halal ya Allah na Muhammad ni Mtume wake
  • Ukristo ni imani

Hakuna sababu ya uislamu kutafuta uhalali dhidi ya ukristo, na hakuna sababu ya waislamu kuhangaika na uhalali wa ukristo.
Sawa ila nataka niulize tu wakristo wa miungu mingapi
 
Back
Top Bottom