Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya Darasa la Saba?

Turudi katika maada mtoto anatakiwa asome masomo mbali mbali ambayo yatamsaidia kuwa na atleast basic knowladge ili kupata hao wataalam wanasayansi inabidi pawe na uwekezaji mkubwa katika elimu kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka vyuoni pia waencourage zaidi learner centered curriculum ambayo ni very expensive
Sawa mkuu
 
Ninachotaka kusema na uelewa wangu juu ya maendeleo na elimu mwanzon nchi nyingi za ulaya walikuwa Wana community centered education curriculum hapa ni kwamba mwanafunzi anasoma apate elimu aisaidie jamii inayomzungunguka later on wakaboresha ili kuruhusu ubunifu katika ujuzi
Okay...
 
Inabidi kuwa na juhudi za makusudi kupitia mitaala ya elimu yetu. Kuna masomo unaona ya na Faida lakini kinachofundishwa huko hujui utakitumia vipi kwa mazingira ya kwetu. Somo Kama la historia lingejikita zaidi kwenye mazingira ya TZ halafu mengine ni Ziada. Shida inakuja kwenye vitabu vya ziada na kiada ...! Watz hatuandiki historia zetu ili katika vitabu ili vitumike kama Rejea mashuleni.
 
Inabidi kuwa na juhudi za makusudi kupitia mitaala ya elimu yetu. Kuna masomo unaona ya na Faida lakini kinachofundishwa huko hujui utakitumia vipi kwa mazingira ya kwetu. Somo Kama la historia lingejikita zaidi kwenye mazingira ya TZ halafu mengine ni Ziada.
Umenena vema mkuu...
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza "directly" na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya darasa la saba na sio kusubiri mpaka afike kidato cha pili?

Yale masomo saba ya msingi yabaki palepale ambayo ni BIOLOGY, GEOGRAPHY, HISTORY, KISWAHILI, ENGLISH, CIVICS, BASIC MATHEMATICS.

Yaani kwanini mwanafunzi aliyepata ufaulu hafifu katika somo la sayansi katika matokeo ya darasa la saba bado analazimika kusoma tena sayansi hiyo hiyo (Physics na Chemistry) kuanzia form I mpaka form II? Huko sio kuwapotezea muda hawa wanafunzi?

Kama ni kweli tunataka kupiga hatua na kuwa na wanasayansi bora hapo mbeleni, kwanini somo la sayansi kwa shule za msingi lisivunjwe mara tatu kisha yakapatikana masomo matatu ya Baiolojia, Fikizia pamoja na Kemia yatakayofundishwa separately kama ambavyo Kiingereza na Kiswahili vinavyofundishwa?

Hayo ni mawazo yangu tu ndugu zangu na ninakaribisha ukosoaji (Constructive Critisism)

NB: Suala la lugha ya kufundishia kati ya Kiingereza na Kiswahili kwa shule za msingi na secondary sio lengo la mada hii ninaomba tusilizungumzie kwa sasa.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Elimu ya sayansi kwa tanzania labda mwisho wa dunia kwa nini !!
Ugumu wa maisha na mjomba siasa kashikilia vyote kuliko hata elimu ya veta kuonekana hina vipaji.

Jeshini kumebaki na wavunja matofali na kubeba kilo hata yule wa tandale anayebeba magunia matatu kamzini.kwa nini ?
Jeshini ndio sehemu za uvumbuzi ukianzia silahaa (Ak47),nyuklia,madawa,magonjwa,kilimo,teknolojia zote.lakini ni afrika tu

Maprofiseli wapo bize na vibinti sio sayansi hata newton kafa bila demu.

Kuna watu wapinga sayansi wamejazana lakini wakiumwa wapo kuomba msaada hapo hapo.

Bajeti za elimu hizi kama ni barakoa bora ziende kusipo na msaada.
 
Mambo huwa yanabadikika
Wanafunzi wasomo masomo yote kwani yote ni muhimu.
Advanced level ndipo watakapochagua nini wanataka kusoma.
 
Jeshini kumebaki na wavunja matofali na kubeba kilo hata yule wa tandale anayebeba magunia matatu kamzini.kwa nini ?
Jeshini ndio sehemu za uvumbuzi ukianzia silahaa (Ak47),nyuklia,madawa,magonjwa,kilimo,teknolojia zote.lakini ni afrika tu
Okay...
 
Maprofiseli wapo bize na vibinti sio sayansi hata newton kafa bila demu.

Kuna watu wapinga sayansi wamejazana lakini wakiumwa wapo kuomba msaada hapo hapo.

Bajeti za elimu hizi kama ni barakoa bora ziende kusipo na msaada.
Umeandika kisela sana mkuu lakini ujumbe mzuri umenifikia
 
Kabisaa.. but english language itabidi iwe compulsory.
NB: Suala la lugha ya kufundishia kati ya Kiingereza na Kiswahili kwa shule za msingi na secondary sio lengo la mada hii ninaomba tusilizungumzie kwa sasa.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu watanzania eti;

Kwanini wanafunzi wasianze kidato cha kwanza "directly" na michepuo ya sayansi (Physics, Chemistry) au arts kwa kuzingatia matokeo ya darasa la saba na sio kusubiri mpaka afike kidato cha pili?

Yale masomo saba ya msingi yabaki palepale ambayo ni BIOLOGY, GEOGRAPHY, HISTORY, KISWAHILI, ENGLISH, CIVICS, BASIC MATHEMATICS.

Yaani kwanini mwanafunzi aliyepata ufaulu hafifu katika somo la sayansi katika matokeo ya darasa la saba bado analazimika kusoma tena sayansi hiyo hiyo (Physics na Chemistry) kuanzia form I mpaka form II? Huko sio kuwapotezea muda hawa wanafunzi?

Kama ni kweli tunataka kupiga hatua na kuwa na wanasayansi bora hapo mbeleni, kwanini somo la sayansi kwa shule za msingi lisivunjwe mara tatu kisha yakapatikana masomo matatu ya Baiolojia, Fikizia pamoja na Kemia yatakayofundishwa separately kama ambavyo Kiingereza na Kiswahili vinavyofundishwa?

Hayo ni mawazo yangu tu ndugu zangu na ninakaribisha ukosoaji (Constructive Critisism)

NB: Suala la lugha ya kufundishia kati ya Kiingereza na Kiswahili kwa shule za msingi na secondary sio lengo la mada hii ninaomba tusilizungumzie kwa sasa.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Hujawahi kusikia mwanafunzi kufaulu vizuri mtihani wa darasa la saba lakini akiingia form one anagundulika hajui hata kuandika jina lake? Hapo ndipo penye shida.
 
Kama mitihani ya darasa la saba haiaminiki, sasa kwanini tuendelee kuamini ubora wa mitihani ya kidato cha pili na cha nne?
 
Kwani la saba miaka hii kuna mtihani au uhuni?
Walimu wanawapa wanafunzi majibu yote, hesabu ni multiple choice.
Nilibahatika kwenda shule ya vipaji 2006/2007. Kule niliwakuta waliopata mpaka 100/100 kwa baadhi ya masomo. Mimi nilipata A 4 na B 1 sikuwa na marks kubwa sana sema tu nilichaguliwa kwakuwa shule ilikuwa kijijini Sana yaani porini na ni changa wakanibeba. Wale niliowakuta na A flat na wengine kupiga 100% kwa masomo 2 au 3 niliwaburuza.
Kigezo Cha matokeo ya la 7 hakina mashiko miaka hii . Kuna vijana walikuja form one na A flat but form four wakatoka na four.
 
Back
Top Bottom