Kwanini wanaompokea Rais Samia huko Manyara wametokea Dar es Salaam?

Kwanini wanaompokea Rais Samia huko Manyara wametokea Dar es Salaam?

Natambua kwamba Mh Rais Samia Ph.D , anaanza ziara ya kikazi Mkoani Manyara , hongera kwake na kwa Wenyeji wake .

Lakini cha kushangaza kwenye ziara hii ni kitendo cha Rais kupokelewa na mamia ya wakazi wa Dar es Salaam ! jambo hili kwangu ni geni mno , Inakuwaje Rais apokelewe na wakazi wa Dar , Je Manyarq haina watu ?

Kwamba Mh Rais naye ameamua kusomba Watu kama anavyofanya Chongolo ili kuongeza Uwingi wa watu ?

View attachment 2780989View attachment 2780990View attachment 2780992View attachment 2780994
Duuh kikosi kazi
Anayelalama yupo songwe sisi watu wa manyara hatujasema kitu!
 
Kumbe hata huelewi wanazikimbilia fursa za kuonana na mama?

Watu wakielewa tu mama ana ziara ya huku au kule, wanawahi mapema kabisa, hata mimi nikisikia na nikiwa na jambo langu nawahi kabisa, huko ndiyo pa kumpata kiwepesi.

Unafikiri ni wepesi kupata appointment Ikulu Dodoma au Dar? Utasota, tena unaweza kufanya appointment Dar ukapigiwa siku moja au mbili kabla ukaulizwa unaweza kwenda Mtwara, huko unaweza kumpata keshokutwa tutakuwekea slot yako kabla ziara hazijaanza. Ukiweza unakwenda au unawaambia mie ntasubiri mpaka nimpate hapahapa tu.

Ziara hizo zina faida sana. Mwenyewe saa nyingine anasangaa, akikuona anakuuliza, na wewe upo hapa? Hapana mama nimekuja kukuona wewe, una shida gani? Unamwagika hapo kwa raha zao.

Kitu nnachompendea mama Samia, hajawahi kukataa shida au ombi la mtu hata iweje, labda liwe halipo kabisa kwenye uwezo wake, nalo pia atakwambia ukweli, hili inabidi nilifatilie hivi na hivi, lakini utatafutwa. Basi ujuwe kweli atalifanyia kazi tena wakati huohuo, hana ngoja baadae huyo.


Mama samia Mweyezi Mungu amzidishie hekima maarifa na upendo alionao kwa Tanzania.


Jinsi anavyochapa kazi huyu mama, mpaka vijana wenyewe wanashika kiuno, muulizeni Zuhura Yunus, anaipatapata. Mie nadhani huyu mama Ma shaa Allah ni nusu robot.
Umesoma vyema ulichoandika?
 
Kwamba ili kusaidiwa nchi hii ni mpaka uonane na Rais ?
Sikiliza kijana, hakuna mtu anayetafutwa kuonana na watu Tanzania hii zaidi ya Rais. Na hii si Tanzania tu, karibia nchi zote duniani ni hivyohivyo.

Watu wana mambo yao mbalimbali, usifikiri wewe kwa kuwa yako yanaweza kuishia hukuhuku mitaani basi wote ni hivyo hivyo.
Acha uongo wewe, basi kusingekuwepo na watendaji wengine. Muongo sana wewe Ajuza.
 
Acha uongo wewe, basi kusingekuwepo na watendaji wengine. Muongo sana wewe Ajuza.
Kwani ulikatazwa kuwaona watendaji wengine? Sasa uongo uko wapi hapo?

Mimi siyo wale ambao amri zao kumi hakuna inayosema "usiseme uongo".
 
Mama amezungukwa na Machawa sijui kama anajua hali halisi ya Maisha ya dhiki wanayopitia Watanzania
"Maisha ya dhiki wanayopitia waTanzania"?

Umeziangalia vizuri hizo picha mkuu 'imhotep', na kuona mtu mweye kuonyesha maisha ya dhiki katika hao wote walioonyeshwa kwenye picha?

Huu ndio "uwekezaji" anaouhimiza mama kila mahali. Yeye mwenyewe yupo mstari wa mbele kutekeleza "maono" yake ya uongozi.

Kuna mahela chungu nzima, mama hajui ayatumie vipi. Hao unaowasema kuwa na "dhiki" tatizo lao ni kutojua tu jinsi ya kumfanya mama ayatumie kwao.

Waeleze hao "waTanzania" wako jinsi wanavyoweza kunufaika. Kama nawe hujui, waulize hao wanaonufaika sasa waliweza vipi kuwa kitega uchumi kwa mama.
 
Usichokijua Huo Ni Mchanganyiko Wa Chawa Na Kunguni Sasa Hapo Wanatafuta Connection Kama Ujuavyo Nchi Imefunguka
Tukizima Mwenge Ziara Singida Mpaka Tabora
Kote Huko Utaona Chawa Na Kunguni Wengi Sana Sana
 
Natambua kwamba Rais Samia Ph.D, anaanza ziara ya kikazi Mkoani Manyara, hongera kwake na kwa Wenyeji wake.

Lakini cha kushangaza kwenye ziara hii ni kitendo cha Rais kupokelewa na mamia ya wakazi wa Dar es Salaam! jambo hili kwangu ni geni mno, Inakuwaje Rais apokelewe na wakazi wa Dar, Je Manyarq haina watu?

Kwamba Rais naye ameamua kusomba Watu kama anavyofanya Chongolo ili kuongeza Uwingi wa watu?

View attachment 2780989View attachment 2780990View attachment 2780992View attachment 2780994
Sasa wewe ulitaka apokelewe na akina Dr. Slaa?
 
Back
Top Bottom