Kwanini wanaume wengi wanaogopa kuoa wanawake wapambanaji na wanaojielewa?

Mutuache wanaume tuwe huru kuoa wanawake tunaowataka, kwa ajili ya furaha na amani yetu
Upambanaji wenu utumieni kujenga maisha yenu, na watoto wenu
Sasa watu mnataka amani,
Badala ya kuoa wasiosoma ili mpate amani lakini mmekazana kuoa vichomi waliosoma.
Haki mnachokitafuta wanaume hamkijuiπŸ™†
 
Ndani huyo mwanaume huwa anasaidia kupiga deki na kupika?.
 
Unapenda support ya mke
Na we unatoa support ya majukumu yake nyumbani?

Mana usilaumu wkt ukifika home mwanaume unageuka mdoli/mwinyi mkuu hugusi kitu

Ndoa kukubaliana/kusaidiana
Ukijigusa kutoa mkono majukumu ya nyumbani hata ye hatoona uzito siku unakwama kifedha
 
Kwanza hamna ndoa kama hiyo na haito kuwepo unajidanganya na kujitia moyo na hata ikiwepo haitodumu ,hiyo ndio nature eti mgawanyo wa majukumu ya nyumbani hamna ndoa kama hiyo.

Kwanza kitu kinachoitwa 50/50 hamna bali michongo ya watu kuzipiga hela za wazungu kwenye hizo NGO.

Utabisha utakataa mwanamke kwenye hela yake mbinafsi, kwenye nyumba mwanamke akiwa na 1mil mwanaume laki 3,nyumba ina laki tatu, 50/50 mnaipenda maeneo yote,ila ya kishagusa kipato chenu mnakuwa wa binafsi, hata mwanaume awe anafua na kuosha vyombo, ila ikija kwenye HELA YA MWANAMKE hamna 50/50.

Ndio maana wengine wanaamua kuoa mama wa nyumbani na kumfungulia biashara hapo home basi na kuna wengine wanafikia hatua ya kuwaachisha kazi wanawake sababu haoni msaada wa mke wake.

At the end of the day ndoa itadumu mkiishi kwa misingi yake kiasili, mwanaume atakula kwa jasho na kuwa KICHWA CHA FAMILIA,mwanamke wewe utakuwa unafuata muongozo wa mwanaume na si vinginevyo.

NB:Wapo wanawake watafutaji na wasomi ila wanajua nafasi na wajibu wao ni upi katika familia zao na mme wake na ukichunguza wengi wameshiba imani (kikristo au uislam) percent yao ni ndogo approximately equal zero na hawaendeshwi na upuuzi huu wa 50/50.
 
50/50 ni upuuzi sn chief
Bora umeliona hilo..

Ila raha ya kusaidiana na mume
Inategemea na jamaa mwenyewe
 
Kutokujiamini, na pia wasi wasi wa kupigwa matukio...
 
Mwanamke hajaumbiwa kumiliki . Ikitokea akamiliki uchumi atahitaji kutawala pia Kitu ambacho aliumbiwa mwanaume
 
Kwasababu mwanamke anaejiita mpambanaji na msomi hua na hulka ya kutaka kuishi kama mwanaume ndani ya nyumba.

Imeandikwa, mwanaume atamuoa mwanamke. Na sio mwanaume atamuoa mwanaume mwenzake.
Ndio maana umepata like nying kuliko mleta mada mnk umejibu [emoji817]
 

Kwa sababu ataanzisha mapambano ndani ya nyumba.
 
Huko ulaya kwenyewe 50/50 hamna
 
Hakuna ugolikipa mkuu, ku manage nyumba ni shughuli pevu sana.
 
Hakuna ugolikipa mkuu, ku manage nyumba ni shughuli pevu sana.
Sasa kama hamtaki wanawake magolikipa ndiyo mjue kuwa wanawake wakifanya kazi lazima wakose muda wa kufanya kazi za nyumbani! Kwahiyo ni either mume asaidie au aletwe housegirl bila kelele za kwamba yeye ndiyo anafanya kila kitu!
 
Sina uhakika ila kama ni kweli basi huwa hivi.

Kama mwanamke anapambana, atashindwa kupambana na mimi?


Kama mwanamke anajielewa, ataweza kunielewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…