Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Mimi nadhani sehemu kubwa ya viwanda au taaisis kushindwa kuperform ilikuwa too mucha siasa.. Sio kuwa watu hawakuwa na uwezo. Ni Mameneja na wakuruengezi hawakuepewa uwezo na mdaraka ya kufanya maamuzi.
...Right on! And the game still continues!
 
Mimi nadhani sehemu kubwa ya viwanda au taaisis kushindwa kuperform ilikuwa too mucha siasa.. Sio kuwa watu hawakuwa na uwezo. Ni Mameneja na wakuruengezi hawakuepewa uwezo na mdaraka ya kufanya maamuzi.

Chukulia mfano wa TANESCO
TANESCO
Chini ya viongozi na wakurungezi wa Kitazania haikuwa rahisi au walizuiwa kufanya mamauzi fulani. Tanesco wasingeweza kukata umeme Hospitali ya Bugando au muhimbili au wasingeweka kukata umeme Ikulu ndogo au wizara fuani . Wakienda kukata umeme Ofisi ya RC, RC Anapigia waziri wa nishati. Waziri wa Nishati anampigia Mkurugenzi wa Tanesco unaweza kujua........
LAkini hayo hayo madeni waliyokuwa wanadai tanesco ya watanzania wakaja Netwgroup. Wao tena wakapewa na masharti ya 10% kulingana na mapatazo watayokusanya. Walichofanya netgroup hata mimi ningefanya. Ni kukomalia yale maedeni ya TANESCO orginal ( Madaia mkubwa ni serikali). Tukasikia sifa kem kem za kisiasa kuwa Netgroup Slution wameweza kile Tanesco ya watanzania ilichoshindwa. Zanzibar inapata umeme kwa gharama za Kisiasa hawaipi deni au tarrrfi sahihi za soko . Meneja harusiwi kukata sabau za kisiasa Netgrup wao wanaruhusiwa....... Sasa mambo ama haya hapa ni lawama chache sana zinakwenda kwa Viongozi wa Tanesco....
Ka hiyo utaona baadhi ya visababu vya ya umasikini wetu kwanza hatuaminiani . Tunadhani suuisho la mataizo yetu ni kutoka kwa TX fuani wa nje . Iikuwa rahisi wa wanasiasa kuruhusu NETGROUPwapewe 10% ya lile deni la tanesco lakini hawakuwai ufirkira haata siku moja kuwaambia tanesco watapewa 10% ya deni wataloweza kudai na na kurecover.

Suprise Suprise !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mzungu anakuja na , mwanasiasa anampa uwezo wa kufanya vyote. Mkenya anakuja anapewa kiwanda cha makaratasi anaweza kuendesha kwa kutumia mitambo hilehile mtanzania aliyoshindwa kuitumia. Mkiulizwa mnasema siasa ndio tatizo.

Lini watanzania mtaacha kuchukua personal responsibilities?
 
...Its more than that, my friend. Unaangalia malighafi unapata wapi. Je, chuma ilishaanza kuchimbwa na kuyeyushwa huko Liganga? Halafu, skills, established supporting infrastructure, getaway to markets, lengo la kuanzisha kiwanda, and the list goes on. Wakati mwingine location ni swali gumu sana katika kupanga mradi.

...Ungeniuliza, ningependekeza most of them, not all, to be based in Mtwara [you may argue, with the benefit of hindsight].

Makarabashi yangu YAnaonyesha mradi wa chuma ulikuwepo kwenye agenda toka 1963. Na ndio ilikuwa sababu ya ujenzi wa TAZARA. Vilevile viwanda vinaamishwa. Mnachofanya hapa ni execuse. Kulikuwa hakuna national strategies.
 
...Je, tulikuwa na sera yeyote ya viwanda kwa ajili ya export na huo mradi ulipitia mchanganuo uliouhakikishia kwamba utaanza vizuri? au tulifikiria kujenga kiwanda bila kujali matokeo, alimradi jamaa wa WB na IMF wamesema? ...Ushasema walikuwa wanapewa. Nani alikuwa anawapa hao wasio na skills? Ukizingatia kwamba karibu viwanda vyote vya maana vilikuwa ni vya umma, nani ni wa kulaumiwa? Je, unafahamu mameneja wa viwanda hivi hawakuwa na uhuru wa maamuzi. Tusiende mbali. Unafikiri TANESCO wangeingia mikataba kadhaa yenye gharama kubwa za kuacha madeni ya kufa mtu, peke yao kama menagement? ...Sasa, hapo kosa la nani? anayemweka mtu wake au huyo mtu?

Kwangu mimi, umuhimu wa maswali kama haya ni kujifunza wapi tulikosea hili tusirudie. Lakini tukianza mijadala kama hii, wenzetu waliopenda mambo ya kiNyerere-Nyerere wanasema alijenga viwanda na waliofuatia wameviuza na kulipa taifa hasara.
 
Suprise Suprise !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mzungu anakuja na , mwanasiasa anampa uwezo wa kufanya vyote. Mkenya anakuja anapewa kiwanda cha makaratasi anaweza kuendesha kwa kutumia mitambo hilehile mtanzania aliyoshindwa kuitumia. Mkiulizwa mnasema siasa ndio tatizo.

Lini watanzania mtaacha kuchukua personal responsibilities?

Zakumu suprise ni surprised ukisema kushidwa basi tubanishe na tuelezne kushindwa kivipi. Nimenadika mfano wa Netgroup kama nimekosea sema netgrup walichofanya ambacho Mkurugenzi yeyote awe masanja au mwakalebela angeshindwa.

Netgroup walikuwa rewarded kwa kuusanya madeni waliyoyakuta. Je walifanya negoatition za kichawi ambazo masanja na mwakalebea walishindwa??? Hwakufanya kitu kipya ni proffesiaal walipewa full authrity ya kufanya maamuzi bia kuingiliwa......

Netgroup wakisema wanakata umeme zanzibar hazina ikachomoa fedha lakini tanesco ya "mwakaebela" au "Masanja" aliyeteuliwa na Rais kukata umeme kwa deni halali ingeweza kuonekana ni uhaini"

Katika Personal responsibiities si kama hakuna tatizo ndipo maana kama umenisoma vizuri kuna sehemu nimeandika hivi..........
.......Sasa mambo kama haya hapa ni lawama chache sana zinakwenda kwa Viongozi wa Tanesco....

It means kuna lawama na uongozi wa Tannaesco na institution unabeba lakini na siasa zimechangia sana.
 
Zakumu suprise ni surprised ukisema kushidwa basi tubanishe na tuelezne kushindwa kivipi. Nimenadika mfano wa Netgroup kama nimekosea sema netgrup walichofanya ambacho Mkurugenzi yeyote awe masanja au mwakalebela angeshindwa.

Netgroup walikuwa rewarded kwa kuusanya madeni waliyoyakuta. Je walifanya negoatition za kichawi ambazo masanja na mwakalebea walishindwa??? Hwakufanya kitu kipya ni proffesiaal walipewa full authrity ya kufanya maamuzi bia kuingiliwa......

Netgroup wakisema wanakata umeme zanzibar hazina ikachomoa fedha lakini tanesco ya "mwakaebela" au "Masanja" aliyeteuliwa na Rais kukata umeme kwa deni halali ingeweza kuonekana ni uhaini"

Katika Personal responsibiities si kama hakuna tatizo ndipo maana kama umenisoma vizuri kuna sehemu nimeandika hivi..........

It means kuna lawama na uongozi wa Tannaesco na institution unabeba lakini na siasa zimechangia sana.

Mtazamaji,

Nakubaliana na wewe kuwa siasa imechangia kwa kiasi kikubwa sana. Na sasa ni miaka 50 toka tumepata uhuru na lini tutajifunza?
 
Zakumi,
Mimi nadhani kuna maswala mawili hapa ambayo yote yanafanyika kimakosa na ndio yanatuchanganya sana..

1. Majukumu ya serikali - Katika mfumo wa Ubepari serikiali haitakiwi kabisa kuingilia utendaji kazi wa mashirika yake au hata binafsi unless huduma hizo zinaathiri wananchi ama kukiuka sheria. Serikali inatakiwa kuwawekea wananchi mazingira ya kisiasa (sera) yanayowawezesha wananchi kuendesha na kukuza Uchumi kulingana rasilimali tulokuwa nazo. Lakini ukitazama kwaundani utagundua kwamba mali yote nchni ni mali ya serikali na serikali ndio wenye mamalka ya kuchagua nani atapewa nini..

Unaweza kuwa na mtaji wako kufungua kiwanda cha Chuma lakini ukanyimwa uchimbaji akapewa Mchina japokuwa machimbo hayo umeyagundua wewe. Kila kitu nchini bado ni mali ya serikali..Tazama hata swala la Tanesco na mashirka mengine yote nchini utagundua kwamba yanaendeshwa na serikali kuu bado na yule CEO aliyepo madarakani anafuata tu mipango iliyokwisha pangwa na serikali. Serikali ndio iloamua tender za uzalishaji umeme apewe nani na sii Tanesco wenyewe au hata wewe ukitaka kuzalisha umeme wa upepo hutatazamwa kama mwekezaji bali ni posa ya kuomba ambayo unaweza kataliwa kwa madai kwamba mpango huo haupo ktk mikakati ya serikali. Mwaka unaofuata likapewa shirika la nje.

Mbunge ni lazima ajue jinsi ya kumfuata waziri ili meadi fulani ufanikiwe jimboni kwake.. Ukikaa tu na kusubiri ahadi za serikali itakula kwako..Na sijui kama wabunge wetu wote wanafahamu hili ama hata kujua kuandika project plan na kuiwakilisha kwa waziri iwe hata mradi wa maji... Majimbo mengi hayapati maendeleo kwa sababu mbunge hakuomba ama kufuatilia serikali kuu. Miradi mingi sana ya miaka 60s na 70s imesimama kwa sababu sio jukumu tena la serikali kuzalisha Chuma ila wananchi lakini pia wananchi hao wanatakiwa kusubiri maamuzi ya serikali ktk uwekezaji wowote ule, wananchi hawana mamlaka kamili ya uwekezaji.

2. Majukumu ya wananchi -
Sisi wananchi wenyewe tunategemea sana serikali yetu ituletee maendeleo japokuwa mfumo wetu wa maendeleo bado unapitia serikali kuu. Unaweza kuamini hadi leo watu wenye TIN number hawafiki mil2, watu wenye account bank hawafiki mil 4, walipa kodi kwa ujumla hawafiki mil 3, sasa kweli tutaweza vipi kufika tunakotaka ikiwa leo tunakata mikoa na wilaya kwa sababu ya uchaguzi badala ya kuirahisiha serikali kazi ya ukusanyaji kodi na maendeleo ya maeneo hayo.

Na kumekuwepo na kupumbazwa na mchanganyiko wa mifumo hii miwili yaani Ujamaa na Ubepari kiasi kwamba kumekuwepo na conflict baina yake. Ni sawa na swala la dini na tamaduni zetu, yaani leo utamsikia Muislaam akilaani Pombe lakini anaenda kwa waganga wa kienyeji na wapiga bao (ramli), Utamsikia Mkristu akinywa Pombe kama vile hilo ni swala la Waislaam (upinzani) yeye karuhusiwa japokuwa haliruhusiwi ktk Ukristu. Ukienda harusi au misiba za kiislaam/kikristu utakuta mengi ya kiasili yamechukuliwa pia ambayo kidini ni haramu kubwa...Tunafanya mambo mengi ya kiasili ndani ya dini hizi bila kujijua na ndio maana tupo ktk mgogoro wa kiimani.

Kwa hiyo, nakubaliana na wewe sana tu ktk kuwaamsha Watanzania ya kwamba ifike wakati tukubali tunakosea wapi.. Na hakuna wakati mzuri sana kama huu wa kuunda KATIBA MPYA. Tuache kabisa hizi hadithi za mgawanyiko baina yetu kupitia vyama au dini na tuijenge katiba ambayo itatuwezesha sisi wananchi kutofanya makosa au uzembe uliokuwepo.
 
Tanzania ni masikini kwa sababu ya mfumo wa utawala. Tumejenga mfumo wa utawala ambamo viongozi hawawajibishwi na wananchi. Kwa hiyo kufeli kwa sera za nyerere za viwanda kulitokana na watu waliokuwa wamepewa majukumu ya kuviendesha kutokutekeleza wajibu wao ipasavyo bila kupewa adhabu yoyote. Kuwa kwake viwanda vya umma hakukuwa sababu ya kuvifanya vianguke kwa sababu nchi nyingi sana za kibepari zimewahi kuwa na makampuni ya umma na yakafanikiwa. Sehemu kubwa ya makampuni vya China leo ni vya umma na vinafanikiwa.

Mfumo huo ndio unaofanya viongozi wa serikali wauze raslimali za nchi kwa watu wa nje bila kujali kuwa kufanya hivyo wanazidi kuwadidimiza wanachi.

Ili tujikomboe na umaskini tunahitaji mambo mawili tu:

(1) Fukuza CCM
(2) Katiba mypa yenye kutoa nguvu kwa wananchi, siyo kwa viongozi.
(3) Tutunge sheria inayotoa adhabu kali kwa mtu yeyote anayegundulika kuonyesha matendo ya kivivu katika maisha yake ya kila siku. Sheria hiyo itakuwa na metrics za kupima uvivu.
 
Zakumi,
Mimi nadhani kuna maswala mawili hapa ambayo yote yanafanyika kimakosa na ndio yanatuchanganya sana..

1. Majukumu ya serikali - Katika mfumo wa Ubepari serikiali haitakiwi kabisa kuingilia utendaji kazi wa mashirika yake au hata binafsi unless huduma hizo zinaathiri wananchi ama kukiuka sheria. Serikali inatakiwa kuwawekea wananchi mazingira ya kisiasa (sera) yanayowawezesha wananchi kuendesha na kukuza Uchumi kulingana rasilimali tulokuwa nazo. Lakini ukitazama kwaundani utagundua kwamba mali yote nchni ni mali ya serikali na serikali ndio wenye mamalka ya kuchagua nani atapewa nini..

Unaweza kuwa na mtaji wako kufungua kiwanda cha Chuma lakini ukanyimwa uchimbaji akapewa Mchina japokuwa machimbo hayo umeyagundua wewe. Kila kitu nchini bado ni mali ya serikali..Tazama hata swala la Tanesco na mashirka mengine yote nchini utagundua kwamba yanaendeshwa na serikali kuu bado na yule CEO aliyepo madarakani anafuata tu mipango iliyokwisha pangwa na serikali. Serikali ndio iloamua tender za uzalishaji umeme apewe nani na sii Tanesco wenyewe au hata wewe ukitaka kuzalisha umeme wa upepo hutatazamwa kama mwekezaji bali ni posa ya kuomba ambayo unaweza kataliwa kwa madai kwamba mpango huo haupo ktk mikakati ya serikali. Mwaka unaofuata likapewa shirika la nje.

Mbunge ni lazima ajue jinsi ya kumfuata waziri ili meadi fulani ufanikiwe jimboni kwake.. Ukikaa tu na kusubiri ahadi za serikali itakula kwako..Na sijui kama wabunge wetu wote wanafahamu hili ama hata kujua kuandika project plan na kuiwakilisha kwa waziri iwe hata mradi wa maji... Majimbo mengi hayapati maendeleo kwa sababu mbunge hakuomba ama kufuatilia serikali kuu. Miradi mingi sana ya miaka 60s na 70s imesimama kwa sababu sio jukumu tena la serikali kuzalisha Chuma ila wananchi lakini pia wananchi hao wanatakiwa kusubiri maamuzi ya serikali ktk uwekezaji wowote ule, wananchi hawana mamlaka kamili ya uwekezaji.

2. Majukumu ya wananchi -
Sisi wananchi wenyewe tunategemea sana serikali yetu ituletee maendeleo japokuwa mfumo wetu wa maendeleo bado unapitia serikali kuu. Unaweza kuamini hadi leo watu wenye TIN number hawafiki mil2, watu wenye account bank hawafiki mil 4, walipa kodi kwa ujumla hawafiki mil 3, sasa kweli tutaweza vipi kufika tunakotaka ikiwa leo tunakata mikoa na wilaya kwa sababu ya uchaguzi badala ya kuirahisiha serikali kazi ya ukusanyaji kodi na maendeleo ya maeneo hayo.

Na kumekuwepo na kupumbazwa na mchanganyiko wa mifumo hii miwili yaani Ujamaa na Ubepari kiasi kwamba kumekuwepo na conflict baina yake. Ni sawa na swala la dini na tamaduni zetu, yaani leo utamsikia Muislaam akilaani Pombe lakini anaenda kwa waganga wa kienyeji na wapiga bao (ramli), Utamsikia Mkristu akinywa Pombe kama vile hilo ni swala la Waislaam (upinzani) yeye karuhusiwa japokuwa haliruhusiwi ktk Ukristu. Ukienda harusi au misiba za kiislaam/kikristu utakuta mengi ya kiasili yamechukuliwa pia ambayo kidini ni haramu kubwa...Tunafanya mambo mengi ya kiasili ndani ya dini hizi bila kujijua na ndio maana tupo ktk mgogoro wa kiimani.

Kwa hiyo, nakubaliana na wewe sana tu ktk kuwaamsha Watanzania ya kwamba ifike wakati tukubali tunakosea wapi.. Na hakuna wakati mzuri sana kama huu wa kuunda KATIBA MPYA. Tuache kabisa hizi hadithi za mgawanyiko baina yetu kupitia vyama au dini na tuijenge katiba ambayo itatuwezesha sisi wananchi kutofanya makosa au uzembe uliokuwepo.

Mkandara,

Kwa mtanzania yoyote mwenye kuipenda nchi yake, suala la kwanini Tanzania ni masikini lipo vichwani kwa miaka mingi. Na suala zima sio sayansi au uhandisi au hisabati.

Kwenye suala la matatizo ya maendeleo ya Tanzania huwezi kusema leo unajumlisha mbili na mbili na kupata nne kama ilivyo kwenye hesabu.

Ufumbuzi wa matatizo wa maendeleo ya maisha yetu, unatakiwa kuwa na mbinu nyingi na ambazo zinabadilika kutokana na wakati na matatizo yanayokabili nchi.

Na kwa sababu zinazojulikana na zisizojulikana tumehamua kufuata demokracia ya nchi magharibi, basi watu na serikali na umuhimu katika maendeleo ya nchi.

Watu ni lazima wawe wajasiri kuchagua viongozi na kuwaondoa kutoka madarakani. Hii itawezesha wale wenye uwezo wa kutafuta ufumbuzi wa kutatua matatizo yaliopo sasa wafanye kazi. Kwa mfano, Tanzania kwa sasa inakabiliana na matatizo ya kifedha. Hivyo kuwepo na serikali inayoongeza mikoa na wilaya ni kutolisaidia taifa. Na kama kuongeza idadi ya mikoa ni kuleta maendeleo, basi mikoa ya Singida na Dodoma ingekuwa mbali.

Serikali nayo iwe na wajibu katika kuondoa umasikini. Lakini tukumbuke kuwa umasikini wetu hautokani na kuporomoka kwa utajiri uliokuwepo miaka ya nyuma. Hivyo mbinu za kuboresha maisha ya watanzania, zitakuwa tofauti na mbinu za nchi zilizokuwa tajiri lakini uchumi wake ulidondoka kwa sababu mbalimbali.

Kwa mfano uchumi wa sasa wa Tanzania ni lazima utegemee kwa kiasi kikubwa unskilled labour. Hii ni kwa sababu watanzania wengi hawasoma vizuri au unskilled workers. Swali je ni uchumi gani utawafaa watanzania wakati wana-build capabilities zao? Je kuanzisha silicon Valley inawezekana?
 
Mkandara,

Kwa mtanzania yoyote mwenye kuipenda nchi yake, suala la kwanini Tanzania ni masikini lipo vichwani kwa miaka mingi. Na suala zima sio sayansi au uhandisi au hisabati.

Kwa mfano uchumi wa sasa wa Tanzania ni lazima utegemee kwa kiasi kikubwa unskilled labour. Hii ni kwa sababu watanzania wengi hawasoma vizuri au unskilled workers. Swali je ni uchumi gani utawafaa watanzania wakati wana-build capabilities zao? Je kuanzisha silicon Valley inawezekana?
Mkuu wangu binafsi yangu nakubaliana na wewe sana tu ktk hili isipokuwa hilo la kuanzisha silicon valley kwa sababu umesha sema tayari sisi tuna hesabu kubwa ya unskilled workers hivyo wakati tunaelimisha wamnanchi wetu ni lazima tutazame mbali na elimu kuna kitu gani kingine ambacho wananchi wetu wamejaliwa nacho na ni chachu ya maendeleo. Na sababu nyingine kubwa sababu ambayo haiendani na biashara ni kutokana na kwamba sisi hatuna skilled workers lakini gharama ya utumishi wetu ni kubwa sana ukilinganisha na sehemu nyingine zozote duniani..
Hakuna Mtanzania anayeweza kufanya kazi kiwandani kwa kulipwa 30 cent per hour!akiondoka na Ths 3,000 kwa siku hivyo mwekezaji yeyote hawezi kuitazama Tanzania ikiwa kuna nchi kibao Asia zina maisha ya chini zaidi. Sisi tuna mishahara ya ajabu ajabu yaani waziri wetu au mbunge anapokea mshahara mkubwa kuliko Mbunge wa Canada kisha anapewa gari, mafuta na malupulupu kibao kwa visingizio vya kwamba mazingira yetu magumu kuliko Ulaya. Yaani huwezi kupima tunawezaje kuwa na serikali kubwa kiasi hiki wakati tunadai kwamba nchi yetu ni maskini.

Na kama ulivyosema hapo juu Suala la umaskini wetu sio sayansi au uhandisi au hisabati isipokuwa ni kama nisemavyo mimi linategemea WATU na MAZINGIRA waliyopo. Hakuna suhulu zaidi ya KILIMO, UVUVI NA UFUGAJI hivi ni vipaji WATANZANIA (watu) tulopewa na Mungu na kujikuta tukiishi ktk nchi yenye rasilimali hizi. Na kama unakumbuka niliwahi kusema kipoaji cha kilimo ndicho kilituponza sisi tukachukuliwa ktk Utumwa kwa sababu Wabantu ni wakulima kwa asili na pia kukoloniwa kumetokana na Afrika ni nchi yenye ardhi yenye rutuba ya kilimo na madini ambayo waliyahitaji makwao.

Lakini tazama tulipokabidhiwa Uhuru wetu, ndio kwanza kila mmoja wetu alitaka kurithi kile alichokiacha mzungu.. Majumba ya Oysterbay, Kawe na Masaki yakavamiwa na wazee wa Magomeni na Kariakoo. Nyerere mwenyewe alitaka kupinduliwa zaidi ya mara nne kwa sababu tu hakutaka kubadilisha vichwa vya watawala toka mzungu kuja Mkoloni mweusi. Na tukampinga sana isipokuwa yote aloyakanya yanajirudia leo hii, tumerudi kule tulikotoka kutaka kuwa kama Wazungu maana hakuna mfano bora wa binadamu na maisha kama ya mzungu na Ulaya.

Wenzetu hawakuzijenga nchi zao kwa kutazama model fulani bali mahitaji yao ndiyo yaliwasukuma kuboresha vipaji vyao ktk elimu ya sayansi na teknologia. Ile sababu ya kwamba KILA UGONJWA UNA DAWA na hakuna kitu kisichowezekana iliwapa ari ya kuvumbua vitu ambavyo viliweza kukidhi mahitaji yao na nchi zao kuendelea hatua kwa hatua.

Sisi ambao tumejaribu Kilimo kwanza -mtumeee, ndio kwanza tukampiga chini Mwandosya kwa sababu alikuwa hakubaliani na mpango wa GMO seeds ambazo ni biashara kubwa ya maabara za nje. Tukaingiza pembejeo za ajabu ajabu, mbolea inatolewa kwa voucher utadhani zaka za walfare ili mradi madeal tunagawana deal. Nchi inazidi kupata ukame kutokana na visima vya maji kuchimbwa kila kona kwa matumizi ya nyumbani wakati tunayo maziwa na mito mingi kuliko nchi yoyote Afrika, tena maji masafi na matamu ajabu lakini ndio ktk kufuru zetu tunatumia zaidi ya chupa kutoka ktk visima na maporomoko kama Ulaya ambao hawakubahatika kuwa na mazingira kama yetu. Taratibu mazao mengi hayawezi kuota bila mbolea kutoka Ulaya maana ardhi tayari imeshakuwa sugu.

Haya ktk Uvuvi tukaletewa Sangara samaki anayeharibu mazingira mbali kabisa na kuondoa exygen ziwa Victoria anakula na sakmaki wengine.. Ziwa hilo leo limebakia tupu. Ufugaji nako tunajifunza ule wa n'gombe wa kizungu ambao unatushinda lakini wapi hatuachi, tunawafuga n'gombe hawa wa Ulaya waliokuzwa kwa kula majaini makavu yaliyowekwa madawa kama n'gombe wetu Zebu na Ankole matokeo yake n'gombe hawa wamekuwa kama mazuzu barabarani na hutafuta kula majani usiku wa manane.

Halafu kitu kingine kikubwa ni Madini, tunayo lakini hatuna miners wala uwekezaji ktk kipaji hicho. Tupo radhi kuwatetea wafanyabiashara dhidi ya wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimba madini wakati hawa ndio wanaojenga asilimia 99 ya asili ya WATANZANIA. lakini leo hakuna Mtanzania anayependa hata kuitwa mkulima wote tunataka kuitwa wafanya biashara au wafanyakazi, waajiri na waajiriwa wa mashirika ya sayansi na teknologia kama unabisha tazama passport za watu utaona siku hizi kila mtu mfanyabiashara.

Haya wametuachia blueprint ya maendeleo yetu yanaweza vipi kuboreka kiuchumi kwa kutuwekea reli ya kati maana zamani Kigoma ilikuwa connection ya kibiashara baina ya Afrika mashariki na magharibi toka utumwa hadi mazao na madini lakini sisi ndio kwanza tumeiua reli hiyo na Kigoma leo ni mji wa magofu japokuwa kina Zitto wanajitahidi kurudisha umaarufu wake. Tazama Bagamoyo mji ulokuwa kitovu cha biashara zote za utumwa na Spices, connection baina ya bara na visiwani, Uajemi, Ulaya na Asia leo hata ktk Utalii hauna soko..Aaaah inatia uchungu sana naweza andika kitabu kizima -Tunashindwa na mengi mkuu wangu yaani basi tu!
 
Mzungu anakuja na , mwanasiasa anampa uwezo wa kufanya vyote. Mkenya anakuja anapewa kiwanda cha makaratasi anaweza kuendesha kwa kutumia mitambo hilehile mtanzania aliyoshindwa kuitumia. Mkiulizwa mnasema siasa ndio tatizo.
...Simple math, really. Aliyekichukua hata angekuwa Mkongomani kingefanya kazi na angekiendesha vizuri. Its all about private enterprise and profit maximization. Hawezi kwenda bank kukopa halafu akaja cheza sindimba za deni lake. H/she would make sure the loan deliver the intended goal. And above all, there are incentives in making sure the plant works according to the plan, for both the manager and the owner.

...Now, hakukuwa na faida kwa meneja wa kiwanda wakati huo [chini ya serikali] kufanya vizuri. And then, you had a govt. which didn't give a f@%*!, just because it was told so by the IMF/WB bunch of thugs. What do you expect?
 
Kwa mfano uchumi wa sasa wa Tanzania ni lazima utegemee kwa kiasi kikubwa unskilled labour. Hii ni kwa sababu watanzania wengi hawasoma vizuri au unskilled workers.
...Ndugu, hebu tusaidie ni namna gani hao unskilled labour watakuwa nguzo ya uchumi [kuwategemea kwa kiasi kikubwa] katika dunia ya leo, ambayo kwa bahati mbaya, haivumilii tena ujinga?

...Labda tuangalie ni value addition gani kwnye kilimo, madini, na hata utalii tutaweza kuifanya kwa kutumia unskilled labour. Dunia ya leo, mwenye kutaka faida na kuendelea lazima atumie teknologia kwa kiasi kikubwa, na kwa maana hiyo kuwapiga kikumbo wasio na elimu au ujuzi. Je, kwa kutumia hao watu tutaendelea?

...Unskilled labour will be our biggest problem in the near future, and i'm afraid there will be not much to do about it.
 
DSL,

Kwanza kutumia lebel unskilled labour ni makosa. Utafiti unaonyesha kuwa kila watu wana-skill za kumudu mazingira yao. Lakini kuendeleza mjadala tuendelee kulitumia.

Japokuwa waChina walikuwa na historia ya Ustaarabu, mapinduzi ya maendeleo yao sasa hayakuanza na skilled labour.

Je tunaweza kuiga mifano mizuri ya wachina hili kufanya watanzania wengi washiriki katika shughuli za maendeleo? Jibu ni ndio.

Mkoa wa Kilimanjaro hawakuanza kujenga shule kwanza na baadaye kulima kahawa. Walianza kulima kahawa na pesa zilipopatikana walipeleka watoto shule na kufanya diversification.

Je kuna mikoa yenye potential kwenye shughuli za kilimo? Ndio hipo. Na mikoa hii inaweza kuzalisha chakula kwa watanzania na kuuza nchi jirani.

Dunia sasa ina watu bilioni 7 na kuwalisha watu hawa ni biashara kubwa. Nchi kama Saudi Arabia inatafuta mashamba Africa hili wazalishe na kulisha kwao. Kwanini waAfrika, hususa watanzania hawafanyi juhudi katika kilimo?

Tanzania ina shule ya kilimo karibu kila wilaya. Ina vyuo vya kilimo karibu kila kanda. Na zaidi ya hapo ina chuo cha kikuu cha kilimo. Niambie ni skill gani inatakiwa zaidi?
 
...Simple math, really. Aliyekichukua hata angekuwa Mkongomani kingefanya kazi na angekiendesha vizuri. Its all about private enterprise and profit maximization. Hawezi kwenda bank kukopa halafu akaja cheza sindimba za deni lake. H/she would make sure the loan deliver the intended goal. And above all, there are incentives in making sure the plant works according to the plan, for both the manager and the owner.

...Now, hakukuwa na faida kwa meneja wa kiwanda wakati huo [chini ya serikali] kufanya vizuri. And then, you had a govt. which didn't give a f@%*!, just because it was told so by the IMF/WB bunch of thugs. What do you expect?

DSL,

Kama kila mtu angefanya vizuri, kwanini watanzania hawakupewa nafasi? Kwa hiyo hata Mengi au Mkandara hawakufaa kupewa nafasi ya kuendesha viwanda?

Nilipata bahati ya kuwa kwenye nchi za wakomunisti wa zamani. Watu waliuziwa viwanda kwa dollar moja hili ownership ibakie kwa wazawa na waendeleze ajira.
 
Mkuu wangu binafsi yangu nakubaliana na wewe sana tu ktk hili isipokuwa hilo la kuanzisha silicon valley kwa sababu umesha sema tayari sisi tuna hesabu kubwa ya unskilled workers hivyo wakati tunaelimisha wamnanchi wetu ni lazima tutazame mbali na elimu kuna kitu gani kingine ambacho wananchi wetu wamejaliwa nacho na ni chachu ya maendeleo. Na sababu nyingine kubwa sababu ambayo haiendani na biashara ni kutokana na kwamba sisi hatuna skilled workers lakini gharama ya utumishi wetu ni kubwa sana ukilinganisha na sehemu nyingine zozote duniani..
Hakuna Mtanzania anayeweza kufanya kazi kiwandani kwa kulipwa 30 cent per hour!akiondoka na Ths 3,000 kwa siku hivyo mwekezaji yeyote hawezi kuitazama Tanzania ikiwa kuna nchi kibao Asia zina maisha ya chini zaidi. Sisi tuna mishahara ya ajabu ajabu yaani waziri wetu au mbunge anapokea mshahara mkubwa kuliko Mbunge wa Canada kisha anapewa gari, mafuta na malupulupu kibao kwa visingizio vya kwamba mazingira yetu magumu kuliko Ulaya. Yaani huwezi kupima tunawezaje kuwa na serikali kubwa kiasi hiki wakati tunadai kwamba nchi yetu ni maskini.

Na kama ulivyosema hapo juu Suala la umaskini wetu sio sayansi au uhandisi au hisabati isipokuwa ni kama nisemavyo mimi linategemea WATU na MAZINGIRA waliyopo. Hakuna suhulu zaidi ya KILIMO, UVUVI NA UFUGAJI hivi ni vipaji WATANZANIA (watu) tulopewa na Mungu na kujikuta tukiishi ktk nchi yenye rasilimali hizi. Na kama unakumbuka niliwahi kusema kipoaji cha kilimo ndicho kilituponza sisi tukachukuliwa ktk Utumwa kwa sababu Wabantu ni wakulima kwa asili na pia kukoloniwa kumetokana na Afrika ni nchi yenye ardhi yenye rutuba ya kilimo na madini ambayo waliyahitaji makwao.

Lakini tazama tulipokabidhiwa Uhuru wetu, ndio kwanza kila mmoja wetu alitaka kurithi kile alichokiacha mzungu.. Majumba ya Oysterbay, Kawe na Masaki yakavamiwa na wazee wa Magomeni na Kariakoo. Nyerere mwenyewe alitaka kupinduliwa zaidi ya mara nne kwa sababu tu hakutaka kubadilisha vichwa vya watawala toka mzungu kuja Mkoloni mweusi. Na tukampinga sana isipokuwa yote aloyakanya yanajirudia leo hii, tumerudi kule tulikotoka kutaka kuwa kama Wazungu maana hakuna mfano bora wa binadamu na maisha kama ya mzungu na Ulaya.

Wenzetu hawakuzijenga nchi zao kwa kutazama model fulani bali mahitaji yao ndiyo yaliwasukuma kuboresha vipaji vyao ktk elimu ya sayansi na teknologia. Ile sababu ya kwamba KILA UGONJWA UNA DAWA na hakuna kitu kisichowezekana iliwapa ari ya kuvumbua vitu ambavyo viliweza kukidhi mahitaji yao na nchi zao kuendelea hatua kwa hatua.

Sisi ambao tumejaribu Kilimo kwanza -mtumeee, ndio kwanza tukampiga chini Mwandosya kwa sababu alikuwa hakubaliani na mpango wa GMO seeds ambazo ni biashara kubwa ya maabara za nje. Tukaingiza pembejeo za ajabu ajabu, mbolea inatolewa kwa voucher utadhani zaka za walfare ili mradi madeal tunagawana deal. Nchi inazidi kupata ukame kutokana na visima vya maji kuchimbwa kila kona kwa matumizi ya nyumbani wakati tunayo maziwa na mito mingi kuliko nchi yoyote Afrika, tena maji masafi na matamu ajabu lakini ndio ktk kufuru zetu tunatumia zaidi ya chupa kutoka ktk visima na maporomoko kama Ulaya ambao hawakubahatika kuwa na mazingira kama yetu. Taratibu mazao mengi hayawezi kuota bila mbolea kutoka Ulaya maana ardhi tayari imeshakuwa sugu.

Haya ktk Uvuvi tukaletewa Sangara samaki anayeharibu mazingira mbali kabisa na kuondoa exygen ziwa Victoria anakula na sakmaki wengine.. Ziwa hilo leo limebakia tupu. Ufugaji nako tunajifunza ule wa n'gombe wa kizungu ambao unatushinda lakini wapi hatuachi, tunawafuga n'gombe hawa wa Ulaya waliokuzwa kwa kula majaini makavu yaliyowekwa madawa kama n'gombe wetu Zebu na Ankole matokeo yake n'gombe hawa wamekuwa kama mazuzu barabarani na hutafuta kula majani usiku wa manane.

Halafu kitu kingine kikubwa ni Madini, tunayo lakini hatuna miners wala uwekezaji ktk kipaji hicho. Tupo radhi kuwatetea wafanyabiashara dhidi ya wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimba madini wakati hawa ndio wanaojenga asilimia 99 ya asili ya WATANZANIA. lakini leo hakuna Mtanzania anayependa hata kuitwa mkulima wote tunataka kuitwa wafanya biashara au wafanyakazi, waajiri na waajiriwa wa mashirika ya sayansi na teknologia kama unabisha tazama passport za watu utaona siku hizi kila mtu mfanyabiashara.

Haya wametuachia blueprint ya maendeleo yetu yanaweza vipi kuboreka kiuchumi kwa kutuwekea reli ya kati maana zamani Kigoma ilikuwa connection ya kibiashara baina ya Afrika mashariki na magharibi toka utumwa hadi mazao na madini lakini sisi ndio kwanza tumeiua reli hiyo na Kigoma leo ni mji wa magofu japokuwa kina Zitto wanajitahidi kurudisha umaarufu wake. Tazama Bagamoyo mji ulokuwa kitovu cha biashara zote za utumwa na Spices, connection baina ya bara na visiwani, Uajemi, Ulaya na Asia leo hata ktk Utalii hauna soko..Aaaah inatia uchungu sana naweza andika kitabu kizima -Tunashindwa na mengi mkuu wangu yaani basi tu!

Mkandara,

Kuhusu Silicon Valley niliuliza tu swali. Hii ni kwa sababu miaka ya nyuma kila mtu ninayemfahamu alitaka kufungua internet cafe. Ni wachache nawasikia kuanzisha uzalishaji ambao hauitaji skill kubwa na zenye faida kama kilimo.
 
Tatizo lipo kwenye Ardhi. Watu wengi ikiwa ni pamoja na mimi tumeporwa mashamba ili kujenga kupisha ujenzi wa blaa blaa blaa!..wananchi na hasa maskini hawana haki na ardhi zao hivyo, kwa kuogopa kuporwa wengi wanaziuza kabla hawajanyang'anywa.
 
Je kuna mikoa yenye potential kwenye shughuli za kilimo? Ndio hipo. Na mikoa hii inaweza kuzalisha chakula kwa watanzania na kuuza nchi jirani.
...Wakizalisha, wanavuna, wanaweka kwenye junia, wanapakia kwenye magari, wakifika njiani mnawatoza kodi kila mahala. Halafu baadae, mnawaambia hawawezi kuuza nje, ati kuna upungufu sijui inflation, wtf?

...Unafikiri kwa mazingira hayo hiyo mikoa itazalisha na kufikia uwezo wake halisi? Hakuna manufaa!
Dunia sasa ina watu bilioni 7 na kuwalisha watu hawa ni biashara kubwa. Nchi kama Saudi Arabia inatafuta mashamba Africa hili wazalishe na kulisha kwao. Kwanini waAfrika, hususa watanzania hawafanyi juhudi katika kilimo?
...Wakulima hawa maskini, wanaotegemea mvua, halafu mnawakataza kuuzia mabichi wenzao na kusafirisha makavu kwenda malawi, zambia, kongo na kenya? Hivi, nani alisema mahindi makavu ndio chakula pekee? Tunakula ya kuchoma na glasi ya juisi ya miwa, tunaenda lala, siku imepita.
Tanzania ina shule ya kilimo karibu kila wilaya. Ina vyuo vya kilimo karibu kila kanda. Na zaidi ya hapo ina chuo cha kikuu cha kilimo. Niambie ni skill gani inatakiwa zaidi?
...Hizo shule zina walimu siku hizi? Huduma za ugani ziko wapi?
 
Kama kila mtu angefanya vizuri, kwanini watanzania hawakupewa nafasi? Kwa hiyo hata Mengi au Mkandara hawakufaa kupewa nafasi ya kuendesha viwanda?
...Muulize Mengi alijibiwa nini. Nadhani ana ufahamu mzuri wa hili.
Nilipata bahati ya kuwa kwenye nchi za wakomunisti wa zamani. Watu waliuziwa viwanda kwa dollar moja hili ownership ibakie kwa wazawa na waendeleze ajira.
...Huku its otherwise, unfortunately.
 
Tatizo lipo kwenye Ardhi. Watu wengi ikiwa ni pamoja na mimi tumeporwa mashamba ili kujenga kupisha ujenzi wa blaa blaa blaa!..wananchi na hasa maskini hawana haki na ardhi zao hivyo, kwa kuogopa kuporwa wengi wanaziuza kabla hawajanyang'anywa.
...100%. The American Dream was 1st built on land ownership!

...When it comes to kilimo, land has to be capitalized.
 
Tumezungumza mengi sana kuhusu umaskini wa Mtanzania na nadhani kwa mapana yake tumekubali kwamba nchi yetu ni tajiri kati ya nchi matajiri duniani lakini tumeshindwa kabisa kutumia nafasi, mtaji na vipaji vyetu kuweza kuutumia utajiri huo kwa faida ya wananchi au hata Taifa lenyewe.

Sasa kinachofuata ni - TULIKOSEA WAPI? ni wakati gani tumefanya maamuzi ambayo yanaendeleza hali hii iliyopo maana kama tutarekebisha hicho ama hivyo kutajenga tumaini jipya kama tulivyokuwa wakati tunaingia Ubepari mwaka 1985 na nakumbuka vizuri sana furaha tulizokuwa nazo. Leo tumepoteza kila kitu ni mateka wa kifikra na Utaifa, hatuna uzalendo wala tumaini tena kibaya zaidi hadi roho za watu zimejenga chuki na unafiki kiasi kwamba tumerudi nyuma hadi kifikra na imani za uchawi zimeshehena vichwani mwa kila mtu - WHAT'S WRONG?
 
Back
Top Bottom