Mkandara,
Kwa mtanzania yoyote mwenye kuipenda nchi yake, suala la kwanini Tanzania ni masikini lipo vichwani kwa miaka mingi. Na suala zima sio sayansi au uhandisi au hisabati.
Kwa mfano uchumi wa sasa wa Tanzania ni lazima utegemee kwa kiasi kikubwa unskilled labour. Hii ni kwa sababu watanzania wengi hawasoma vizuri au unskilled workers. Swali je ni uchumi gani utawafaa watanzania wakati wana-build capabilities zao? Je kuanzisha silicon Valley inawezekana?
Mkuu wangu binafsi yangu nakubaliana na wewe sana tu ktk hili isipokuwa hilo la kuanzisha silicon valley kwa sababu umesha sema tayari sisi tuna hesabu kubwa ya unskilled workers hivyo wakati tunaelimisha wamnanchi wetu ni lazima tutazame mbali na elimu kuna kitu gani kingine ambacho wananchi wetu wamejaliwa nacho na ni chachu ya maendeleo. Na sababu nyingine kubwa sababu ambayo haiendani na biashara ni kutokana na kwamba sisi hatuna skilled workers lakini gharama ya utumishi wetu ni kubwa sana ukilinganisha na sehemu nyingine zozote duniani..
Hakuna Mtanzania anayeweza kufanya kazi kiwandani kwa kulipwa 30 cent per hour!akiondoka na Ths 3,000 kwa siku hivyo mwekezaji yeyote hawezi kuitazama Tanzania ikiwa kuna nchi kibao Asia zina maisha ya chini zaidi. Sisi tuna mishahara ya ajabu ajabu yaani waziri wetu au mbunge anapokea mshahara mkubwa kuliko Mbunge wa Canada kisha anapewa gari, mafuta na malupulupu kibao kwa visingizio vya kwamba mazingira yetu magumu kuliko Ulaya. Yaani huwezi kupima tunawezaje kuwa na serikali kubwa kiasi hiki wakati tunadai kwamba nchi yetu ni maskini.
Na kama ulivyosema hapo juu Suala la umaskini wetu sio sayansi au uhandisi au hisabati isipokuwa ni kama nisemavyo mimi linategemea WATU na MAZINGIRA waliyopo. Hakuna suhulu zaidi ya KILIMO, UVUVI NA UFUGAJI hivi ni vipaji WATANZANIA (watu) tulopewa na Mungu na kujikuta tukiishi ktk nchi yenye rasilimali hizi. Na kama unakumbuka niliwahi kusema kipoaji cha kilimo ndicho kilituponza sisi tukachukuliwa ktk Utumwa kwa sababu Wabantu ni wakulima kwa asili na pia kukoloniwa kumetokana na Afrika ni nchi yenye ardhi yenye rutuba ya kilimo na madini ambayo waliyahitaji makwao.
Lakini tazama tulipokabidhiwa Uhuru wetu, ndio kwanza kila mmoja wetu alitaka kurithi kile alichokiacha mzungu.. Majumba ya Oysterbay, Kawe na Masaki yakavamiwa na wazee wa Magomeni na Kariakoo. Nyerere mwenyewe alitaka kupinduliwa zaidi ya mara nne kwa sababu tu hakutaka kubadilisha vichwa vya watawala toka mzungu kuja Mkoloni mweusi. Na tukampinga sana isipokuwa yote aloyakanya yanajirudia leo hii, tumerudi kule tulikotoka kutaka kuwa kama Wazungu maana hakuna mfano bora wa binadamu na maisha kama ya mzungu na Ulaya.
Wenzetu hawakuzijenga nchi zao kwa kutazama model fulani bali mahitaji yao ndiyo yaliwasukuma kuboresha vipaji vyao ktk elimu ya sayansi na teknologia. Ile sababu ya kwamba KILA UGONJWA UNA DAWA na hakuna kitu kisichowezekana iliwapa ari ya kuvumbua vitu ambavyo viliweza kukidhi mahitaji yao na nchi zao kuendelea hatua kwa hatua.
Sisi ambao tumejaribu Kilimo kwanza -mtumeee, ndio kwanza tukampiga chini Mwandosya kwa sababu alikuwa hakubaliani na mpango wa GMO seeds ambazo ni biashara kubwa ya maabara za nje. Tukaingiza pembejeo za ajabu ajabu, mbolea inatolewa kwa voucher utadhani zaka za walfare ili mradi madeal tunagawana deal. Nchi inazidi kupata ukame kutokana na visima vya maji kuchimbwa kila kona kwa matumizi ya nyumbani wakati tunayo maziwa na mito mingi kuliko nchi yoyote Afrika, tena maji masafi na matamu ajabu lakini ndio ktk kufuru zetu tunatumia zaidi ya chupa kutoka ktk visima na maporomoko kama Ulaya ambao hawakubahatika kuwa na mazingira kama yetu. Taratibu mazao mengi hayawezi kuota bila mbolea kutoka Ulaya maana ardhi tayari imeshakuwa sugu.
Haya ktk Uvuvi tukaletewa Sangara samaki anayeharibu mazingira mbali kabisa na kuondoa exygen ziwa Victoria anakula na sakmaki wengine.. Ziwa hilo leo limebakia tupu. Ufugaji nako tunajifunza ule wa n'gombe wa kizungu ambao unatushinda lakini wapi hatuachi, tunawafuga n'gombe hawa wa Ulaya waliokuzwa kwa kula majaini makavu yaliyowekwa madawa kama n'gombe wetu Zebu na Ankole matokeo yake n'gombe hawa wamekuwa kama mazuzu barabarani na hutafuta kula majani usiku wa manane.
Halafu kitu kingine kikubwa ni Madini, tunayo lakini hatuna miners wala uwekezaji ktk kipaji hicho. Tupo radhi kuwatetea wafanyabiashara dhidi ya wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimba madini wakati hawa ndio wanaojenga asilimia 99 ya asili ya WATANZANIA. lakini leo hakuna Mtanzania anayependa hata kuitwa mkulima wote tunataka kuitwa wafanya biashara au wafanyakazi, waajiri na waajiriwa wa mashirika ya sayansi na teknologia kama unabisha tazama passport za watu utaona siku hizi kila mtu mfanyabiashara.
Haya wametuachia blueprint ya maendeleo yetu yanaweza vipi kuboreka kiuchumi kwa kutuwekea reli ya kati maana zamani Kigoma ilikuwa connection ya kibiashara baina ya Afrika mashariki na magharibi toka utumwa hadi mazao na madini lakini sisi ndio kwanza tumeiua reli hiyo na Kigoma leo ni mji wa magofu japokuwa kina Zitto wanajitahidi kurudisha umaarufu wake. Tazama Bagamoyo mji ulokuwa kitovu cha biashara zote za utumwa na Spices, connection baina ya bara na visiwani, Uajemi, Ulaya na Asia leo hata ktk Utalii hauna soko..Aaaah inatia uchungu sana naweza andika kitabu kizima -Tunashindwa na mengi mkuu wangu yaani basi tu!