Kwanini watu wa kamera wanaruhusiwa kuhujumu ziara ya Rais Samia?

Huyo jamaa aliyeimba mwanzo anaitwa nani?bado yupo hai?kama unamjua jina nitajie.Anaonekana alikuwa mhamasishaji mzuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye kaona anahujumiwa ili hali sisi tunapomuuliza maswali mustakabali wa kero zetu anatuuelekeza tukawaambie wa chini yake, kwani sisi hatujawaona hao wa chini yake? Kwaiyo kaona lake halijawekwa sawa ndio anaropoka.Vip kuhusu matatizo yetu? Tunapomueleza afu anayatupa kapuni ww kwa ubongo wako ni sawa?Mbona Magufuli alikua anayatatua hapo kwa papo kama linahusiana na mahakama anampa mtu wa mahakama aliangalie kwa haki.
 
Iko hivi, huo umati zaidi ya 70% wanahudhuria kwa vitisho na shuruti,na hao wapiga picha wanajua ni umati wa mchongo. Kwanini wapige picha za kuhadaa umma kwa umati wa kulazimisha?
 
CCM na watendaji wa serikali wanaotayarisha ziara waende wakajifunze kwa makada wa chama cha MPR ya Mobutu waliobakia, jinsi ya kutukuza, kusifu pamoja na kufanya nchi isimame wote wakifuatilia matamasha ya chama tawala

 

Hata angetaza hizo ziara kila chombo cha habari hapa duniani, bado watu wameichoka CCM. Magufuli ndio alikuwa bingwa wa media, lakini ndio kiongozi aliyenajisi uchaguzi kuliko kiongozi yoyote yule. CCM haitegemei kura kukaa madarakani, huo ugumu wa kampeni unatoka wapi?
 
Mh Rais mama Samia Alipokelewa kwa shangwe Sana huku mkoani Mbeya Tangia aliposimama katika mji wa Mbalizi, kwa kuwa wananchi wanamkubali Sana na wanamuunga mkono

Kwa hela anazohonga na watu kusombwa kwa malori atakosaje watu? Hilo neno kumkubali sana liondoe. Hakuna mtu anakubali majizi ya kura.
 
Kwani huko kampeni zimeanza mpaka mtu kutaka kuwe na nyomi?
 
Hapo wanamuombea aishi milele 🤣
 
Chuki mchukieni HAKI YAKE MPENI!
Hakika Hali yake ya kumpongeza na kumtia moyo Tunampatia mh RAIS wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa afanyazo kututumikia wananchi wake, sisi vijana tunaendelea kumuunga mkono Rais wetu

Tunasema mama aendelee kuchapa kazi bila kuchoka Wala kukatishwa Tamaa na mtu yoyote yule, Tulio bega kwa bega na Rais Ni wengi kuliko wachachee wasiofurahia kazi nzuri afanyazo,maana walitegemea waone akishindwa lakini kwa mshangao wao wanashangaa namna anavyo endelea vizuri na kupata uungwaji mkono mkubwa toka kwa wananchi
 
Ngoja kwanza nipige nduru!
 
Huyo jamaa aliyeimba mwanzo anaitwa nani?bado yupo hai?kama unamjua jina nitajie.Anaonekana alikuwa mhamasishaji mzuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Ngoja tupite mitaa ya Château Rouge jijini Paris France au ikishindikana baadaye nifike Matonge Brussels Belgie lazima tutapa historia kamili ya huyu John Komba wa MPR ya Mobutu.
Diaspora ya Jamaa zetu hawa wa DR Congo wanamkubali sana Mobutu na vitu vyake alivyofanya ktk siasa za Congo.
 
Rais Samia Suluhu amedai kwamba, Waandishi wa habari wanaandika kwamba kwenye ziara yake inayofanyika Nyanda za Juu Kusini watu wanaohudhuria ni wachache.

Jambo analoliona kama ni Upotoshaji , Kwake yeye anaamini Umati ni mkubwa wa kutisha, amewaomba waandishi waandike uhalisia, huku akiwataka Wapiga picha wapande juu ili wapige vizuri picha za umati unaohudhuria mikutano yake.

Kwa kadri ya kumbukumbu zangu hili ni jambo Jipya tangu niifahamu Tanzania , sijawahi kusikia Rais wa Tanzania akilalamikia kuhusu taarifa za ziara zake kupotoshwa na wanahabari na wapiga picha.

Hivi Ikulu haina Wapiga picha ambao wanaweza kunogesha.

Ziara ya Rais hata kwa Propaganda za uongo , kama enzi za akina Michuzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…