Nimemsikia mwenyewe LIVE, wakati Rais anatoa hotuba leo huko Arusha katika kikao Cha watendaji wakuu wa Taasisi za Umma, akikiri kuwa katika miaka Ile ya mwanzoni wa miaka ya 80, wakati alipokuewa Waziri wa kawaida, aliwasikia baadhi ya wakuu wa mashirika ya Umma, namna wanavyojimwambafai, Kwa kutamka kwenye kikao Chao Cha "Siri" kuwa ni lazima Kila Mkuu wa Taasisi ya Umma, ale kutokana na urefu wa kama yake!
Amedai kuwa yupo Mkuu wa shirika Moja la Umma, aliyedai kuwa Kila mwisho wa wiki, alikuwa "akiiba" kutoka Kwenye shirika Hilo siyo chini ya shilingi milioni 2 Kwa madhumini tu ya kutumbua, Kwa ajili ya weekend!😭
Hivi kama Kila Mkuu wa Taasisi ya Umma, ndivyo afanyavyo, ina maana kuwa haya mashirika ya Umma, wanayaua hao viongozi wa Taasisi hizo Kwa makusudi kabisa!
Hii nchi hakuna jambo lngine litakaloweza kuikombia hii nchi, zaidi ya kukiondoa madarakani Kwa chama hiki Cha CCM, Kwa njia ya kupiga kura Kwenye box la kura mwakani, Kwenye uchaguzi Mkuu, ambao tunawatupa nje hawa viwazi Jeshi wa Mali ya Umma
Mungu ibariki Tanzania