Kweli nimeamini, ukimfadhili mwanamke usitegemee kwamba atakuja kukusaidia wakati wowote

Kosa la mdada ni kutokujibu ujumbe wako ila kukusaidia au la ni uamuzi wake. Huwezi jua hela zake anazifanyia nini japo umeshampangia kuwa hana majukumu.
 
Kinachouma ni kusoma meseji alafu akakaa kimya.
angemjibu tu pale pale
 
Kosa la mdada ni kutokujibu ujumbe wako ila kukusaidia au la ni uamuzi wake. Huwezi jua hela zake anazifanyia nini japo umeshampangia kuwa hana majukumu.
Yeah, angalau angejibu mapema. Hamna aliyempangia matumizi.
 
Duh, hapa basi wanawake ni wa tofauti sana.
 
Pengine kwa watu wengine ni kiasi kikubwa ila kwangu sioni kama ni kikubwa. Huyu ni mtu tunawasiliana mara nyingi kwahiyo ujumbe ni hakika aliuona. Aliamua tu kupotezea.

Mambo gani ya msingi sikufanya?
 
Hamkomagi kusomesha mwanamke ni shimo lataka akilizao zinawawezesha kuvuka mistari mweupe ya barabarani tu
 
Naunga mkono hoja,
 
Ukitaka kumsaidia mtu msaidie tu usihtaji malipo baadae. Binadamu ndio walivyo. Me kuna demu nilimtafutia kazi na tupo poa tu na sikutaka kuomba mchezo nilimsaidia kama wanadamu wengine. That is all
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…