LATRA waruhusu Mabasi kuanza safari saa 9 Usiku

LATRA waruhusu Mabasi kuanza safari saa 9 Usiku

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Nadhani ni suala la muda tu, maana kuna mambo hayaepukiki kwenye dunia hii inayokwenda kwa kasi ajabu.

Ilianza saa 12 mara saa 11, sasa ni saa 9 kutoka popote pale ndani ya Tanzania kuelekea mikoa mingine ili mradi ukidhi vigezo hasa kigezo cha LATRA kukuruhusu.

Mamlaka ya usafiri ya udhibiti wa usafiri ardhini nchini imewaagiza wamiliki wa mabasi wanaopenda kuanza safari muda huo wa saa tisa usiku wafike katika Ofisi zao kuomba upya leseni.

Salum Pazzy anayekaimu kitengo cha uhusiano na mawasiliano cha LATRA amesema, ni lazima madereva wasajiliwe ili kuwa na taarifa zao za msingi.

Kwa maoni yangu, angalau kidogo mnasogea japo bado sana maana tunapaswa kusafiri 24hrs katika dunia inayopungua ukubwa kila siku, ikiwa watu hawalali kwa sasa wakikimbia huko na huko.

==============
IN UPDATES:
Hatimaye serikali imeruhusu mabasi kusafiri masaa 24.
Waziri Mkuu Dododma.jpg
 
Wazo zuri. Lakini Sasa madereva wetu hawa mmh!
Labda kuwe na ufuatiliaji katika kila kituo. Wawe wanapimwa Kama hawajapiga kamnyweso.
 
Masaa 24 kwa madereva wepi? Ni hawa hawaa wa mabasi wanaotanua hovyo hovyo na kutowajali watumiaji wengine wa barabara? Trust me ajali zitakazofuatia hapo ….zitakuwa za kutisha sanaa!
HAPANA.

Utakuwa hujaelewa au hujui issue ya 24hrs, but ipo hivi mkuu.

Mfano unatoka Sumbawanga alasiri as saa 9 unakuja kulala let say Iringa, hapo iringa unafika saa 7 usiku na badala ya kulala hapo dereva mwenzako anakusubiri hapo wewe unabaki yeye anapeleka chombo.

Ukiachia hilo hata hivi sasa mabasi karibia yote yatokayo Bukoba, Songea kuja Dar au Dar to Musoma nk yote badala ya kulala njiani yanatoboa, lini umesikia ajali ya bus la usiku mnene?.

Although hofu na uoga wako unatokana na kutosafiri nadhani, napenda kurudia hii hapa, chuma za hapo kwa Ruto asilimia kubwa zinatembea usiku.

Kuna chombo hii hapa 👉🏾Aliyeamua kuchukua hii Route ya Johannesburg to Dar Es Salaam ni Mtanzania Kweli? usidhani Itakuwa inatembea mchana tu hadi kufika kwa babu madiba mkuu.
 
Speed SIO chanzo pekee cha ajali nyingi hapa Tanzania, tatizo kubwa barabara zetu bado sana,Dar to Arusha ni kama 650km,huu ni mwendo wa saa nane kwa bus na mapumziko juu, nashauri tutengeneze hizi barabara kwa kiwango kinachokubaliwa na tuziwekee road tolls ili watumiaji wachangie gharama za uboreshaji wa barabara zetu, mabus yaruhusiwe 24hrs yatembee barabarani au majambazi wametuzidi kete?
 
HAPANA.

Utakuwa hujaelewa au hujui issue ya 24hrs, but ipo hivi mkuu.

Mfano unatoka Sumbawanga alasiri as saa 9 unakuja kulala let say Iringa, hapo iringa unafika saa 7 usiku na badala ya kulala hapo dereva mwenzako anakusubiri hapo wewe unabaki yeye anapeleka chombo.

Ukiachia hilo hata hivi sasa mabasi karibia yote yatokayo Bukoba, Songea kuja Dar au Dar to Musoma nk yote badala ya kulala njiani yanatoboa, lini umesikia ajali ya bus la usiku mnene?.

Although hofu na uoga wako unatokana na kutosafiri nadhani, napenda kurudia hii hapa, chuma za hapo kwa Ruto asilimia kubwa zinatembea usiku.

Kuna chombo hii hapa 👉🏾Aliyeamua kuchukua hii Route ya Johannesburg to Dar Es Salaam ni Mtanzania Kweli? usidhani Itakuwa inatembea mchana tu hadi kufika kwa babu madiba mkuu.
Mkuu chombo hicho kikiingia zambia tu,ni kutambaa usiku na kikifika Harare kinakutana na wababe wa Harare to jhb, nani kutusua beitbridge mapema?akina intercape waanze kujipanga
 
Kabla ya kufikia kuruhusu hayo kwanza waboreshe miundombinu ya barabara...... barabara mbovu zinachangia asilimia kubwa za ajali za barabarani.........wasifanye maamuzi ya kisiasa na kutuangamiza sie tusiokuwa na hatia.....maana wao wanasafiri na vieiti na ving'ora sisi tunapelekwa kama ng'ombe......
 
HAPANA.

Utakuwa hujaelewa au hujui issue ya 24hrs, but ipo hivi mkuu.

Mfano unatoka Sumbawanga alasiri as saa 9 unakuja kulala let say Iringa, hapo iringa unafika saa 7 usiku na badala ya kulala hapo dereva mwenzako anakusubiri hapo wewe unabaki yeye anapeleka chombo.

Ukiachia hilo hata hivi sasa mabasi karibia yote yatokayo Bukoba, Songea kuja Dar au Dar to Musoma nk yote badala ya kulala njiani yanatoboa, lini umesikia ajali ya bus la usiku mnene?.

Although hofu na uoga wako unatokana na kutosafiri nadhani, napenda kurudia hii hapa, chuma za hapo kwa Ruto asilimia kubwa zinatembea usiku.

Kuna chombo hii hapa [emoji1485]Aliyeamua kuchukua hii Route ya Johannesburg to Dar Es Salaam ni Mtanzania Kweli? usidhani Itakuwa inatembea mchana tu hadi kufika kwa babu madiba mkuu.
Watu wengi wana uoga wa kufikirika.

Makampuni yana uwezo wa kufanikisha hili, labda shida ije kuwa na upungufu wa abiria kinyume na hapo ni jambo linalowezekana.
 
Ninayo furaha kuwajulisha kuwa zile kelele zetu zimefanikiwa kwa asilimia kubwa na hivyo mabasi yataanza safari saa tisa usiku kwa kuomba kibali.

Ni hatua kubwa na nzuri maybe very soon tutasafiri 24hrs, tuachane Sasa na habari za Speed meter a.k.a Ving'amuzi.

Pia andiko langu lingine hili

Taarifa hii hapa

IMG-20230504-WA0047.jpg
 
Back
Top Bottom