LATRA yapiga Stop usafirishaji kwa kutumia magari madogo kuepuka ajali za kila siku

Hata kama mbadala haujapatikana, maamuzi aliyochua Kafulila ni sahihi ili kuokoa maisha ya wananchi.
Hapa umeonyesha akili huna
Kama mbadala haupo.Wajawazito na wagonjwa mahututi mfano wataendaje hospitali zilizo mbali si unatengeneza vifo vya mama na mtoto na wagonjwa mahututi majumbani
 
Kwa hiyo LATRA wamezidiwa akili na mkuu wa Mkoa moja tu kwa akili. Wenyewe wamekaa tu pfisini hawana ubunifu wowote. Siyo ifunjwe litaasisi ambalo halina kazi? Noah ziondolewe barabarani, huwezi kusafirisha abiria kM 150 kutumia Noah na abiria wamebanana, line ya abiria watatu wao wanalazimisha wanne hata huwezi kupumua vizuri. Nauli yao kubwa kishenzi, kwa mfano Arusha-Karatu KM140 nauli sh. 8,000/
 
Na ukisoma habari huoni kama sababu ya ajali ni ukaaji mbaya wa dereva au mbanano wa abiria. Uso kwa uso ni ajali inayotokea baada ya bad overtaking, sasa hiyo bad overtake haitokani na aina ya gari, ni maamuzi yasiyo sahihi ya dereva. Kuzuia madereva hawa wasiendeshe michomoko hakuwafunzi kuwa madereva bora, watahamia kwenye mabasi na watafanya overtaking za muundo huohuo, napo sijui mtayazuia mabasi!!

Ingekuwa michomoko inapinduka kutokana na kuzidiwa uzito au haina balance angalau katazo lingekuwa na mashiko.

Hili suala la kusema abiria wanakufa wengi inapotokea ajali hata kwenye mabasi hutokea hivyo, na sababu kubwa mara nyingi huwa ni mwendokasi na dereva kushindwa kulimudu gari, bado huoni mahali ambapo gari ni tatizo bali madereva.

RC Kafulila, rejea uamuzi wako, hapo utatesa wananchi na kuchelewesha ukuaji uchumi mkoani kwako. Wape elimu madereva na usimamizi uwe imara.
 
Noah ziondolewe barabarani, huwezi kusafirisha abiria kM 150 kutumia Noah na abiria wamebanana, line ya abiria watatu wao wanalazimisha wanne hata huwezi kupumua vizuri. Nauli yao kubwa kishenzi, kwa mfano Arusha-Karatu KM140 nauli sh. 8,000/
Hiyo inaitwa shida ya usafiri eneo husika
Kama usafiri uko vizuri nani atakubali kupanda kwa kubanana ma kilomita yote hayo na nauli ikiwa kubwa hivyo na akiwa Kakaa mkao wa kushindwa hadi kupumua ?

Hapo shida ni kubwa hivyo wakati Noah bado zipo ! Sasa ukiamka kama mkuu wa mkoa na kutaka kuanzia sasa hivi ukasema marufuku kuanzia sasa hivi Noah kuweko watu watapanda punda? Mbadala uko wapi?
 
RC Kafulila, rejea uamuzi wako, hapo utatesa wananchi na kuchelewesha ukuaji uchumi mkoani kwako. Wape elimu madereva na usimamizi uwe imara.
Uchumi wa vituo vya mafuta Simiyu lazima pia ushuke hao michomoko ndio wajaza mafuta wao vituoni
 
Mfano nilioutoa magari ni mengi tena sana. Arusha-Karatu kuna mabasi makubwa, kuna Coaster, kuna Hiace. Yapo mpaka mabasi ya kwenda Dar Es Salaam moja kwa moja.
 
Huwa Hawa Latra hawajitambui, wanasubiri maafa ndio wanajitokeza na Matamko!! Fikiria hapa Dar Bajaji ambayo ni hatarishi sana WA usalama na uendeshwaji usiozingatia sheria za barabarani, pia waendeshaji kutokuwa na hata leseni ya kuendesha guta, achilia mbali abiria wapo wanadunda!! Na full fujo!! Route stand Magufuli to Manzese no leseni
 
Mfano nilioutoa magari ni mengi tena sana. Arusha-Karatu kuna mabasi makubwa, kuna Coaster, kuna Hiace. Yapo mpaka mabasi ya kwenda Dar Es Salaam moja kwa moja.
Lakini hayakidhi mahitaji ndio maana watu wanabanana kwenye Noah kilomita nyingi kwa nauli kubwa

Yaliyopo yangekuwa yakidhi mahitaji halisia ya abiria wasingejazana hivyo kwenye Noah
 
Unatetea Sana, Pole kwa uwekezaji
Kafulila na Latra ni economic hitmen
Wameamua kutumia nafasi zao ku hit economy na business chain za michomoko nchi nzima kwa kisingizio cha ajali za michomoko miwili Simiyu

Maamuzi yao ni ya kupiga Rungu uchumi kitaifa na mzunguko wa pesa kitaifa uliokuwa ukichochewa na michomoko.

Kifupi Latra na Kafulila ni wahujumu uchumi kupitia maamuzi yao
 
Unafurahi watu kufa kila siku?
 
Unatetea Sana, Pole kwa uwekezaji
Wawekezaji wakiondoka mnaanza kubweka ohhh tutangaze mkoa wetu tuvutie wawekezaji wakija mnaleta vituko na maamuzi ya ajabu ajabu ya kuumiza wawekezaji. Halafu mnaanza kuhangaisha mama Samia akatafute wawekezaji nje watakaoongeza ajira .Huku mnaua uwekezaji wa watu wa ndani waliotoa kuwekeza vituo vya mafuta ,michomoko nk na kutoa ajira zinazoongeza mzunguko wa pesa na kuchangamsha uchumi maeneo yenu na kuongeza Mapato ya kodi kwenye huo mzunguko unaosaidia hata mishahara ya wafanyakazi wa Serikali kupanda
 
Kabla ya ajali alikuwa hayaoni hayo magari?
Kosa liko kwa magari au madereva na askari wa usalama barabarani?
 
Pole Sana YEHODAYA kwa kuwekeza kwenye ' mchomoko ' ili kuua watu
Kazi ya michomoko ni Kuua watu? Akili wewe hazimo gombea jimbo ndio utawajua michomoko ni akina nani

Kafulila ana mpango wa kugombea ubunge 2025 mwambieni anasubiriwa kwa hamu atawajua michomoko ni akina nani.Abiria wapenda michomoko na wamiliki watampa jibu lake hata akiteuliwa na Chama .

Hii issue sio ndogo .Kama Kafulila anavyodhani.Maamuzi yake na Latra yanachafua Serikali ,na Chama na Mama Samia nchi nzima
 
Acha ujinga wako,

Chama kinataka watu wafe?

Rais anataka watu wafe?
 
Tatizo hiyo michomoko ni ya hao hao, halafu hiyo mingi ina marejesho sijui itakuwaje
 
Acha ujinga wako,

Chama kinataka watu wafe?

Rais anataka watu wafe?
Nchi nzima michomoko iligongana hadi marufuku itolewe nchi nzima,? Hata Simiyu tu haikuwa sahihi kupiga marufuku mkoa mzima.Kila mtu anatakiwa kubeba mzigo wake .Huwezi bebesha zigo la michomoko miwili ukabebesha michomoko mkoa wote au nchi yote

Chama cha CCM na Serikali kazi kwenu .Huku sio kutenda haki

Waziri mkuu na Mama Samia ingilieni kati ni uonezi .Halafu watu wanaropoka tu wakati mbadala haujaandaliwa .Majaliwa tengua hiyo Amri hadi mbadala upatikane

Raisi ukiona Waziri Mkuu yuko kimya tengua wewe na uwatengue wote wakaa kimya wakikusubiri wewe

Ina maana kazi yao nini sasa kama hawakusaidii vitu vitu vidogo kama hiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…