LATRA yaruhusu Mabasi ya Dar - Mtwara yapite Barabara ya Songea, Makambako, Iringa kwa dharura

LATRA yaruhusu Mabasi ya Dar - Mtwara yapite Barabara ya Songea, Makambako, Iringa kwa dharura

Hapo ndio namkumbuka bw Mwaibula, alianzisha kupiga mistari ya rangi tofauti, na maandishi ya Kila ruti ya daladala,

Hawa watoto wa juzi hawajui hilo. Pia hawajui kwamba pale Ubungo interchange palikuwa panaitwa ubungo mataa. Hatafu kulikuwa na kituo cha daladala pale karibu na ofisi za Tanroads za mkoa wa Dar. Halafu opposite kulikuwa na kituo cha ubungo maji. Hawajui hatua tulizopitia.
 
1. Kwani utaratibu ndiyo upi ndugu?

2. Kumbe soko huria maana yake nini?

3. Au market forces nayo nini?

4. Prof. Shivji ana hoja tuacheni kumezeshwa bila kutafuna:

Shivji: Chimbuko la wasiokuwa na Hoja au uthubutu wa Kuhoji, linalo ligharimu Taifa (Part 1)

5. Hapo #4, kwa mwendo uliopo tutamezeshwa hadi matango pori!

Ukienda kokote duniani, hakuna biashara inayofanyika bila kuwa regulated. Biashara huria, haimaanishi watu kufanya mambo bila kufuata utaratibu. Vinginevyo itakuwa fujo sasa.
 
Ukienda kokote duniani, hakuna biashara inayofanyika bila kuwa regulated. Biashara huria, haimaanishi watu kufanya mambo bila kufuata utaratibu. Vinginevyo itakuwa fujo sasa.

1. Ukienda kwenye dunia iliyostaarabika biashara ni huria na huendelea ikizingatiwa nguvu za soko.

2. Ilipokuja corona ndege zA abiria zilibeba mizigo maisha yakasonga.

3. Hapo #2 jaribu kubeba mizigo kwenye bus uwaone wanaojua biashara ya mabasi pasipokuwa na mabasi.

5. Ziangalie mamlaka za serikali wapi zimefanikiwa na biashara ipi?

6. Hapo #5, ni atcl, TRC, tanesco, ttcl, TPA, TMA, mwendokasi, Uda, kamata, kauru, kauma, moretco, co-cabs...?

7. Wacheni biashara za watu kama mmayaweza si muanzishe yenu tuone na kujifunza?!
 
MOJA YA MIKOA AMBAYO NAHISI SIO TANZANIA BASI NI MTWARA KWA NAMNA ULIVYO NA MIUNDO MBINU MIBOVU.!!! KUNA VIDARAJA UCHWARA SANA.! NJIA YA HOVYO HOVYO KABISA KUWAI KUTOKEA

KWA HIYO NJIA BORA UPANDE NDEGE TU

Wananchi waelezea ujenzi wa madaraja mapya usiozingatia mazingira, wakumbuka madaraja ya 'mkoloni' ujenzi wake ulizingatia mambo mengi badala ya mtindo wa mainjinia na wakandarasi wa sasa kujaribu kupasua milima kutafuta level / tambarare kitu kinachopelekea madaraja na barabara mpya kukumbwa na mafuriko ...


February 2024

MAJI YAFURIKA TUNDURU DARAJA YA MTO MUHUWESI


View: https://m.youtube.com/watch?v=BKuBc7enwJI

Daraja la mto Muhuwesi Tunduru ni daraja muhimu sana kitaifa na kima taifa maana linapitisha bidhaa mbali mbaliza kimataifa..mvua kubwa zinazonyesha ukanda wa Morogoro na Selous, daraja la Mto Muhuwesi lililopo wilaya ya Tunduru hukumbwa na mafuriko

... Kwa niaba ya Madereva wa Magari yaliokwama kutokana na kadhia hiyo, Ndg. Fabian Ignas Mnyenyelwa Dereva wa magari makubwa ya kusafirisha Makaa ya Mawe, amesema kadhia hiyo inawaathiri kwani wametumia muda Mrefu katika eneo hilo ambalo halina huduma za kijamii, pia ameiomba serikali kufanyia marekebisho Daraja hilo , ikiwezekana kwa kuliinua zaidi ya kina kilichopo kwa sasa....

Hali hii imeathiri usafiri kuelekea Mtwara, Dar es Salaam, Lindi na Pwani Na kutoka katika mikoa hiyo kuelekea Tunduru, Namtumbo, Songea Njombe, Iringa na Mbeya...

N.B
Habari za ziada kina na za ndani kabisa :


MAJI daraja la Muhuwesi yajaa DC atahadharisha​

thumb_5139_800x420_0_0_auto.jpeg
Imewekwa Kuanzia Tarehe: February 13th, 2024

Daraja kubwa la Mto Muhuwesi lililopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma limejaa maji hadi juu na kutishia usalama wa watu na mali.

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Mheshimiwa Julius Mtatiro amesema kujaa kwa katika mto Muhuwesi kumetokana mvua kubwa zinazonyesha ukanda wa Morogoro na Selous.

“Kwa hiyo tumechukua uamuzi wa haraka wa kufunga barabara kuu ya Mangaka - Tunduru Mjini kwa muda. Eneo la barabara linalofungwa ni eneo la mto lililo kati ya kata za Muhuwesi na Majimaji”,amesema Mtatiro.

Amebainisha kuwa Magari yanayotokea Mbeya, Iringa, Songea na Mkoa wote wa Ruvuma kuelekea Mkoa wa Lindi, Mtwara, Pwani na Dar yatakapofika Tunduru Mjini yapaki na kupumzika kusubiri hali iwe sawa kwenye Mto Muhuwesi.

Amesema magari yanayotokea mikoa ya Lindi , Mtwara, Pwani na Dar Es Salaam kwenda Tunduru, yanashauriwa kusimama na kupaki Nakapanya, Namiungo au Majimaji.
1714993839471.png

Ametahadharisha kuwa madereva wasilazimishe kuvuka katika daraja hilo kwa sababu wanaweza kuleta madhara kwa watu na mali.
Source : tovuti ya mkoa ruvuma.go.tz na wilaya tundurudc.go.tz
 
Wazo la hovyo. Jeshi lisaidie. Lilete na kivuko chao na boti zao ziferry watu maeneo korofi.
 
05 May 2024

TANROADS RUVUMA YAFANYA UKARABATI MKUBWA MIUNDOMBINU KATIKA DARAJA LA MUHUWESI WILAYANI TUNDURU

1714995798014.png

Na Mwandishi Maalum Ruvuma

WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Ruvuma, imekamilisha kazi ya kuimarisha daraja la mto Muhuwesi wilayani Tunduru ambalo liliathirika na mvua za masika na kusababisha taaruki kwa watumiaji wa daraja hilo.

View: https://m.youtube.com/watch?v=FEgteyhTaMQ
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Saleh Juma alisema, kwa sasa daraja hilo ni salama na haliwezi kusogea tena kama ilivyotokea hapo awali, na amewatoa hofu watumiaji hasa wenye magari kuhusu uimara wa daraja hilo linalounganisha mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara.
1714996620512.png

Aidha alitaja kazi nyingine zilizofanyika, ni kuziba mashimo makubwa kwenye barabara inayoingia katika daraja hilo yaliyosababishwa na maji ya mvua kupita chini ya barabara na kukatika kwa sehemu ya lami.
1714994776891.png

Alisema, katika eneo hilo barabara imemeza maji na kusababisha ifumuke,lakini tayari TANROADS kwa kumtumia Mkandarasi Kampuni ya Ovans Constructions Ltd imefanikiwa kuziba mashimo yaliyojitokeza.
1714994973405.png

“katika eneo hili magari yanayopita yalikuwa yanakwama na kusababisha adha kubwa, lakini tayari serikali kupitia wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) imefanya matengengezo ya haraka na sasa hali ni shwari” alisema.

Kwa upande wake Mhandisi wa kampuni ya Ovans Constructions Ltd Azimio Mwapongo alisema, katika eneo hilo kulitokea changamoto ya maji kutokea chini kuja juu ya barabara na kusababisha lami kukatika.

Kwa mujibu wa Mwapongo,kazi zilizofanyika ni ulazaji wa mabomba chini ya ardhi kwa ajili ya kunyonya maji kutoka chini na kuyapeleka nje ili yasikae tena pamoja na kurudishia tabaka la lami.
1714994859310.png

Alisema,kwa sasa daraja na sehemu ya barabara hiyo usalama wake ni mkubwa na kazi iliyoendelea ni ujenzi wa mifereji ya kupitisha maji ambayo nayo iliathiri na mvua.

Mkazi wa kijiji cha Muhuwesi wilayani Tunduru Salum Gambagamba, ameipongeza serikali kupitia TANRAODS kwa kufanya matengenezo ya haraka katika daraja la mto huo na maeneo ya barabara yaliyoanza kuharibika na mvua.
Mhandisi wa kampuni ya Ovans Construtions Ltd Azimio Mwapongo kulia, akitoa taarifa ya ukarabati wa miundombinu ya daraja la mto Muhuwesi linalounganisha mkoa wa Ruvuma na mikoa ya kusini Lindi na Mtwara kwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Saleh Juma aliyetembea daraja hilo ili kujionea kazi ya kurejesha baadhi ya miundombinu yake,kushoto msimamizi wa kitengo cha matengenezo TANROADS Godfery Robbi.
Meneja wa TANROADS Mkoani Ruvuma Mhandisi Saleh Juma kushoto,akitoa maelekezo kwa mhandisi wa Kampuni ya Ovans Construtions Ltd Bw. Azimio Mwapongo wa pili kulia baada ya kukagua matengenezo ya kipande cha Barabara ya Songea-Mangaka eneo la Muhuwesi wilayani Tunduru kilichoharibiwa na mvua za masika,wa pili kushoto msimamizi wa kitengo cha matengenezo Tanroads Godfre Robbi na kulia mkuu wa kitengo cha mipango Tanroads Rubara Marando.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Saleh Juma, akiangalia sehemu ya mifereji ya kupitisha maji katika barabara ya Songea-Mangaka eneo la daraja la Mto Muhuwesi wilayani Tunduru ambayo imeharibika vibaya kutokana na mvua za masika akiwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya barabara hiyo jana.

Source : michuzi blog / michuzi.co.tz

2022 15 February

Historia ya mafuriko na uharibifu kwa daraja la mto Muhuwesi wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiwa ameongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa na Wilaya ya Tunduru wamekagua Daraja la Muhuwesi ambalo limeharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha



View: https://m.youtube.com/watch?v=kZmf5PZ_0hc
 
TOKA MAKTABA:


Daraja jipya la Muhuwesi lenye uzito wa zaidi ya tani 1,000 lilivyosukumwa na kuhamishwa na nguvu ya mto Muhuwesi


View: https://m.youtube.com/watch?v=QKPSCVAeD04

Serikali yatoa zaidi ya Bilioni 1 kufanya Marekebisho Daraja la Muhuwesi Tunduru likosegezwa na nguvu ya maji ya mto Muhuwesi mnamo mwezi February 2022 lina urefu wa mita 40 na kusifika kuwa mojawapo ya madaraja imara hadi hapo 2022 lilopopata changamoto ni njia muhimu kuunganisha mikoa ya Lindi Mtwara, Ruvuma, Njombe kuelekea Iringa hadi mikoa ya Pwani na Dar es Salaam

2016 DARAJA LA ZAMANI KATIKA MTO MUHUWESI TUNDURU

1715039068461.png
 
Ruti ndefu ni Dar to Tarime hatari hiyo
Ruti ndefu ni Dar kwenda Karagwe
Na mwanaume anaeenda ni mmoja tu kampuni ya City boys
 

Attachments

  • Screenshot_20240506_214858_Firefox.jpg
    Screenshot_20240506_214858_Firefox.jpg
    722.9 KB · Views: 1
  • Screenshot_20240506_214648_Firefox.jpg
    Screenshot_20240506_214648_Firefox.jpg
    707.8 KB · Views: 2
Waruhusu wapite njia ya masasi, liwale hadi ifakara/mahenge japo sio rasmi lakini ni fupi kuliko huo mzunguko na kupunguza gharama ya nauli kwa abiria
Ifakara, Malinyi na Mahenge nako barabara zake ni majanga makubwa miaka yote hasa kipindi cha Masika.
 
Hiyo route hadi tako za wasafiri zitaota lengelenge!
 
07 May 2024

ILI UREJESHAJI WA MAWASILIANO BARABARA YA DAR - LINDI UTIMIE NDANI YA SAA 72, KAZI NAENDELEA USIKU NA MCHANA



View: https://m.youtube.com/watch?v=edmnSghwvyk
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akikagua kazi ya urejeshaji mawasiliano ya barabara ya Lindi – Dar es Salaam ambayo inaendelea kufanyika usiku na mchana ili kuhakikisha huduma za usafiri na na usafirijishaji zinarejea ifikapo siku ya Alhamisi.

Waziri Bashungwa akiwa amesalia katika Mkoa wa Lindi ili kusimamia timu ya wataalamu wa Wakala ya Barabara (TANROADS) na makandarasi huku akisisitiza kuwa kazi itafanyika usiku na mchana ili kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ndani ya saa 72 alizoeleza awali
 
07 May 2024

ILI UREJESHAJI WA MAWASILIANO BARABARA YA DAR - LINDI UTIMIE NDANI YA SAA 72, KAZI NAENDELEA USIKU NA MCHANA



View: https://m.youtube.com/watch?v=edmnSghwvyk
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa akikagua kazi ya urejeshaji mawasiliano ya barabara ya Lindi – Dar es Salaam ambayo inaendelea kufanyika usiku na mchana ili kuhakikisha huduma za usafiri na na usafirijishaji zinarejea ifikapo siku ya Alhamisi.

Waziri Bashungwa akiwa amesalia katika Mkoa wa Lindi ili kusimamia timu ya wataalamu wa Wakala ya Barabara (TANROADS) na makandarasi huku akisisitiza kuwa kazi itafanyika usiku na mchana ili kuhakikisha zoezi hilo linakamilika ndani ya saa 72 alizoeleza awali


08 May 2024

HALI ILIVYO SOMANGA BARABARA YA LINDI - DAR ES SALAAM


View: https://m.youtube.com/watch?v=XrM7YkL8xHU
 
Back
Top Bottom