LATRA yatangaza ongezeko la nauli za Safari za Masafa Marefu na Mafupi kuanzia Desemba 8, 2023

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza mabadiliko ya nauli katika safari za masafa marefu na masafa mafupi baada ya kupitia maoni ya wadau wa usafiri nchini.

Kwa mujibu wa LATRA nauli za safari zisizozidi kilometa 10 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 500 sasa itakuwa 600. Kwa safari za kilometa 11 hadi 15 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 550 sasa itakuwa shilingi 700.

Kwa kilometa 15 hadi 20 ambapo nauli ilikuwa shilingi 600 sasa itakuwa 800 huku kwa safari za kilometa 21 hadi 25 nauli imetoka 700 hadi shilingi 900. Safari ya kilometa 26 hadi 30 nauli ni shilingi 1100, safari ya kilometa 31 hadi 35 ni shilingi 1300 na kilometa 36 hadi 40 nauli ni 1400.

Aidha nauli za wanafunzi zitaendelea kusalia 200 kwa safari za masafa mafupi.

Nauli za mabasi zimeorodheshwa kwenye jedwali hapa chini.

F_8N0PNXIAASRZx.jpeg
F_8N0zFXgAABlEP.jpeg
F_8N1c0WUAEApTt.jpeg
F_8N2EiXYAAOr8e.jpeg
 
Mama kashapandisha nauli mara mbili ndani ya miaka 2, chuma kilikaa na nauli miaka yote aliyokuwa madarakani.. Sekta ya usafirishaji huwa inaleta mfumuko mkubwa sana wa bei
Magu hakujua chochote kuhusu biashara,mafuta yapande,na mafuta ndiyo yanaendesha gari,halafu nauli isipande!?..Ila je,mafuta yamepanda Tena!?
 
Back
Top Bottom