LATRA yatangaza ongezeko la nauli za Safari za Masafa Marefu na Mafupi kuanzia Desemba 8, 2023
Hali ni tete, hali ni mbaya, gharama za maisha lazima zipande..

Wao wanakula keki ya taifa tu, itafika hatua wote tutazungumza lugha moja hakuna cha ccm wala chadema, wale ambao watakaa kimya ni wale tu ambao wanafaidika na taifa hili.
 
Bila shaka na ya Bagamoyo imeongezwa imekuwa 2000, basi utashangaa na Nauli ya Msata inapanda tena wakati hiyo ya 5000 tu sijui iliwekwaje wekwaje, daah sema hivi vichenchi chenchi vya 50, 100, 200 huwa sivipendi kukaa navyo basi tu
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza mabadiliko ya nauli katika safari za masafa marefu na masafa mafupi baada ya kupitia maoni ya wadau wa usafiri nchini.

Kwa mujibu wa LATRA nauli za safari zisizozidi kilometa 10 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 500 sasa itakuwa 600. Kwa safari za kilometa 11 hadi 15 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 550 sasa itakuwa shilingi 700.

Kwa kilometa 15 hadi 20 ambapo nauli ilikuwa shilingi 600 sasa itakuwa 800 huku kwa safari za kilometa 21 hadi 25 nauli imetoka 700 hadi shilingi 900. Safari ya kilometa 26 hadi 30 nauli ni shilingi 1100, safari ya kilometa 31 hadi 35 ni shilingi 1300 na kilometa 36 hadi 40 nauli ni 1400.

Aidha nauli za wanafunzi zitaendelea kusalia 200 kwa safari za masafa mafupi.

Nauli za mabasi zimeorodheshwa kwenye jedwali hapa chini.

View attachment 2826735View attachment 2826734View attachment 2826733View attachment 2826732
Kipato hakiongezeki, ila gharama kila nyanja zinapanda. Ati uchumi unakua! Na kuna mbobezi (kwenye makaratasi)wa masuala ya uchumi!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Serikali nayo iache upuuzi bhana.. hivi treni ya mwendokasi imeishia wapi?. Nauli imepandishwa mwaka jana mwezi aprili, leo tena nauli mnapandisha
. Hivi mnajua athari zake kiuchumi kweli?. Mama Samia usicheke na wafanyabiashara watakuharibia. Namkumbuka sana Magufuli kwa kweli.
 
Back
Top Bottom