LATRA yatangaza ongezeko la nauli za Safari za Masafa Marefu na Mafupi kuanzia Desemba 8, 2023
Kupanda kwa nauli ya daladala kunahusika vp na vitu?
Broo vitu vingine havihitaji utumie akili kubwa sana hata mtoto wa nursery atakushangaa........nikupe mfano mtu anachukua samaki ferry anawaleta mbezi akipandishiwa naul nae lazima kidogo abandishe samaki bei ili apate faida, the some Kwa bidhaa nyingine, Kwa mikoani ndyo usiseme.

Acha kukaza fuvu.
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza mabadiliko ya nauli katika safari za masafa marefu na masafa mafupi baada ya kupitia maoni ya wadau wa usafiri nchini.

Kwa mujibu wa LATRA nauli za safari zisizozidi kilometa 10 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 500 sasa itakuwa 600. Kwa safari za kilometa 11 hadi 15 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 550 sasa itakuwa shilingi 700.

Kwa kilometa 15 hadi 20 ambapo nauli ilikuwa shilingi 600 sasa itakuwa 800 huku kwa safari za kilometa 21 hadi 25 nauli imetoka 700 hadi shilingi 900. Safari ya kilometa 26 hadi 30 nauli ni shilingi 1100, safari ya kilometa 31 hadi 35 ni shilingi 1300 na kilometa 36 hadi 40 nauli ni 1400.

Aidha nauli za wanafunzi zitaendelea kusalia 200 kwa safari za masafa mafupi.

Nauli za mabasi zimeorodheshwa kwenye jedwali hapa chini.

View attachment 2826735View attachment 2826734View attachment 2826733View attachment 2826732
Samia hana social intelligence kuna siku wananchi watazingua na hamna Jeshi wala wapinzani walionunuliwa watamsaidia.
 
Mama kashapandisha nauli mara mbili ndani ya miaka 2 ya utawala wake, chuma kilikaa na nauli miaka yote aliyokuwa madarakani.. Sekta ya usafirishaji huwa inaleta mfumuko mkubwa sana wa bei kwenye uchumi.
Mkuu unachokiongea na ninachokisoma kwenye mabango ya Mama mbona vitu viwili tofauti...au nipo nchi gani mimi??
 
Na sheria inasema wafanye review ya nauli mpya kila baada ya miaka mitano toka kuanza kutumika kwa nauli za awali. Sasa sijui kimetokea nini tena huko LATRA.
Mkuu ile mibasi ya mchina ni ya mkopo ujue kwa hiyo kusubili hiyo miaka mitano ni jehanamu ujue.
 
daah kuelekea uchaguzi Serikali za mitaa ndio haya mambo yanaibuka! Kama vile Muvi za kumkwamisha Mama naona
It's reality bro! Vitu vinaenda ni sayansi, mafuta, yamepanda, Kodi kibao, lazima, nauli Zita panda tu, ni logic ndogo Sana, kwenye kila Lita ya mafuta, asilimia kubwa ni tozo na Kodi, serikali ipunguze matumizi, ya sio, ya, lazima, semina, walsha,safari za, nje, punguza ukubwa wa serikali, futa baadhi ya wizara, unganisha mikoa, punguza ukubwa wa bunge na ma Jimbo yabaki 100!
Hakuna kununua magari, v8, ikibidi kununua, tutumie land cruiser hardtop, zile ndogo(cruiser 2).
 
Mama kashapandisha nauli mara mbili ndani ya miaka 2 ya utawala wake, chuma kilikaa na nauli miaka yote aliyokuwa madarakani.. Sekta ya usafirishaji huwa inaleta mfumuko mkubwa sana wa bei kwenye uchumi.
Chuma lazima kikumbukwe
 
Dodoma to Singida kupitia manyoni nauli 62,000/? Nchi haipo serious
Huo mkeka wa nauli haujakaa sawa.
Kwa mfano; nauli ya Dodoma Kigoma inaonekana kuwa ndogo kuliko nauli ya Dodoma Tabora wakati Kigoma ni mbali kuliko Tabora.
 
Tutakuwa hatusafiri sasa[emoji1787][emoji1787]
Samia kaza hapo hapo.
Tena ikibidi uongeze ili ikifika mwaka 2025 Panapo uhai.
TUKUCHAGUE TENA UWE RAISI

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Sasa wamewapa watoto wa intern waandae hizi data ama?
Umbali Dar to Dodoma na nauli ni elfu 5?
Singida Dodoma nauli ni 72,000 eti na umbali ni 1,268 KM?
Au aliyeandaa jedwali alilewa?
Majedwali hayajakaa sawa. Angalia pia Dodoma Iringa nauli 67,000/= how comes??
 
Nauli mlizozipandisha jana kuna makosa makubwa ya umbali wa maeneo mbali mbali kulikosababisha kufanya nauli kuwa kubwa.

Mfano umbali wa kutika Dodoma kwenda Moshi kupitia Babati mmeweka umbali ni kms 1090 badala ya kms 502.
 
Hahaha aliyeandaa alifanya copy and paste. Hakukuwa na umuhimu wowote wa kupandisha nauli mwisho wa mwaka.
 
Nauli mlizozipandisha jana kuna makosa makubwa ya umbali wa maeneo mbali mbali kulikosababisha kufanya nauli kuwa kubwa.

Mfano umbali wa kutika dodoma kwenda moshi kupitia babati mmeweka umbali ni kms 1090 badala ya kms 502.

Inategemea unapita wapi, tatizo lako unalazimisha iwe Kondoa.
 
Back
Top Bottom