Hakuna mwenye akili timamu wakumkumbuka muuaji wa uhai na uhuru wa kujieleza na democracy
 
JPM ni kama maji, hutaki kuyaoga hutasita kuyanywa,
Hatuna desturi ya kuheshimu mda lakin mda hautasita kutumbusha
 
Bigbrotherrugambwa YOU NAILED IT .

Hakika legacy ya JPM haifutiki imechorwa kwa kalamu ya moto wabaya wake wangetafuta vitu vingine vya kufanya.

Magufuli anabaki kuwa ni Rais bora aliewahi kutokea Tanzania na kumpata mwingine ni baada ya miaka 50.
Dikteta muuaji,Nani wakumkumbuka ,alidhulumu haki za watu za kuishi pamoja na Bashite
 
Nakubaliana na wewe kwamba ni bonge la UZI but pale alipozungumzia issues za CAG nadhani kakosea, mwendazake hakua anaamini sana kwenye transparency; we all knows what happened kwa profesa Asadi. Tatizo la watu wengi hua ni hii, wanapenda kujadiri mabaya ya mtu fulani as if hakuwahi kufanya mazuri na wengine hupenda kujadiri mazuri tu ya mtu fulani bila kutaja mabaya yake, hapo ndio tunapotofautiana kibinadamu, mfano watu ambao walikua against na mwendazake ukiwatajia mazuri yake watakuita wewe ni SUKUMA Gang na ukiamua kueleza mabaya yake, unaonekana wewe ni mpinzani yaani Chadema, ni ujinga na upuuzi uliopitiliza. Nilimsikiliza mwenyekiti wa Chadema kwenye hotuba yake, alianza kueleza mazuri ya Magufuli then akaeleza mabaya yake. Hivi angekuwepo mwana ccm aliyefungiwa account zake zote (including account yake ya mshahara ) angeweza kutaja zuri hata moja la Magufuli? Tumemsikia hadi mwenyekiti wa ccm Mwanza, kaenda mbali zaidi wakati hakufungiwa account zake wala, kunyimwa tu matangazo ya biashara kwa TV yake karopoka vile, what if angefanyiwa nusu ya alichofanyiwa Mbowe?
 
Unajua maana ya legacy vizuri? Legacy siyo SGR, INTERCHANGE, STIGULA, ELIMU BURE na BARABARA. Hivyo hata HITLER na IDD AMIN walijenga.
 
Salaam!

JPM alikuwa ni rais dhaifu kuliko marais wote waliowahi kutumika Tanzania kwa vigezo vifuatavyo:

1. Alikuwa ni mwoga sana - hii ni kutokana na kutokujiamini kiuongozi

2. Alikuwa mtu wa visasi - issue ya Yusuf Manji ni mfano wa mingi iliyokuwapo

3. Alikuwa anapenda misifa - at the expense of professionalism. Look at what the likes of Kabudi have turned out to be!

4. Alikuwa ni mbinafsi - sihitaji kurudia kwani sote tunajua yale mambo yake ya Chato

5. Kupenda sifa (rejea # 3) kuliruhusu wapambe kujineemesha - Kakoko, Bashite, Sabaya, nk

6. Alikuwa ni mjinga katika mambo mengi lakini hakurusu watu wamsaidie

7. Uadilifu wake ulikuwa wa mashaka - alihakikisha vyombo huru vyote anavidhibiti (bunge, judiciary, media, CAG). Alimshindwa CAG akafanya njama za kumwondoa kinyemela. Matokeo yake ni matumizi mengi kufanyika kiholela na bila kukaguliwa. No checks & balances!

8. Kutoka na woga wake (rejea # 1), alihakikisha wapinzani wake ndani na nje ya CCM wanadhibitiwa kwa namna YOYOTE. Hapa tuna:
  • Lissu (story sote twaijua)
  • viongozi wa upinzani wengine kama Mbowe (kesi za kubumba, nk) na Maalim Seif (kuivunjilia mbali CUF). Ninaamini hadi mauti yake, moja ya majuto yake makubwa ni kushindwa kuivunja Chadema pamoja na mbinu zote chafu zilizotumika
  • ndani ya CCM kuna JK, Kinana, Makamba (Jr & Sr), Nape, Membe, nk

9. Kutokusema ukweli - mifano ipo mingi. Ndiyo maana Rais Samia ana struggle sana sasa hivi kwani amekumbana na REALITY.

10. Usahaulifu katika masuala mengi ya msingi - kiashiria kidogo ni kutamka (tena mara mbili mbili) kuwa eti siku ina masaa 48!

Hayo 10 hapo juu - kwa uchache - ndiyo MAGUFULI's LEGACY kama mimi ningeulizwa. Si ya kujivunia hata kidogo.

Madaraja, mabarabara, viwanda, nk hata wakoloni walijenga - hii siyo legacy bali ni wajibu wa serekali yoyote iliyo madarakani. In fact Mwalimu JKN (rip babu yetu) was the best performer kwenye masuala ya infrastructure and industrial upheaval nchini.

Wakatabahu!
 
yaani kuteseka na kulalama mpaka mishipa ya shingo inakusimama hakutaisha leo wala kesho... magu bado ana mengi mazuri ambayo yatakuchoma na kukucharanga wewe mpaka vitukuu vyako na hamtaweza kushinda kamwe... endelea tu kuteseka mzee
Mazuri hatatetewi wala hayachomi.
Mazuri hujitetea.
 
Sifa Apewe MUNGU kutuondolea Huyo Mtu
 
Mazuri hatatetewi wala hayachomi.
Mazuri hujitetea.
kwani nani anayatetea mazuri yake? yapo tu na wala hayaitaji mtetezi hata kwa miaka 100 ijayo ila isipokuwa nyie mnaomtwika matakataka yenu ya kuokoteza huko mnapiga kelele weee mpaka vichwa vinawauma na hakuna anayewasikiliza... hicho ndicho kinachowauma ninyi, maana mnajitahidi kufurukuta lakini waapi?

kila mtu abaki na msimamo wake afu uone nani anayeteseka zaidi kati yangu na nyie? mi muda wote ni kufurahia mazuri ya mzee magu huku nikipata raha ya moyo kuona jinsi mnavofurukuta kuwapigia mbuzi magitaa mpaka mnaumia kuona hawachezi
 
Nimeishia hapo no 1! Tu nikaacha kusoma
 
...
Sihitaji kurudia mazuri ya Magufuli. Tunajua alikuwa Rais wa watu aliyeongoza kwa ajili ya watu wa chini kabisa. Wazalendo wa Nchi hii hatuwezi kubabaishwa na kelele za wachache waliomchukia kwa sababu tunazozijua.
...

Kuhusu "legacy" ya Magufuli, ukweli ni kwamba yaliyofanyika chini ya utawala wake ni yale yaliyokuwa yameidhinishwa na Chama chake (CCM) kama yalivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi 2015 na kuboreshwa kwenye Ilani ya Uchaguzi 2020.

Anakumbukwa na Watanzania kwa sababu ya matokeo mazuri ya utekelezaji wa hiyo Ilani ya Uchaguzi. Hilo liliwezekana kwa sababu alisimamia utekelezaji wake bila kupepesa macho, kwa uthubutu, uzalendo na utashi wa kisiasa.

Kama ulivyodadavua, wanaojaribu kufuta hiyo "legacy" ni kundi la Watanzania waliofadika na uongozi mbovu na Sera/Sheria za hovyo. Katika kundi hili wamo Viongozi wa kisiasa wa chama chake (CCM) na vyama vya upinzani, Wafanya biashara wakwepa kodi, Viongozi wa Serikali na Taasisi zake, Mafisadi, na Watanzania wa "mission town".

Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mama SSH ni wateule wake Magufuli. Kwa kujua na kuthamini uwezo na utendaji wa mtangulizi wake, Rais mama SSH amefanya mabadiliko machache sana kwenye Serikali, Taasisi zake na hata Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Na hata Wabunge wa CCM wengi wao wamepata kura na kuingia mjengoni kwa sababu ya utendaji wake Magufuli.

Nakubaliana na wewe kwamba Siasa Uchwara haziwezi kufuta "Legacy" ya Magufuli hata kama zikiongozwa na kigogo yupi kwa uwazi au kwa uficho. Kadiri wanavyojitahidi kufuta "legacy" yake, wanazidi kujichimbia kaburi la kuzikwa kisiasa. Uchaguzi Mkuu 2025 ndio utakuwa kipimo cha hao Wanasiasa (Chama Tawala au Upinzani).
 
Ongeza Volume 📣📣📣📣📣 hawajasikia bado
 
Magufuli Kesha kufa na account yake imefungwa let him rest in peace
Usitumie jina lake kuendesha siasa zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…