Legacy ya Magufuli Haiwezi Kufutika kwa Siasa Uchwara
Legacy kubwa ya Magufuli aliyoaiacha na itakumbukwa kwa vizazi vingi ni kuwa Rais wa nchi akiwa ni mgonjwa wa akili.
Hiii ni legacy ya pekee sana maana vichaa wengi huishia barabarani lakini yeye kaishia ikulu,what a legacy!
Kuna mwingine ana legacy ya kushikishwa ukuta huko ubeberuni, nayo ni legacy tu
 
The man.
FB_IMG_1626497608524.jpg
 
kwani nani anayatetea mazuri yake? yapo tu na wala hayaitaji mtetezi hata kwa miaka 100 ijayo ila isipokuwa nyie mnaomtwika matakataka yenu ya kuokoteza huko mnapiga kelele weee mpaka vichwa vinawauma na hakuna anayewasikiliza... hicho ndicho kinachowauma ninyi, maana mnajitahidi kufurukuta lakini waapi?

kila mtu abaki na msimamo wake afu uone nani anayeteseka zaidi kati yangu na nyie? mi muda wote ni kufurahia mazuri ya mzee magu huku nikipata raha ya moyo kuona jinsi mnavofurukuta kuwapigia mbuzi magitaa mpaka mnaumia kuona hawachezi
Pole kwa kuteseka.
 
Ni kweli na bahati mbaya mnafiki anaweza kumgeuka yeyote
Kumwamini mnafiki ni kujichimbia shimo then ukajifukia mwenyewe; ni ukichaa usio na viwango. Wagonjwa wa aina hiyo, hata Mirembe hawapokelewagiNi
 
Point hapa ni kuwa viongozi wanaotaka kumkosoa wafanye hivyo moja kwa moja na sio kwa uficho
 
Unadhani kuna mtu kashika "duster" anaifuta? Kama ipo ngangari na ya kupendeza, itadumu. Kama ni kinyume chake, utashangaa ukitaka kumsimulia mtu anakupiga kofi au akikuhurumia anakucheka.Manta hofu mkuu!Do not,ever, force a button!🤣🤣🤣🤣
Legacy imeajiandika. Wenye donge tu ndio wanahangaika sio Mimi.
 
Haya ni maoni yangu na mtu yeyote halazimishwi kuyapokea.

Sihitaji kurudia mazuri ya Magufuli. Tunajua alikuwa Rais wa watu aliyeongoza kwa ajili ya watu wa chini kabisa.
Sasa wale wa Juu walikuwa hawana kiongozi na wale wa kati maana ali deal na watu wa chiiiiiiiini kaaabiisa.


Basi alikuwa hafai. Wote tumepiga kura
 
Dhalimu legacy yake ni UDHALIMU NA DHULUMA. Tia hiyo akilini mwako.



Haya ni maoni yangu na mtu yeyote halazimishwi kuyapokea.

Sihitaji kurudia mazuri ya Magufuli. Tunajua alikuwa Rais wa watu aliyeongoza kwa ajili ya watu wa chini kabisa. Wazalendo wa Nchi hii hatuwezi kubabaishwa na kelele za wachache waliomchukia kwa sababu tunazozijua (e.g. u-puppet, kutumbuliwa, u-chadema, n.k). Na zaidi ya yote tunajua pia alitutoa kwenye “utumwa wa wanasiasa na viongozi wa serikali walafi na wauza nchi wasio na chembe ya kuwatumikia wananchi bali matumbo yao”. Kwa hiyo siasa Uchwara haziwezi kufuta Legacy ya Magufuri hata kama zikiongozwa na kigogo yupi kwa uwazi au kwa uficho.

Mbali na wananchi wachache waliomchukia kwa sababu za kisiasa au za binafsi, ndani ya CCM na serikali kumekuwa na majaribio yasiyofanikiwa ya Kumchafua “Hayati”. Nitaongelea Machache.

Report ya CAG – Iliwafanya watu wajulize wizi wa namna hii ulitokeaje chini ya Magufuli. Kinachoshangaza ni style ya kutoa hiyo report ilikuwa tofauti sana na siku za nyuma? Kabla Rais hajaiongelea na Bunge halijaijadili CAG “alipewa ruhusa ya kuichambua kwa kina kabisa” kitu ambacho sio kawaida uhuru huo kutokea. Bila shaka vigogo fulani kwa maslahi ya kisiasa walitaka kuonyesha JPM hakuwa such a great leader. Lakini ukweli unabaki kuwa report zote za nyuma JPM akiwa madarakani zilikuwa na mududu. Tofauti na sasa watu waliofanya madudu hayo walitumbuliwa immediately. Swali la msingi waliotaka JPM aonekane hafai walikuwa akina nani? Labda muhimu zaidi wasaidizi wa JPM (makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri wa Fedha, Waziri wa TAMISEMI – aliyelaumwa sana wakati anaaapishwa na Magufuli, n.k) walikuwa wapi? Report hii haikufanikiwa kumchafua Magufuli bali wasaidizi wake kwa vile uongozi wa Magufuli dhidi ya Inneficiency na Corruption haukuwa na shaka.

Kelele za Bungeni – Baadhi ya makada na mawaziri wa zamani wa CCM waliotumbuliwa na JPM walijaribu kuchukua nafasi ya kifo cha JPM kuponda style yake ya uongozi na kujaribu kufuta legacy yake. Hakuna anayeweza kushangazwa nao kwa kutompenda Magufuli! Ni hulka ya mwanadamu kumchukia adui yako. Lakini swali muhimu hapa ni kuwa wapendwa hawa wa viongozi wa awamu zilizopita walitumwa na nani? Kwa nini wawe Cowards – kwa kutokuwa na ujasiri wa kupinga hayo yote wakati JPM akiwa hai? Inafurahisha kuwa bidii hizi hazikufika popote baada ya wabunge wenzao kuwapuuza na kufanya azimio la kupongeza legacy ya JPM.

Antony Dialo – Kama alivyosema Msukuma huyu “alitoa ushuzi chumbani na akajaribu kuuondoa kwa feni” kitu ambacho hakufanikiwa. Wote tunajua Diallo hakumpenda Magufuli kwa vile yeye na ‘matajiri wengi ndani ya CCM walipoteza influence kwa vile upiga deal uliisha Hata hivyo maneno yake makali sana tena yanayotolewa na kiongozi wa CCM wa Mkoa aliyekuwa chini ya uenyekiti wa JPM yanashangaza kiasi fulani? Sote tunajua wote walioteuliwa au/na kufanya kazi na JPM either “ALIWAAMINI” au “ALIWAPENDA”. Hakuwahi kuwa mnafiki. Diallo kuibuka leo na ‘literally’ kumtukana JPM ni ishara ya wazi “alitumwa”. Tunajua wote, huwezi kumsema kiongozi mstaafu au aliyetangulia (e.g. Nyerere au JMK) na wewe ni kiongozi wa chama ukabaki salama (ukaendelea na kazi za chama as if nothing happened). Sidhani kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM amekuwa so democratic kiasi cha kupuuzia mambo kama haya? Hata hivyo wananchi na wana CCM wa ngazi za chini wamekemea upuuzi huu na kukumbushia mazuri ya JPM. Jaribio hili pia limeshindwa.

Kauli ya Mtaka – Kauli hii inaonyesha mwendelezo wa kuwa-harass waliokuwa-waminifu wa JPM. Naogopa kulisemea sana suala hili! Lakini kila mwenye macho anajua hatima ya watu waliokuwa karibu na walioaminiwa sana na JPM! Viongozi hawa (except wachache kwa sababu "mseto"!) wanatafutiwa style ya kuondoka bila wenye mamlaka kuchafua mikono yao. Kumsema Waziri tena openly mbele ya watu haiwezi kuwa bahati mbaya au tabia tu ya Mkuu huyo wa Mkoa. Ni ajenda ya makusudi kuondoa “remnants” za Magufuli. Sijasikia kakemewa na viongozi wake! Legacy ya magufuli haiwezi kuisha kwa kuwanyanyasa ‘wapendwa’ wake. Legacy yake iko mioyoni mwa watu waliojaza barabara na Stadiums tokea Dar es Salaam mpaka Chato. Legacy yake haifutiki kirahisi hivyo.

Mimi naona haya yote ni Siasa Uchwara, Ni woga (Cowardice) kwa wanaofanya hivyo kwa kujua Mamilioni ya watanzania walimpenda sana JPM akiwa hai na leo wanamkumbuka katika mengi sana kuanzia kwenye approach ya Corona, Upiga deal serikalini unaorudi kwa kasi na Budget isiyojali machungu ya wananchi. Leo tunarudi kwenye nyakati za “Mpende msipende Ndege ya Rais itanunuliwa hataka kama mkila nyasi”. Kutulazimisha kulipa kodi kubwa sana ya Transactions za Simu na kusema kuwa hilo lazima litokee bila shakani kiburi cha viongozi wa siasa wanaojiona miungu watu. Legacy ya Magufuli ni kuondoa kiburi hiki cha viongozi na kuondoa mizigo ya kodi kwa wananchi kwa kutumia vizuri kodi inayokusanywa. Hapa tutamkumbuka kama alivyosema.

Nimalizie kwa kusema kuwa kama baadhi ya viongozi wetu, waliopita au wasasa (ambao wengi wao wako hapo walipo kwa sababu ya JPM) KAMA hawakumpenda kiongozi wao au waliona madhambi yake na wakaogopa kusema , wasijifiche nyuma ya migogongo ya wapinzani wa JPM bali watoke hadharani waseme madhambi yake. Kama hawahusiki waje hadharani wawakemee watu kama akina Diallo na akina Mtaka.
 
Legasi ya kupotezwa kwa Ben Saanane na Azory siyo.....ok tunaisubiri kwa hamu...mpo chapter gani vile?
 

Wabongo hatutumii akili ......ndo maana nchi inakuwa na kodi za ajabu........UMEWAHI SIKIA WAP SERIKALI INAJENGEA WANANCHI NYUMBA ....... ..
 
Back
Top Bottom