LEMA: Baadhi ya wabunge kati ya 19 ni wake wa viongozi wakuu wa CHADEMA

Lemma kaamua kumkoma nyani giladi tu. Safi sana,Mbowe amewafanya watu wajinga sana.
Maana ya kumkoma nyani giladi ni nini mkuu?

Niliwahi kusikia hili neno kwa ngoma moja ja Professor J na pia kwa kingwendu alisema ana ngumi yake moja inaitwa kumkoma nyani giladi.

Tukirudi kwenye mada, wabunge 19 kua bungeni ni mradi wa Mbowe, hilo liko wazi.
 
Hizi habari amezigundua leo ? Au kwanini hakutwambia Kabla ? Ukishawaelewa Politicians nadhani utakuwa haushangazwi na lolote wanalosema.., It's all about Convenience...
 
Kumkoma nyani giladi yaani ukitaka kumuua nyani usimuangaliae usoni maana kiasi fulani nyani wamefanana na binadamu sasa ukimuangalia usoni utaona huruma unaona kama unaua binadamu mwenzako. Ishu ya wabunge 19 ina mkono wa Mbowe hilo halina ubishi tena. Maneno aliyosema leo Lemma kwa mtu ambaye alikuwa mtu wake wa karibu almost ndugu ilihitaji kweli ujasiri.
 
Hapo mkuu nimekupata vyema. Nimeongeza maarifa.

Lema kweli ameamua kumuua nyani bila kumuangalia usoni, ameamua aseme ukweli, aokoe chama.

Jamaa wamevumilia uhuni wa Mbowe sasa wamechoka. Wameamua mbwai na iwe mbwai.

Mbowe anatumia watu kama mtaji wake wa kiuchumi, huku nje anasema hivi halafu ndani anafanya mengine wakiwa ma ccm kitu kimoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…