Lema: Bodaboda imekuwa ni ajira ya Laana

Tupeni ridhaa muone mikakati yetu. Siyo miaka sirini yote ya uongozi hamna ubunifu wowote kazi yenu ni kuwasisitiza tu vijana wajiajiri. Kama mmeishiwa mbinu si mseme?
Kama mumekaa kwenye ubunge miaka 10 hakuna mlichofanya Kwa ngazi hiyo na Halmashauri mlioshika nani awape ridhaa watu wasio na sera wala mkakati?

Mkiacha kulalamika na kuorodhesha matatizo ya Nchi na mkaja na suluhisho ndio mtaaminiwa.
 
Laana watu Wanajenga wana maisha angetafuta namna nzuri ya kuongea aheshimu ajira za watu huyo kijana
Anajua laana ni Nini aende zake

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Huyu Nabii alitabiri hadi kifo cha Jiwe, kwahiyo atakuwa kaambiwa na Mungu kuhusu hao bodaboda.
 
Ndio kawapelekee ujinga wako kwamba vikao vya retreat vimeletwa na Lema.
Mbona umekasirika tena?

Kwan Lema alikuja Kwa kushtukiza Arusha?

Iweje siku hiyo hiyo mkubwa apangiwe safari ya Arusha?

Vp ujio wa Lisu na mkeka wa ma DC?
 
Kama mumekaa kwenye ubunge miaka 10 hakuna mlichofanya Kwa ngazi hiyo na Halmashauri mlioshika nani awape ridhaa watu wasio na sera wala mkakati?

Mkiacha kulalamika na kuorodhesha matatizo ya Nchi na mkaja na suluhisho ndio mtaaminiwa.
Tulitaka kwanza yule killer jpm aondoke ilin chi iwe shwali
 
Mbona umekasirika tena?

Kwan Lema alikuja Kwa kushtukiza Arusha?

Iweje siku hiyo hiyo mkubwa apangiwe safari ya Arusha?

Vp ujio wa Lisu na mkeka wa ma DC?
Kwani Rais anafanya kazi Kwa kuangalia ratiba za Lema? 😁😁
Acha ujinga
 
Mbona unarukaruka tu hueleweki unafafanua mambo ya nje ya mada? Hebu tueleweshe kwanini bodaboda ni laana, Huenda wewe ulimwelewa
 
Kwani Rais anafanya kazi Kwa kuangalia ratiba za Lema? 😁😁
Acha ujinga
Anyway, waeza Dhani najibizana nawe bt Nia yangu ni kujenga na kuboresha kiwango Cha Reasoning ya wengi wasomao majibizano yetu.

Ubarikiwe.
 
Mtu anamaliza degree kisha anapiga boda, hayo hayakua malengo. Hilo nijanga
Kazi hiyo sio yakujivunia. Hakuna boda anaejivunia kazi hiyo. Tatizo nikwamba hakuna mbadala ndio maana
 
Mbona unarukaruka tu hueleweki unafafanua mambo ya nje ya mada? Hebu tueleweshe kwanini bodaboda ni laana, Huenda wewe ulimwelewa
Unaweza kutajirika Kwa kufukuzana na upepo au kukwepa magari road?

Mfumo wa kuaminisha wanafunzi wanaofeli shule za kata kuwa wanaweza jiajiri kwenye boda ndo umelaaniwa.
 
Sawa. Wewe usiyekimbizana na magari hebu Tuambie NET WORTH yako ni kiasi Gani Ili uwa-inspire hawa wafukuza upepo
NET WORTH yangu binafsi inasaidiaje millions of Boda nchini?

Nashauri Tuipumzishe CCM maana imefika UKOMO wake kufikiri.
 
Hebu niambie, ni wapi hapa duniani wanakojielewa ambako utaukuta huu usafiri wa bodaboda? Kama hakuna, tafakari..
Kama hoja ni kuendesha maisha, si hata wanaofanya ukahaba wanaendesha maisha kwa ukahaba wao.
 
Sure Lema amekosea sana aisee maana vijana wamejiajiri sasa alitaka wakae mtaani kusubiri ajira hata nchi tajiri duniani zinazotoa mikopo haina maana eti wameajiri wananchi wote kwanza haya mawazo ya kivivu kabisa huyu anataka kutengeneza vijana wezi mpuuzi sana jamaa
 
Alichoongea Lema ni sahihi kabisa kazi ya kuendesha bodaboda haiwezi kuwa mbadala wa ajira rasmi iwe ya kuajiriwa au kujiajiri ni njaa tu ili watu waweze kusurvive.Uendeshaji wa bodaboda umewafanya vijana wengi wapoteze maisha au wawe tegemezi baada ya kupata ajali zilizotokana na bodaboda.
 
Hebu niambie, ni wapi hapa duniani wanakojielewa ambako utaukuta huu usafiri wa bodaboda? Kama hakuna, tafakari..
Kama hoja ni kuendesha maisha, si hata wanaofanya ukahaba wanaendesha maisha kwa ukahaba wao.
Kwaiyo unataka vijana waache kuendesha bodaboda wakajiuze wakawe mashoga kwakua mnatetea ushoga wapuuzi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…