Lema: Bodaboda imekuwa ni ajira ya Laana

Kabisa dear uwasilishaji ndiyo sio mzuri. Pengine alikua ana hoja lakini uwasilishaji huo hapana kwa kweli.
Lema huwa ni chizi, Wala sio uwasilishaji, kawaida hana akili huyo, ona jinsi alivyomshambulia yule Askofu Mkuu kwa sababu tu amewasaidia wananchi kwa kuwapa 100M, eti anasema ni Bora angeenda kuweka "tiles" kanisani kwake kwanza kuliko kusaidia watu, Sasa hapo Kuna akili kweli?
 
Punguza matusi na ujenge hoja, kwahiyo wewe unadhani bodaboda woote wamesoma?, na kwamba wasomi woote lazima waajiriwe?, au usafiri na usafirishaji sio sehemu ya ajira?, hivi tunapozungumzia makampuni Kama ya "Uber" yanatofauti gani na bodaboda na bajaji?, Ulitaka "Taxi" zote ziwe ni gari hadi vijijini?.
 
Kweli Boda ni laana.
anaebisha hii kauli ni mpuuzi
Upo sahihi kwasababu ni wajinga badala ya kuendelea na shughuli zao kujitafutia kipato wakakodiwa kwenda kumpokea Kwa maandamano.

Inawezekana Lema mnampenda sana na mnamuona Malaika ila kakosea sana hiyo kauli kwasababu hiyohiyo kazi wenye akili wanajenga,wanasomesha watoto na ndugu na kuendesha maisha yao.
 
Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema au Nabii Lema ni vema akatufafanulia vizuri laana ya Bodaboda iko maeneo gani

Je, Pikipiki Ndio zina laana? Sababu hata Bilionea MO na Mwanasiasa msomi Dr Kigwangala urafiki Wao ulikorofishwa na hizi Tukutuku

Je, Vijana wanaoziendesha Ndio Laana kwa sababu huku Unguja tunatumia Vespa miaka na miaka hakuna shida yoyote, Maafisa Kilimo, Maafisa Mifugo, Polisi, DAWASA wanatumia Pikipiki na hakuna shida yoyote

Au Wabunifu wa mradi wa Bodaboda kama ajira Mzee Lowassa na January Ndio walengwa

Au ni kwa sababu ndani ya Biblia hakuna mnyama mwenye miguu miwili aliyetumiwa kama chombo cha usafiri? Alitumika Punda, Farasi na Ngamia

Jumaa kareem!
 
NAONA UMELIVALIA NJUGA HAIKUSAIDII. BODABODA WENYEWE WANAFANYA HIYO ETI KAZI KWA HILA HAWANA JINSI, LAKINI KWA VINYWA VYAO HAWAPENDI MAANA HAIWAPELEKI POPOTE NA MWISHOWE WANAMALIZIA KWA KUWAKABA WATEJA WAO USIKU NA KUFUNGWA
 
Kwaiyo unataka vijana waache kuendesha bodaboda wakajiuze wakawe mashoga kwakua mnatetea ushoga wapuuzi sana
Nadhani hujaelewa. Wahenga walisema ukiona unasoma kitabu huelewi, ujue hukuandikiwa wewe!
 
HIvi umenielewa kweli? Halafu huwa hatusemi harafu!
 
Aliyefanikiwa kwa kutumia bodaboda mafanikio yake yana laana? Hapo umechemsha Lema.
Tena wako wengi,bodaboda Ina mgarantee Kijana sio chini ya 350k Kwa mwezi hata Mwalimu wa shule ya msingi hana lakini wale maarufu au walioko kwenye mazingira harsh wanafikisha hata 700k Kwa mwezi Sasa hii sio pesa ndogo.
 
Aliyefanikiwa kwa kutumia bodaboda mafanikio yake yana laana? Hapo umechemsha Lema.
Tatizo mnaleta ubishi katika uhalisia mkitumia itikadi zenu za kisiasa.
Lema kasema ukweli bila kurembaremba, hivi mzazi gani anaweza kujitapa kwa fahari kuwa "katika watoto wangu wanne nime bahatika 3 ni bodaboda"?
Kwa Tanzania hii iliyokosa ubunifu jinsi ya kusaidia vijana inaonekana boda ni suluhu, lakini ni kazi ya laana maana inaharibu maisha yao.
 
Sasa Lema!!!!! Bodaboda anamzidi mwalimu wa msingi na sekondari kwa kipato, hizo kazi ni za laana?? Hukufundishwa na mwalimu?
 
Mbona unarukaruka tu hueleweki unafafanua mambo ya nje ya mada? Hebu tueleweshe kwanini bodaboda ni laana, Huenda wewe ulimwelewa
Bodaboda siyo kazi ya laana hata siku moja,ila anachokiongelea ni kwamba kuna siku asilimia 70% ya Watanzania wengi wanaweza kuwa bodaboda ambako kuna ajira ya haraka kuliko ajira zote na kusababisha laana kwa kizazi kijacho.
 
Ndio ajira pekee unajivunza usiku na asubuhi unabeba abiria, haipiti mda unakutwa kwenye mtaro umekufa au hospital

Ni ajira pekee vijana wengi wanaikimbilia badala ya serikali kutoa ajira na kushawishi vijana wafanye mengine

Wenzetu wanajituma kwa taaluma walizosomea kwa kuwa ajira zipo nyingi
Sisi hao wanaojiita viongozi na vyeti vyao hawawezi kubuni chochote zaidi ya Tozo

Waziri wa fedha anafurahia kukopa tu huku akitudanganya na kusema zina unafuu
Halafu hatuoni anazipeleka wapi pa maana
Laana wanazo hao wenye elimu na hawajui namna ya kuzitumia na wote ni hali moja hakuna mwenye unafuu
 
Utawezaje kufunga goli ukiwa mtazamaji nje ya uwanja!
 
"Yaani watu wanaendesha familia kwa kazi hiyo" mbona hata wezi na makahaba wanaendesha familia zao, nao tuwapongeze!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…