Uchaguzi 2020 Lema: Msafara wa mgombea Urais, Tundu Lissu washambuliwa vibaya katika Ofisi ya CHADEMA Wilayani Hai, Kilimanjaro

Uchaguzi 2020 Lema: Msafara wa mgombea Urais, Tundu Lissu washambuliwa vibaya katika Ofisi ya CHADEMA Wilayani Hai, Kilimanjaro

Inasemekana mrusha mawe mmoja kauwawa na wananchi huko.

Polisi walikuwepo wakiangalia tu kama sinema vile.
Mkuu hii ni hatari sana watakuja kushituka wakati watu wameshajaa visasi mioyoni mwao.

Mungu atuepushe tufanye siasa za kistaarabu.
 
Tatizo wewe hujui, watu wa kaskazini siyo wale wa miaka ile, huyu tarumbeta wenu hawajui amekwenda kufanya mkutano au amekwenda kutafuta wadhamini? watu wa kaskazini ni wasomi, hiyo ni salamu tuu kuwa awamu hii kaskazini kwa upande wa Rais anajulikana, wazee walishaomba upatanisho na Mh. Magufuli hawataki kufanya makosa wanataka maendeleo. Pia hicho ni chama chao, wanashangaa lijitu limetokea wapi ambalo halijulikani miaka 3 lilikuwa wapi? hajui CHADEMA imepitia machungu gani eti yeye anakurupuka anaanza kuleta sera za uchochezi na RAMRI chonganishi. Wazee wa KILIMANJARO HONGERENI SANA
Endelea kuchochea hasira za watu ila usijejuta yakiwa yamehamia huko unakodhani kuna ulinzi wa kutosha.
 
Huu ni muda wa kudeploy red brigades kwenye matukio kama hayo. Wakija wahuni wachache wanakutana na nguvu sawa au ikibidi zaidi ya ile waliyokuja nayo. Muhenga Newton aliliona hilo kitambo sana: to every action, there should always be an equal and opposite reaction

..hiyo inaitwa provocation.

..mkijibu tu imekula kwenu.

..umebaki muda mfupi sana tuende kwenye uchaguzi.

..VUMILIENI.
 
Acha upuuzi wewe. Kwani wilayani kwake kuna uzio wa kuwazuia wahuni wanaorubuniwa na Mkuu wa wilaya?? Muda sio mrefu mtacheka kama hamtolia.

Wapuuzi ni nyie mnalundikana kama siafu halafu wanatokea wahuni watano au sita wanamshambulia Mgombea uRais ambaye amepita maeneo ya watu mapaka kule Shinyanga jirani kabisa na Chato lakini wameonyesha ustarabu mana wamefundishwa maana ya Demokrasia tofauti na Huyo mpevi aliyeshindwa kuwafundisha watu wa nyumbani kwake maana ya Chama chake na kuiamini itikadi ya Chama chake.

Mnashindwa na yule mwanamke kule Geita aliyegoma bendera kushushwa nyumbani kwake na watu wakamwelewa.

Hawa wenyeviti wa Vyama vya upinzani ni waajabu sana. Wote hawakubaliki kwao zaidi ya kutegemea huruma badala ya kujenga itikadi ya vyama vyao kwenye mioyo ya watu.

Hapo hai kuna sehemu ya mtu kufanya Uhalifu mchana kweupe mbele ya msafara asijulikane na kukamatwa na mkamgawa vipande vya mishakaki.
Mnatetea ujinga ,halafu mnailaumu Serikali ili iwasaidie nini kama mnapigwa mchana kweupe na watu wanaojulikana na kuonekana wazi.
 
Mkuu hii ni hatari sana watakuja kushituka wakati watu wameshajaa visasi mioyoni mwao.

Mungu atuepushe tufanye siasa za kistaarabu.
Rais Magufuli atuachie nchi yetu imemshinda.
 
Aliyekuwa Mbunge Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter amesema msafara wa Tundu Lissu umevamiwa katika Ofisi za Chama hicho Wilayani Hai

Amesema "Msafara wa mgombea Urais Mh Tundu Lissu umevamiwa na kushambuliwa vibaya katika ofisi ya CHADEMA HAI,magari yame haribiwa. Mgombea Uraisi na Team yake wako salama. Polisi wako lakini wana shuhudia, mkutano umevunjika. Taarifa kamili kuwajia"

Yaani cha kushangaza kuna watu hapa watatetea waleta fujo, wachoma ofisi, wavamiaji. Kama tulivyosema ukiwapata watu kwenye mioyo hakuna wa kuzuia. Wanatengeneza mazingira ya fujo halafu wasingizie upinzani!!!
 
Kuna kitu kinakwenda kumpata huyo DC wa hapo mwaka huu.
Tuliona haki iliwahi kudhulumiwa akaibuka mtu anaitwa mng'oa kucha , akatoa malalamiko hakusikilizwa, akalalamika tena hakusikilizwa, akaonya hakusikilizwa, akaonya tena hakusikilizwa.
Mwishowe mng'oa kucha wa watu akaamua kuhitimisha na kutoa hukumu haikupita wiki kama alivyosema hukumu ikatimia na mng'oa kucha kucha akaamua kutoweka mitandaoni.
 
Hii ni hatari kwa mstakabali wa Taifa,vipi upande wa pili wakiamua kujibu mashambulizi.

Wote kwa pamoja tukemee bila kujali vyama vyetu, maana hali ikibadilika haiangalii ulishiriki ama hukushiriki.
Hakuna chama chochote kinachohusika hapo. Ni wao wenyewe wanayatengeneza hayo matukio.
 
Yaani cha kushangaza kuna watu hapa watatetea waleta fujo, wachoma ofisi, wavamiaji. Kama tulivyosema ukiwapata watu kwenye mioyo hakuna wa kuzuia. Wanatengeneza mazingira ya fujo halafu wasingizie upinzani!!!
Hao ni wapinzani tu. Kwa nini iwe Hai?? Tumia ubongo wako vizuri. Kwa nini kwenye jimbo la Mwenyekiti unataka kutuaminisha kuwa Lissu hakjbaliki kwenye jimbo la Mbowe??
 
Back
Top Bottom