Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
Hiyo mentality ya kumtegemea mtu mmoja Lissu tu ni makosa makubwa sana.Mzee.
Kwa mtazamo wako tutampoteza lissu tumaini letu wanamabadiliko yaani tumtoe kafara lissu ili iwe prove ya matendo mabaya ya mfumo wa kutoa haki?
Ni heri tupige magoti lissu atoke tuanze upya mapambano
Kwa sababu, Lissu anaweza kushinda kesi akatoka leo, kesho akagongwa na basi akafa. Simuombei hivyo, naombea aishi maisha marefu, lakini, huu ni ukweli wa maisha tu.
Sasa hapo huoni kuwa kumtegemea mtu badala ya kujenga mfumo, kujenga movement ni makosa?
Unafikiri Mandela angekataa kusema I am ready to die, angekubali kutoka jela kwa masharti ya makaburu ANC wanepata kuchujua nchi walivyochujua?
Kuna siku nilikaa na Lissu tukawa tunaongea, nikamwambia nakushukuru sana kwa kazi yako, nikikubana sikubani kwa uchawa wa CCM, ni maswali ya kifalsafa. Nikamwambia wapinzani mnasema maneno mengi mazuri, mnapigania mambo mengi ya msingi. Lakini siasa za uoinzani si sawa na za kutawala. Watu wakioata power wanabadikika, tutajuaje nyie mkipata power hamtatubadilikia?
Jibu lake lilinifanya nimuheshimu zaidi na zaidi Lissu.
Hakusema kwamba sisi hatutabadilika, hakusema tuna mfumo bora zaidi. Alisema, wananchi inawabidi wasimamie misingi ya kikatiba bila mahaba, bila kujali nani anatawala.
Sasa Watanzania badala ya kujenga taasisi na kuangakia mifumo, wanamuangakia Lissu.
Hivi unaelewa kuwa Watanzania wana nguvu ya kuifanya mahakama imuachie Lissu kwenye hukumu ya not guilty bila kumpigia magoti Samia wala DPP?
Lissu asiuawe, Samia asipigiwe magoti, na haki itendeke?
Unafahamu kwamba Watanzania wana nguvu hiyo?