Lengai Ole Sabaya ashinda rufaa na kuachiwa huru na Mahakama Kuu ya Arusha
Kama lini aliwahi kuupiga mwingi? Yeye hana tu zile siasa za kishamba kama yule bush star wa chattle.
Hana ndio ndiomaana mnapumua baada ya kuonewa sana kwa miaka 5!
 
Serikali kwa mara nyingine ijitathmiini katika uwezo wa Idara na Taasisi zake kutayarisha kesi na mashahidi kwani zimefeli hivyo kushindwa ku-i-move Mahakama Kuu kuwa kulikuwa na kesi ya kusikilizwa kwa kutumia mizania ya kisheria.

Je tatizo ni kukosekana wanasheria wa serikali walioiva ? Je mfumo haki jinai (criminal justice system) yaani Polisi, TAKUKURU, DPP na Mahakama za chini zinakosa rasilimali watu wabobevu wa kuchunguza, kuandaa na kusikiliza tuhuma / kesi toka mwanzo wa mchakato mzima wa kutoa haki Au kesi hii ilikuwa kuna shindikizo?
SHINIKIZO LAZIMA. HATA HIZO ZINGINE HAMNA KITU.
 
Nitamshangaa Sabaya akiomba msamaha kwa hukumu hizi za mahakama zetu. Kama mtu amepatikana na ushahidi wa yale aliyoyatenda na bado anaachiwa, atakuwa ni zuzu kama ataomba msamaha. Labda ccm itoke madarakani ndio ataomba msamaha.
Anaachiwa kwani dhalimu wako yuko madarakani?
 
Hili la kuokoka na kutokuwa mbali na mlango wa kanisa ni ushauri tosha
 
Kashinda rufaa au wameamua kumuachia. Tabia haina dawa
 
Huyu script yake imeshaandikwa ila wanampa adabu kidogo kosa lake kuingiza taasisi kubwa ya Rais katika mambo ya kijinga angebeba msalaba tu mwenyewe ila kumtaja kuwa nimetumwa ndio wakampa adabu ila kisiasa hakuna tena maana baada ya huku hata yule lisemaji la Yanga zamani sijui sasa hivi mkuu wa wilaya wa wapi kimyaaa kama hayupo. Msg sent and delivered
Kutaja ndio kumemsaidia, mana koss sio lake ni yule aliemtuma. Lazima iwe hivyo ili asimwage mboga zaidi.
 
Tusubiri mwitikio wa Jamhuri ila wakiwa kimya huko kwingine mtelezo kijana anatoka na atarudi kwenye ukoka
View attachment 2213874
Wakili wa upande wa utetezi Moses Mahuna akieleza kuhusu Sabaya na wenzake
kushinda rufaa yao na kuachiliwa huru katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

View attachment 2213907

Sabaya na wenzake watatu wamebakiza ngwe moja ya hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mahakama Kuu ya kumwachia huru muda huu. Warufani wengine katika kesi hiyo ni Silvester Nyegu na Daniel Mbura, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Oktoba 15, mwaka 2021, Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo, alimtia hatiani Ole Sabaya na wenzake kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

View attachment 2213863
Ole Sabaya wakati akifikishwa Mahakamani kusikiliza rufaa yake Mei, 2022

Pia, soma=> Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha
 
Na usishangae akitoka akawafanyizia waliotoa ushahidi kwenye kesi yake, na wasifanywe lolote hata serikali ikijua.
Hahaha, kama ambavyo Mbowe ameanza tena kupanga mipango ya ugaidi na hakuna wa kumsumbua!
 
Serikali kwa mara nyingine ijitathmiini katika uwezo wa Idara na Taasisi zake kutayarisha kesi na mashahidi kwani zimefeli hivyo kushindwa ku-i-move Mahakama Kuu kuwa kulikuwa na kesi ya kusikilizwa kwa kutumia mizania ya kisheria.

Je tatizo ni kukosekana wanasheria wa serikali walioiva ? Je mfumo haki jinai (criminal justice system) yaani Polisi, TAKUKURU, DPP na Mahakama za chini zinakosa rasilimali watu wabobevu wa kuchunguza, kuandaa na kusikiliza tuhuma / kesi toka mwanzo wa mchakato mzima wa kutoa haki Au kesi hii ilikuwa kuna shindikizo?
Zaidi ya asilimia 60 ya watumishi wa umma hawana uwezo kwa mujibu wa Prof. M. Assad, ambao ndio ukweli wenyewe na hali halisi.
 
Back
Top Bottom