Lengai Ole Sabaya ashinda rufaa na kuachiwa huru na Mahakama Kuu ya Arusha
View attachment 2213874
Wakili wa upande wa utetezi Moses Mahuna akieleza kuhusu Sabaya na wenzake
kushinda rufaa yao na kuachiliwa huru katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Sabaya na wenzake watatu wamebakiza ngwe moja ya hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi baada ya Mahakama Kuu ya kumwachia huru muda huu. Warufani wengine katika kesi hiyo ni Silvester Nyegu na Daniel Mbura, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi kwa kutumia silaha.

Oktoba 15, mwaka 2021, Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo, alimtia hatiani Ole Sabaya na wenzake kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.



View attachment 2213863
Ole Sabaya wakati akifikishwa Mahakamani kusikiliza rufaa yake Mei, 2022


Pia, soma=> Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha
Duuh kweli maajabu kama ya mechi real madrid vs man city
 
Ole Sabaya Ameshinda Rufaa Yake Dhidi ya Jamhuri.
.
Jaji Wa Mahakama Kuu anashangaa aina ya Hukumu iliyoandikwa na Mhe. Odira ambyo ilikuwa haina Hata Legal Citation Wala Case Authorities za Kujenga hoja yake Dhidi ya Hukumu yake.
.
Jaji anasema Hukumu yoyote Ambayo Haina Case Authorities au Legal Citation Hyo Sio Hukumu Bali ni Mawazo binafsi ya Mwandika Hukumu.
.
Asante Sana adv. Majura Magafu Kwa Ushindi Huu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
kwa hiyo hakimu ambaye hakufanya kazi kiweledi atafutwa kazi au atapeta kama kawaida...
 
Katika hali isiyo ya kawaida, vijana wa Ufipa wameanza kuwa na hofu kubwa baada ya sabaya kurudi uraiani.

Inaelezwa kuwa hawajui cha kufanya hadi sasa, ikumbukwe sabaya ndio alikua kiboko yao kwenye siasa zao za majitaka.

Sabaya alileta usawa wa kisiasa kwenye ngome zao Arusha na Moshi, hivyo kuwa mwiba mchungu hadi kwa mwenyekiti wa kudumu.

Sabaya ni mtu safi, na mahakama imethibitish. Lakini sabaya sio mtu safi kwa wanasiasa wa Ufipa waliojaaa uongo, uzushi, na ubabaishaji wa kila aina.

Hivyo ni vizuri wakaelewa huu utakua mwisho wa uongo na uzushi wao baada ya Jemedari Sabaya kurudi uraiani.

Na hakika mahakama zipo huru kabisa na zimefanya kazi yake vizuri.

#SSH 2025# KAZI IENDELEEEEE#
Sema maana ya SII hasa imetenda kazi yake.
 
Serikali ya CCM ni wajanja sana. Yaani wameona watu wanapiga kelele kuhusu mafuta kupanda. Tayari wanaleta drama nyingine ya kuwapumbaza wananchi ili wasahau ya Mafuta. Kudadeki this time lazima tuite maji mmmaaa
 
Karibu uraiani Comrade SABAYA..

HAKI IMETENDEKA

Baada ya kushangilia hukumu ya Mbowe sasa ni wakati wa kula na kunywa kushangilia haki ya SABAYA.

Hakimu alifanya maamuzi kwa mihemko

KAZI INAENDELEA
 
Back
Top Bottom