Jambo la mtu na mkewe mipango ya maisha yao wanavyotaka kuishi ni juu yao.
Ndoa ina faragha yake. Jambo baya ni mtu kulazimisha au kulazimishwa kitu tu.
Unaweza kujiona unawatetea sana wanawake waweze kufaya kazi, wakati wenyewe hawataki kufanya kazi nje ya nyumba wanataka kufanya kazi nyumbani.
Kifupi haya ni maamuzi ya faragha ya ndani ya ndoa, ambayo, watu wakishakubaliana tu, hayahitaji mjadala, hayahitaji justification. Ukitaka kuyaingilia ndiyo mwanzo wa kuvunja ndoa za watu.
Ni kama mtu akiamua kuwa dini fulani, katika muktadha wa imani, uamuzi huo ni uhuru wa kikatiba na kibinadamu. Ukianza hata kuuhoji uamuzi huo, kwenye muktadha wa imani, unakuwa umevunja faragha ya msingi wa mtu.
Tatizo watu wengi hawajui mipaka, hawajui faragha, hawajui kitu gani kinaweza kuhojiwa na kitu gani hakiwezi kuhojiwa.