Uchaguzi 2020 Leo Mawakala wanaapishwa figisu zimeanza, sahihi za Mawakala zadaiwa kugushiwa. Polisi wachunguza

Naunga mkono hoja
 
Wananchi wamechoka kulaghaiwa na CCM Tume ya Uchaguzi inajiandaa kuvuruga amani iliyopo
 
Sasa wanasema watatoa ajira na ajira Kama hizo zikipatikana wanazifanyia figisu watu tukose pesa na hao Nec walaaniwe kuanzia sasa mpaka vizazi vyao na waadhibiwe kwa nguvu zote.
 
Uchaguzi unatakiwa uwe huru na haki, tunajua wamezoea figisu ,hatutaki figisu, wamezoea rushwa na kutekana ,hatutaki yote hayo, tunataka HAKI tu itendeke kwa kila hatua.
Muda wa kufanya mambo ya kitoto ya kihuni si wakati huu.Tendeni haki nchi iwe ya AMANI.

Hakuna amani kama hakuna haki kwani ,amani ni tunda la haki
 
Ninyi NEC mnataka kuifikisha nchi wapi? Mbona hamsikii?
 
Morogoro mjini nasikia wamegoma kuapisha wakala wa CHADEMA na raia zipo chini zinasubiria majibu
 
Huko Sumbawanga kuna wanne wa cdm wamekufa kwa ajali ya gari. Na taarifa za kiintelijensia zilizopo ni kuwa wakiteuliwa wengine watakufa kwa mtindo huo huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…