Uchaguzi 2020 Leo Mawakala wanaapishwa figisu zimeanza, sahihi za Mawakala zadaiwa kugushiwa. Polisi wachunguza

Uchaguzi 2020 Leo Mawakala wanaapishwa figisu zimeanza, sahihi za Mawakala zadaiwa kugushiwa. Polisi wachunguza

Wakuu

Kichwa cha uzi chahusika. Leo hatutaki kusikia sijui Lissu yupo wapi, sijui Lissu kafanya nini. Tunachotaka kusikia ni je mawakala wote wa upinzani wameapishwa au la?

Itakuwa ni ujinga uliopitiliza kumsikiliza Lissu huku jambo la muhimu zaidi likiachwa.

Nitaongea mengine baadae lakini kwa sasa nisiwachoshe.
Naunga mkono hoja
 
Wananchi wamechoka kulaghaiwa na CCM Tume ya Uchaguzi inajiandaa kuvuruga amani iliyopo
 
1603279672541.png
 
Sasa wanasema watatoa ajira na ajira Kama hizo zikipatikana wanazifanyia figisu watu tukose pesa na hao Nec walaaniwe kuanzia sasa mpaka vizazi vyao na waadhibiwe kwa nguvu zote.
 
Uchaguzi unatakiwa uwe huru na haki, tunajua wamezoea figisu ,hatutaki figisu, wamezoea rushwa na kutekana ,hatutaki yote hayo, tunataka HAKI tu itendeke kwa kila hatua.
Muda wa kufanya mambo ya kitoto ya kihuni si wakati huu.Tendeni haki nchi iwe ya AMANI.

Hakuna amani kama hakuna haki kwani ,amani ni tunda la haki
 
“Wagombea wanaambiwa Mawakala wataapa kwenye Tarafa nk. Hakuna ngazi ya Tarafa kwenye Uchaguzi. Mawakala wanapaswa kuapa ama kwa Msimamizi msaidizi ( kwenye Kata ) au kwa Msimamizi wa Uchaguzi ( Kwenye Jimbo ). Baadhi ya wasimamizi wa Uchaguzi wanasumbua wagombea MAKUSUDI”. Zitto Kabwe.

“Miaka yote katika chaguzi zote Mawakala wetu wanaapishwa makao makuu ya kata na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi. Leo Mkurugenzi anataka tusafirishe watu zaidi ya 1600 kwenda halmashauri maeneo mengine umbali wa km 60 kwa barabara zetu, risk, gharama na usumbufu mkubwa”. John Heche.

“Nimeongea na Mkurugenzi wa tume Dk Mahera akasema anatoa maelekezo kwa msimamizi wa uchaguzi lakini bado msimamizi amegoma. Badala ya uchaguzi kuwa wa wadau unakua mali ya msimamizi ambae alipaswa kuwa facilitator tu. Impunity,ujinga na uhuni”. John Heche.


UPDATES ====•

Mawakala wanne wa Chadema wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa, katika ajali ya gari iliyotokea barabara ya Molo - Sumbawanga mkoani Rukwa, Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Rukwa, Shadrack Malila amesema.
#MwananchiUpdates.

John Mnyika: Jitihada za mawasiliano na NEC juzi, jana na leo mpaka muda huu kudhibiti hujuma kwenye uapishaji wa mawakala zimekwama maeneo mengi. Nitazungumza vyombo vya habari HQ saa 8 mchana. Kwa sasa , #PeoplesPower itumike maeneo ambayo hujuma zinaendelea. #SasaBasi
Ninyi NEC mnataka kuifikisha nchi wapi? Mbona hamsikii?
 
Morogoro mjini nasikia wamegoma kuapisha wakala wa CHADEMA na raia zipo chini zinasubiria majibu
Ek2a5K2WMAAH-eL.jpeg
 
Huko Sumbawanga kuna wanne wa cdm wamekufa kwa ajali ya gari. Na taarifa za kiintelijensia zilizopo ni kuwa wakiteuliwa wengine watakufa kwa mtindo huo huo.
 
Back
Top Bottom