Leo naamka na watu wajinga wanaotaka kufanya sherehe kubwa kwa kuwachangisha wengine

Aisee inakera ,Kun mtu alinipa KADI .Sikuchangia ,na hakika wakati huo nilikuwa juu ya nawe! Akiwa honeymoon Dubai alinitumia ujumbe akiniuliza ..Vipi Mkuu mbona hukunichangia?!😠😠
Eheheheh
Bila shaka alipokuuliza alikuwa juu ya kifua cha mwenzake
 
We ujaishi mtaa wa kaza moyo.
Unajaribu tu kuongea kama umetoka chuo juzi
 
Mimi huwa sichangii mchango wa harusi wala maziko.

Uislam mwema sana. Harusi ni ndoa na mshahidi wawili msikitini inatosha, kama una uwezo wa kuwakirimu watu fanya karamu. Kama hauna uwezo usichangiishe mtu.

Maziko ndiyo kabisa, kinachotakiwa kimzike mtu ni chake mwenyewe alichowacha.

Watu siku hizi wanajifaharisha wakati hawaimudu fahari.

Tujikune tunapofikia.
 
Eheheheh
Hatari.
Unanikumbusha mwamba wa Ukonga aliyeweka X nyekundu picha ya kaka yake na kupita kukusanya shekeli.
Alipata nyingi mwishowe bro akatonywa kilitembea kichapo
 
Waislamu mmenyooka sana kwenye mambo mengi
 
Ila kumbuka ukifiwa ,ukiumwa usitembeze bakuri au kusindikizwa kwenye mazishi.
Mtego unaanzia hapo sio Sheree tu
Mkuu ugonjwa na kifo havina mjadala huwa dharura. Lakini harusi au ndoa ni sio suala la dharura.
Unakuta mtu anataka kuoa familia ya muoaji inatamka kabisaa kikaoni ina laki 1 tu halafu watu wengine ndo wachange mamilioni hadi MAHARI !
Unadhani hilo njemba likioa litamthamini huyo mke? Wakati hata halijui gharama za kuoa zimetoka wapi?!!
Kiukweli ninakerwa sana na michango ya aina hii ni michango ya hovyo.

TUCHANGIANE KWENYE MISIBA NA MARADHI NA MICHANGO ISIWE YA ANASA
 
Ni kweli Uislam ,ingawaje Si uamini 😁 upo realistic kwenye masuala mengi tu! Ungekuwa mjadala wa Dini ningetolea mfano ...Good morning Faiza Foxy !
 
Binadamu unawafahamu au unawasikia.

Unaweza ushiriki kwenye msiba alafu kosa dogo mfano ushindwe kula,kukesha msibani au kujitenga basi tambua watafanya hivo.

Hata ilo la Sheree tu wanaweza kukuchukulia
 
Nimeitafuta sana hiyo ID sikuipata, ilisheheni mawazo mazuri sana! Mkuu naomba kama ninaweza kuipata tena nipitie zile content zilizopo kwenye tharead ya mawazo mbalimbali ya biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…