Leo naamka na watu wajinga wanaotaka kufanya sherehe kubwa kwa kuwachangisha wengine

Leo naamka na watu wajinga wanaotaka kufanya sherehe kubwa kwa kuwachangisha wengine

Mchango wa harusi 10,000 sijawahi ona. Na huyo utakayemchangia elf 10 hataifikisha kwenye michango ataishia kuitumia kwa shida zake binafsi.

Itakua ya Birthday maana watu 20 wakitoa hizo 10k kila mtu, Cake ya 50k, soda 30k, vikali 30k, pilau nyama 50k inayobaki ya birthday girl/boy kununua nguo na kiatu Mtaa wa Congo Kariakoo.

Makeup atafanyiwa na shosti wake anaemiliki salon Mtaa wa nyuma buree [emoji108]
 
Itakua ya Birthday maana watu 20 wakitoa hizo 10k kila mtu, Cake ya 50k, soda 30k, vikali 30k, pilau nyama 50k inayobaki ya birthday girl/boy kununua nguo na kiatu Mtaa wa Congo Kariakoo.

Makeup atafanyiwa na shosti wake anaemiliki salon Mtaa wa nyuma buree [emoji108]
OKeee
 
Moja kwa moja kwenye mada.

Jana wakati naingia ofisini nakuta kadi ya mchango wa harusi mezani nikaambiwa na mfanyakazi mwenzangu kuwa ni yangu.

Nafunua ndani nakuta haina hata jina Iko plain na wanaooana siwajui. Nikamuuliza yule mfanyakazi mwenzangu vipi mbona haina jina? Akasema wewe andika jina lako kadi kasambaza mama mmoja wa pale canteen mtoto wake anaoa.

Nilimuuliza ni mama yupi? Akanipa maelezo kuhusu huyo mama bado sijamjua, yawezekana tunaonana tu ila ndo vile simjui.

Niliwaza nikagundua kuwa huyu mama ananifahamu kidogo tu ndio maana hata jina langu kashindwa kuandika kwenye hii kadi. Nikamuuliza yule dada kwanini huyu mama atoe kadi kiholela? Mada ikaiashia hapo.

Hivi watu kama hawa ukiwaita wajinga unakosea? Kwanini mtu asifanye sherehe kwa kipato chake?

Kuwachangia mamilioni vijana kisha kuwafanyia sherehe kubwa baadaye wanaishi maisha ya kuungaunga na kuanza kutafuta ajira ni sawa na kusema walianza maisha ya fahari kisha wakaishi maisha ya kimaskini.
Binafsi michango ya hharusi na send off nachanga ila naangalia ni nani namchangia.

Ndoa nilifungia kwa DC Ilala kuepuka kashkashi zisizo na sababu. Nitaanza vipi kumdai mtu nisiyemkopesha? Maana kukusanya michango vita yake ni kama unamdai mtu.

Kijana anza maisha kwa level yako kisha pambana, inuka. Ukiwa na pesa utaweza kufanyia harusi hata Juu ya puto kwenye hifadhi ya Tarangire au Serengeti na watu watakuzawadia mamilioni mengi.

Mimi kijana akija kwangu na wazo zuri la kumwinua nawiwa kumsaidia. Nimetoa support kwa vijana kadhaa mitaani, hata hapa JF nilianzisha kamchezo nilianza kutoa mitaji midogomidogo rejea account yangu ya zamani niliyopigwa ban ya BONDE LA BARAKA.
Bro kuna gharama kwenye hiz Mambo lakin kuna faida kubwa. Jitahd uwe sehem ya jamii. Ckuambii uchangie harus zote lakin hakikisha na wewe na sehem ya watu. Kuna watu bilionears nawajua lakin wanachanga. Hawahtaji hela yako wanahtaji uwepo wako. Furah na watu na kulia nao ndio maisha. Achana ubinafs wa kizungu. Mtu kama amepewa miaka 40 ya kuishi na katika hizo siku akakupa hapo cku moja huyo mtu ni muhim kwako sana. Ni kama ukiwa na gar jitahd hata kama una gar cku moja moja unapanda dalala utakuja kufikir tofauti.
 
Ndoa au sherehe si dharura so kulamtu ajipange au tuanze mfumo wa watu kuja na vyajula na vinywaji vyetu kwenye hizo sherehe zunu kama hamna hela za kuandaa sherehe hiZo
 
Kwani kwenye ukristo imeandikwa wapi ndoa au harusi kuwe na sherehe kubwa.
Imeandikwa wapi mazishi yawe ya gharama au msiba uwe wa siku nyingi kabla ya mazishi?

Yale yote yenye gharama kwa wakristo ni kujitakia. Shela na suti kwenye ndoa siyo lazima.
Sanduku la kuzikia na suti ya marehemu ni anasa tu. Mkristo anaweza zikwa hata na gunia au akiwa mtupu au akachomwa moto tu.
Unayumba mkuu
 
Mtu akikupa kadi ya mchango kama huna hela mwambie tu sina. Usiharibu bajeti au kuingia kwenye madeni kwa starehe za watu.
Mimi huwa nachua ten nalikunja halafu namfinyia kwa stori nyingi na vicheko namwambia dont look it, dont show me, dont show anyone, basi na yeye analitia mfukoni bila kuangalia huyooo.
 
Kiukweli harusi zinatutia umasikini mtu hata hamjuani sana anataka mchango na masalamu kibao atayaanzisha ,akishafanikisha jambo lake njiani anakupita kama hakujui utadhani hukumchangia ,pia waliosoma na wew wanataka michango,nyumba za ibada, makazini,mtaani ,ndugu nao Kila sehem michango alafu hapo unakuta una kiwanja hakina hata tofali 50....mim harusi sitochangia kbsa nishasema haiwezekani unakuwa na kadi zaidi ya 6 na zote wameweka single eti 70 au laki Moja ,nendeni mkafunge harusi za kiserikali msilazimishe " " kula muwa
 
Kuwachangia mamilioni vijana kisha kuwafanyia sherehe kubwa baadaye wanaishi maisha ya kuungaunga na kuanza kutafuta ajira ni sawa na kusema walianza maisha ya fahari kisha wakaishi maisha ya kimaskini.
Binafsi michango ya hharusi na send off nachanga ila naangalia ni nani namchangia
Mimi nachangia wagonjwa tu. Hata nikikuchangia sizidishe elfu 50 never.
 
Back
Top Bottom