Leo natimiza miaka 5 na mke wangu, siku ya kwanza kutoka date alinipa ujumbe mzuri sana

Ngoja ukiijua michepuko yake ndiyo utakuja kujua hujui
Nyinyi ndio wale fungu la kukosa kwenye mapenzi,

Kwahiyo mnaishi kwenye dunia yenu mliyojitengenezea ya kuwa hakuna mapenzi ya ukweli.

Pole bro.
 
Si ndio team kataa ndoa hao?

Sijambo mkwe wangu, kitambo sana!
Hahahaha nifah

Kwani wewe uko kwenye ndoa hapo!?.

Sisi tunakataa ndoa ila hatujasema mahali hatutaki mahusiano na Wanawake.

Tunawapenzi ila concept ya ndoa ndio haituikubali.

Tuna familia huku kitaa ila Ile concept ya kufangamana na mtu kinafiki hadi kifo ndio hatuikubali.

Tunaamini Katia hiari. Kwani hiari yashindwa utumwa.

Bila shaka hata wewe na Ze bolidi mliapply hiari kuushinda utumwa.
 
Mkuu, naona kuna namna hujanielewa au tuna mtazamo tofauti ambao sio vibaya pia.

Mimi naamini kilele cha mapenzi ni ndoa, huwezi kusema unampenda sana huyo mpenzi uliyenaye ila hutaki kufungamana nae! Hayo ni mapenzi ya aina mpya ambayo siyajui.

Na ndoa ni hiyari pia, ukiona ndoa ni shuruti bado hujampenda kweli huyo unayefungamana nae hadi kifo.

Nafikiri umeyapata majibu ya swali lako la mwisho.
 
Hawa wanawake wa English nyingi huwa malaya sana sijui nataka kusema nini

Ila usijinyonge tu siku yakikukuta
 
Miaka mitano bado ni michache sana,hata hivyo hongera sana mkuu.
 
Kuna jambo umelikosea kwa kujua ama bila kujua.

Mkeo ama mwanamke wako, huwa hasifiwi hadharani kwa tambo kama ulizozitamka wewe.

Ndiyo maana kuna comment zingine zimekunanga sana.

Unapomtambulisha mkeo kwa watu ama marafiki zako, ishia tu kusema: ... 'Huyu bi flani ndiye mke wangu wajameni'...

Sasa hapo 'hadhira' ndiyo itayokupangia sifa za mke wako, mrembo au kavaa sura ya babake!

Halafu, wanawake wote duniani, ni wazuri kwa mantiki kwamba kila sura ya mwanamke imeumbwa mahsusi kwa ajili ya chaguo la mwanamme flani.

Ndiyo maana kuna msemo kwamba: 'uzuri/urembo wa mwanamke upo machoni pa mwanaume ampendaye.

Mkeo unayemsifia kwa uzuri, kwa mwanamme mwingine aweza kuwa siyo mzuri kama unavyomuona wewe machoni pako.

Siku nyingine usirudie kuziweka sifa za mkeo kwenye kadamnasi ni tabia ya kutia fedheha hiyo.

Enzi zetu za ujana usingeweza kunitajia sifa za uzuri wa mwanamke wako bila kitendo hicho kukufanya ujute sana, maana nilikuwa ni 'samaki asiyepisha chambo', nilikuwa siwezi samehe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ