Leo natimiza miaka 5 na mke wangu, siku ya kwanza kutoka date alinipa ujumbe mzuri sana

Miaka mitano, bado kabisa shetani hajaanza kuwafuatilia. Wenye miaka 30 na kuendelea ndio Wana kila sababu ya kujipongeza maana shetani ameachana nao.
Shetani hayupo mkuu hizo stori tu.

nilikubaliana kwamba naishi na mtu dhaifu na mimi ni dhaifu pia makosa ni lazima.

Hakuna ndoa plain isiyokuwa na changamoto, ila lazima tusamehane maisha yaendelee.
Mkuu wewe ushaoa?
 
Sisi tulifikisha miaka 15 na bado tukaachana, nikiwa na muda nitawaletea jumbe zote nzuri tulizoshare since day 1.
 
Sisi tulifikisha miaka 15 na bado tukaachana, nikiwa na muda nitawaletea jumbe zote nzuri tulizoshare since day 1.
Pole sana mkuu.

Nafikiri ulienjoy moment kwa wakati huo?

Mimi pia nimepita kwenye mahusano mabaya na magumu hata ya usaliti.

The beautiful of life lies in the memory we create.

Ulete tujifunze.
 
Hongera Sana!
Na hii ndo Radha ya Ndoa Hasa ukimpata Mtu sahihi..
"Soul mate"

Naomba Baraka ndoa Yenu izidi kuimarika Na muepushwe na Misukosuko na Upepo mbaya katika ndoa endapo mtapitia Ugumu utambue ni Just maisha ya Kawaida na ujue jinsi ya kuyavuka..

Mikwaruzano, Ugomvi kutoelewana zote hizi ni hatua na hakikisha unaisolve Mara tu inapotokea Pride,Ego na Ubinafsi Hivi viwekeni kando mtaongeza maisha mengi sana kwenye ndoa..

kongole Mimi na Shemeji yako Huu mwaka wetu wa 17
 
Daaah hongera sana kaka mungu akusaidie uendelee kumtunza mke wako na mwanao, mimi sijapata tu ila nikipata nikaona wakuifaa nitaoa.
Mke anaweza kukuweka kwenye reli au akakutoa maisha ya ukapera yanachosha kubadilika wanawake pesa hata uioni unayopata inaenda wapi.
 
Mke wangu alikuwa anaulizia sehem kipindi hicho nina kibanda nikamwambia nisubir nimuuzie mteja. Akasubiri nikamalizana na mteja. Nikawa namuelekeza haelewi ikabidi nimpeleke akaniomba nimsubiri. Akarudi baada ya dakika kama 5. Njian stor hapa na pale akataka kujua kwangu. By then anasoma chuo mwaka wa3. Cku hiyo hiyo akajua kwangu na ndio kuoa hivyo. Tuna miaka 23 cjawah kumpiga wala kumtukana. Cna la zaid kumuongelea ila. Ninamshukuru Mungu sana. Alijua kunipendelea. Tuna watoto wanne nathubutu kusema tumebarikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…