Licha ya Rais kujitahidi kuchapa kazi lakini bado Wananchi hawamuelewi!

Licha ya Rais kujitahidi kuchapa kazi lakini bado Wananchi hawamuelewi!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Sabato Njema!

Tangu Rais arithi kiti cha Urais mwaka Jana hajapumzika wala sijasikia Kama alipata likizo. Anachapa kazi, Leo yupo huku kesho yupo Kule. Anachapa kazi.

Lakini licha ya jitihada zake zote katika kulitumikia taifa hili bado Wananchi hawamuelewi.

Hii inasababishwa na nini? Kuna yeyote anaweza kutuambia sababu ya hayo?

Mimi nikajiuliza maswali haya labda ni sehemu ya sababu;

1. Je ni Kwa sababu yeye sio mwanaume?

2. Je ni kutokana na gharama za maisha kupanda maradufu?

3. Je, ni maneno au Ile minong'ono kuwa nchi imerudi kuwa Shamba la Bibi?

4. Je, ni Kwa sababu Vijana hawana Ajira za uhakika Hali inayowafanya wakate tamaa?

5. Je, ni Kwa sababu aliowateua wanajulikana vibaya Kwa wananchi?

Unafikiri nini KIFANYIKE ili Wananchi wamkubali au wakubali kazi zake?

Taikon yeye msimamo wake ni kuwa;
i. anasapoti Rais au kiongozi yeyote apendaye HAKI,

ii. Asiye mroho, Mlafi wa Mali,
iii. Asiyejigeuza mungumtu, anayekubali kukosolewa,
iv. Anayeheshimu watu na kuwatumikia na sio wao wamtumikie.
v. Anayekemea na kuhakikisha Wezi wa Mali za nchi wanapewa Haki Yao ikiwa ni pamoja na adhabu Kali Kwa mujibu wa sheria.
vi. Atakayefanya Raia wasitawaliwe na Wageni. Wasigeuzwe Watumwa katika nchi Yao wenyewe.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ukweli ni kuwa anajitahidi sana, sema ndo hivyo kuna walaaniwa kadhaa daima wao huwa hawaoni jema la mtu, na ukizingatia muda mgumu alioingia huyu basi yote yanampa changamoto......walaaniwa wanakesha kupika na kukuza chochote chenye kuyumba ili imani itoweke imani na wakati huohuo hudunisha kila alifanyalo ili agenda yao itimie.
 
Tulikuwa tunalalamika kuwa Kikwete dhaifu, tukaanza kulalamika kuwa Magufuli ni Dikteta, kaja Tausi wetu Samia mpolee na lafudhi yake isiyotisha nae...

Au tatizo liko kwenye Afroshirazi?
 
Baada ya mfalme Suleimani kufariki, Rehoboamu akasimikwa kuwa mfalme badala yake. Wazee wa Israeli wakamwendea na kumuomba awapunguzie uzito wa kazi, kodi na ugumu wa maisha ambao baba yake Suleimani aliwafanyisha waisraeli. Washauri wa baba yake walimwambia kama atasikiliza kilio cha raia wake kuhusu ugumu wa maisha na kuwapunguzia kazi ngumu na kodi zisizo na msingi basi watu wale wangemtumikia na kumtii maisha yao yote.

Rehoboamu akaamua kwenda kufuata ushauri wa vijana wenzake wasiokuwa na akili, ambao wengi wao walikuwa wamezaliwa kwenye familia za kibwanyenye za Israeli. Hichi kikundi kilikuwa kinaamini kwamba wao ndiyo wenye haki ya kutawala wengine, au kileo hawa ndiyo wale wanaojiiita NCHI INA WENYEWE. Basi wakamwambia Rehoboamu kawaambie wale raia kwamba kama baba yangu Suleimani aliwapiga kwa mijeredi basi mimi nitawapiga kwa ng'e (Mijeredi ya chuma) na kuwaongezea kazi na kodi zaidi.

Muda haukupita, Israeli yote ikaanza kuleta minong'ono ya kutoridhika na mfalme wao mpya na ikafanyika hujuma kubwa sana ambapo nchi nzima ikamuasi Rehoboamu na kumuachia kabila la YUDA tu ambalo lilikuwa linapata raha wakati wengine wote wakihangaika na tozo na ugumu wa maisha.

NB 1: Ikumbukwe tu, ufalme wa Israel ulikuwa ni muunganiko wa mataifa mawili, YUDA (Hebroni) ambalo ni dogo na Israel ambalo ni kubwa. Basi kwasababu Rehoboamu alikuwa ametoka taifa dogo ndani ya muungano ilitakiwa acheze karata zake vizuri, kwasababu mwisho wa siku waisraeli wote waliichukia hadi YUDA kwasababu Rehoboamu aliwawekea kodi kubwa Israel huku nchini kwake YUDA wakiwa wanapata maisha mazuri.

Hasira na manung'uniko zilikuwa nyingi na mwisho wa siku muungano wa nchi mbili, (moja kubwa na moja ndogo) ukavunjika kwasababu mfalme alipendelea upande wa kwao huku upande wa pili wa muungano ukiwa na malalamiko aliyoyapuuza kwa kebehi na vijembe.
 
Sabato Njema!

Tangu Rais arithi kiti cha Urais mwaka Jana hajapumzika wala sijasikia Kama alipata likizo. Anachapa kazi, Leo yupo huku kesho yupo Kule. Anachapa kazi.
Lakini licha ya jitihada zake zote katika kulitumikia taifa hili bado Wananchi hawamuelewi.

Hii inasababishwa na nini? Kuna yeyote anaweza kutuambia sababu ya hayo?

Mimi nikajiuliza maswali haya labda ni sehemu ya sababu;

1. Je ni Kwa sababu yeye sio mwanaume?
2. Je ni kutokana na gharama za maisha kupanda maradufu?

3. Je ni maneno au Ile minong'ono kuwa nchi imerudi kuwa Shamba la Bibi?

4. Je ni Kwa sababu Vijana hawana Ajira za uhakika Hali inayowafanya wakate tamaa?

5. Je ni Kwa sababu aliowateua wanajulikana vibaya Kwa wananchi?

Unafikiri nini KIFANYIKE ili Wananchi wamkubali au wakubali kazi zake?

Taikon yeye msimamo wake ni kuwa;
i. anasapoti Rais au kiongozi yeyote apendaye HAKI,

ii. asiye mroho, Mlafi wa Mali,
iii. asiyejigeuza mungumtu, anayekubali kukosolewa,
iv. anayeheshimu watu na kuwatumikia na sio wao wamtumikie.
v. Anayekemea na kuhakikisha Wezi wa Mali za nchi wanapewa Haki Yao ikiwa ni pamoja na adhabu Kali Kwa mujibu wa sheria.
vi. Atakayefanya Raia wasitawaliwe na Wageni. Wasigeuzwe Watumwa katika nchi Yao wenyewe.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Labda nyie wa mjini ndio hamuelewi ila sie wa Vijijini tunamuelewa..

Sio lazima wote mumuelewe wengine waendelee kupinga Pinga ndio ilipo riziki yao.
 
Anajichanganya yeye mwenyewe.

1. Anafukuza wamachinga bila kuwa na sehemu za kutosha kuwaweka, anataka wakale wapi?
2. Anafukuza wamasai ili kufurahisha mwarabu
3. Anafanya teuzi za ajabu ajabu. Sasa mtu kama Kingai alifaa kuwa na nafasi ile?
4. Anakumbatia wabunge 19 walioko bungeni kinyume cha katiba
5. Hana ubunifu wa vyanzo vya mapato, yeye kutwa kucha anakopa tu anakopa tu
6. Anatuwekea tozo na kodi za ajabu ajabu, Tozo kwenye miamala ya simu, tozo tukitoa pesa zetu benki, anatulipisha kodi ya jengo la mwenye nyumba pindi tukinunua LUKU
7. Anatangaza kutuongezea mishahara kwa 23.3% halafu anaenda kutuongezea buku kumikumi, kisha anaichukua juu kwa juu tukitoa pesa benki.
8. Sisi tunataka katiba mpya, yeye anajifanya kuunda tume mpya ya Mukandala wakati Jaji Warioba alishamaliza kazi!

Sasa mtu kama huyu tutaanzia wapi kumuelewa kwa mfano?
 
So far mama yupo vizuri, ugumu wa maisha uliopo haujaletwq na mama, hata Mimi pia nasulubika lakini kesi ya shetani Putin siwezi kumuuzia mama.

Mbaya wetu ni Putin tuache unafki.
 
Baada ya mfalme Suleimani kufariki, Rehoboamu akasimikwa kumwa mfalme badala yake. Wazee wa Israeli wakamwendea na kumuomba awapunguzie uzito wa kazi, kodi na ugumu wa maisha ambao baba yake Suleimani aliwafanyisha waisraeli. Washauri wa baba yake walimwambia kama atasikiliza kilio cha raia wake kuhusu ugumu wa maisha na kuwapunguzia kazi ngumu na kodi zisizo na msingi basi watu wale wangemtumikia na kumtii maisha yao yote.

Rehoboamu akaamua kwenda kufuata ushauri wa vijana wenzake wasiokuwa na akili, ambao wengi wao walikuwa wamezaliwa kwenye familia za kibwanyenye za Israeli. Hichi kikundi kilikuwa kinaamini kwamba wao ndiyo wenye haki ya kutawala wengine, au kileo hawa ndiyo wale wanaojiiita NCHI INA WENYEWE. Basi wakamwambia Rehoboamu kawaambie wale raia kwamba kama baba yangu Suleimani aliwapiga kwa mijeredi basi mimi nitawapiga kwa ng'e (Mijeredi ya chuma) na kuwaongezea kazi na kodi zaidi.

Muda haukupita, Israeli yote ikaanza kuleta minong'ono na ikafanyika hujuma kubwa sana ambapo nchi nzima ikamuasi Rehoboamu na kumuachia kabila la YUDA tu ambalo lilikuwa lilikuwa linapata raha wakati wengine wote wakihangaika na tozo na ugumu wa maisha.

NB 1: Ikumbukwe tu, ufalme wa Israel ulikuwa ni muunganiko wa mataifa mawili, YUDA (Hebroni) ambalo ni dogo na Israel ambalo ni kubwa. Basi kwasababu Rehoboamu alikuwa ametoka taifa dogo ilitakiwa acheze karata zake vizuri, kwasababu mwisho wa siku Israeli iliamua kuichukia hadi YUDA kwasababu Rehoboamu aliwawekea kodi kubwa Israel huku nchini kwake YUDA wakiwa wanapata maisha mazuri.

Hasira na manung'uniko zilikuwa nyingi na mwisho wa siku muungano wa nchi mbili, (moja kubwa na moja ndogo) ukavunjika kwasababu mfalme alipendelea upande wa kwao huku upande wa pili wa muungano ukiwa na malalamiko aliyoyapuuza kwa kebehi na vijembe.

Ngoja nikasome kitabu cha Wafalme Kwanza Mkuu. Kabla sijachangia chochote
 
Back
Top Bottom