Kwa akili hizi, Siwezi endelea bishana na wewe...HUJITAMBUI.
Hawa wengine kujadiliana nao ni kujisumbua tu.
Yani hawana hata elimu ya msingi kuhusu mambo kama uhuru wa mtu binafsi, wote wamekulia kama mifugo wanaswagwaswagwa tu "hameni kwenye vijiji vya Ujamaa, Mwalimu Nyerere kasema" wanahama kwa lazima kama ng'ombe. Hawajhi hata uhuru ni nini.
Wanaambiwa haya nunueni vyakula kwenye maduka ya kaya tu, ukinunua kwingine ni ulanguzi, wanakubali.
Wanaambiwa chama ni kimoja, CCM tu, hakuna chama kingine, wanakubali.
Wanaambiwa "Zidumu fikra za Mwenyekitii" wanaitikia "Zidumuuu".
Sasa watu kama hawa washazoea kwenda ki ng'ombe ng'ombe kwa kufuata kundi, herd mentality, kuja kuwaeleza kuwa mtu mmoja mmoja ana haki za kujiamulia mambo katika maisha yake mwenyewe mpaka wakakuelewa ni kazi sana. Ni kama wanahitaji rewiring kwenye ubongo kuelewa.
Wanakuwa kama samaki ambao maisha yao yote wamekulia baharini kwenye maji, ukiwaambia kuna jangwa la Sahara huko hakuna maji, hawawezi kukuelewa.
Hili ni tatizo kubwa sana katika kufanya mazungumzo na Watanzania wengi sana.
Wana mawazo mafupi sana lakini ni wabishi kupita maelezo.