Lindi: Mtumishi wa LATRA amtishia sime dereva wa lori ili ampe leseni

Lindi: Mtumishi wa LATRA amtishia sime dereva wa lori ili ampe leseni

Kuna siku nilisema humu.kazi ya kukagua ubovu wa gari na kudai reseni Ni kazi ya traffic watu wakanibishia.
Polisi wa kawaida Hana mamlaka ya kukagua ubovu wa gari au reseni.
Huyu awe wa mfano! akauze chips huko! kazi ya leseni kudai ni ya Traffic police na wenyewe walikuwa hapohapo! huu ni ujinga wa kiwango cha Trump.
 
Manase nimesoma nae udsm.. ni mtata sana...
Tofautisha utata na upumbavu,huyu manase ni mpumbavu.
Ni basi tu imekuwa bahati hili limefika mitandaoni lakini kuna mengi sana ya hovyo kwenye taasisi nyingi sana zenye mamlaka yakupigisha watu faini,yanayoendelea mamlaka kama TRA yanatisha,watu wanaonewa sana.
 
Hilo gari lake ajiandae kuliuza ili kujikimu na ukali wa maisha maana kuna uwezekano mkubwa wa kufukuzwa kazi kwa tukio hilo.

Muajiri sio LATRA peke yake na kazi ameshafanya sehemu nyingi tu na bado kujenga na hata kununua magari hajafanya kwa hela za LATRA. LATRA ameingia mwaka jana tu akitokea Huawei, pia ameshafanya kazi sehemu nyingi kwa cv yake tu, amefanya Nabaki Africa, bandari kavu ya Ami, Alistair Logistics na Huawei then ndio akaenda LATRA mwaka jana.

Muajiri sio LATRA tu. Kama CV yako nzuri na una uzoefu na connection huwezi kosa kazi. Manase anavyo vyote hivyo. Hawezi kaa kijiweni muda mrefu hata kama akifukuzwa LATRA. Pia bado kijana tu hajavuka 33 nguvu za kupambana na maisha anazo.
 
Kwanza anaitwa nani, na hapo tukio lilipo tokea ni wapi??
Hapo bila shaka ni kituo cha kwanza cha trafiki kutoka lindi mjini kama unaelekea mtwara

1. Hivi afisa wa LATRA ana mamlaka ya kukagua leseni ya udereva?
2. Kwanini afisa wa LATRA anatembea na panga? Bila askari angejeruhi na kama angekuwa na bastola angeua huyu
3. Nguvu imetumika kuliko akili na busara na kukiuka kabisa maadili ya kazi kwa kumtisha mtu hadharani
4. Jeshi la polisi nalo limefanya uzembe na upendeleo kwa sababu mtu kumtisha silaha mwenzake hadharani ni kosa la jinai, polisi walitakiwa wamkamate mtumishi huyo wa latra na kumfikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria, kumuacha ni kujidharau, kwa sababu ingekuwa dereva amefanya hivyo wangemkamata

mwisho nashauri mtumishi huyo afukuzwe kazi kwa kuwa amekosa sifa ya kuwa mtumishi wa umma na afikishwe mahakamani kujibu mashtaka ya kumtishia mtu maisha kwa silaha
 
Tusishangae ila muda ni rafiki mzuri siku si nyingi utasikia kapandishwa cheo
 
Muajiri sio LATRA peke yake na kazi ameshafanya sehemu nyingi tu na bado kujenga na hata kununua magari hajafanya kwa hela za LATRA. LATRA ameingia mwaka jana tu akitokea Huawei, pia ameshafanya kazi sehemu nyingi kwa cv yake tu, amefanya Nabaki Africa, bandari kavu ya Ami, Alistair Logistics na Huawei then ndio akaenda LATRA mwaka jana.

Muajiri sio LATRA tu. Kama CV yako nzuri na una uzoefu na connection huwezi kosa kazi. Manase anavyo vyote hivyo. Hawezi kaa kijiweni muda mrefu hata kama akifukuzwa LATRA. Pia bado kijana tu hajavuka 33 nguvu za kupambana na maisha anazo.
Kuna atakayetaka kumuajiri tena kwa negative trend aliyopata. Labda ofisi za kipuuzi. Credible orgs haziwezi haribu reputation ya ofisi kwa kumwajiri mtu kama yeye
 
Back
Top Bottom